Monday, July 3, 2023

Siri ya baraka kwa baba wa kiroho

 *SIRI YA BABA WA KIROHO*

Utangulizi daka hii

BABA WA KIROHO......


1. Si kila aliyekuongoza “sala ya toba” ni baba wa kiroho.

Baba wa kiroho ni yule anayekulisha (anayekufanya ukue na usife kiroho), anakufanya umjue Mungu, ujue siri za Ufalme wa Mungu, na utembee ndani yake!

“Na kondoo zangu wanaijua sauti yangu”

(Yesu katika Yohana 10 ).

Ni mtu ambaye “sauti yake” inaeleweka kwako, na ina nguvu moyoni na maishani mwako!

Hata ukiwa mahali pa kukosea au kutenda yasiyo sawa, akilini mwako ukikumbuka somo lake au maonyo yake, unaghairi na kuahirisha, hata kama hayupo.

Sauti yake iko hai ndani yako hata asipokuwa nawe.

Mafundisho yake yako hai hata kama hayupo ulipo.


2. Mtu hawi baba wa kiroho kwa kukuombea ukaponywa au kufunguliwa.

“Waliponywa wengi wakati wa Yesu, walifunguliwa na kutendewa miujiza wengi… Lakini alipofufuka alikuwa na watoto wa kiroho 120 waliobaki CHUMBA CHA JUU hadi siku ya pentekoste… Japo alilisha wanaume zaidi ya 5000, bila kuhesabu wanawake na watoto, na makundi ya maelfu yalimfuata… Lakini alikuwa na watoto 120 tu waliokuwa wakitii MAELEKEZO YAKE NA KUFANYA ALICHOWAAGIZA (kukaa ghorofani mpaka wavikwe uweza)”

Idadi kubwa ya wanaokufuata, wanaofurahia mafundisho yako, walioponywa, waliotendewa miujiza na wewe, isikupotoshe ukadhani ni wanao wa kiroho!


3. Baba wa kiroho ni yule mtu ambaye “hachoshwi” na mapungufu, makosa, na matatizo yako, bali anaamini “UNA HAZINA KUBWA (He believes in you and your God given potentials)”

Petro ni mfano halisi wa Ubaba unavyotakiwa kuwa.

Ali-mess up mara nyingi sana, lakini Yesu alimwambia, “NINAKUOMBEA UKISHAVUKA UTAWAIMARISHA WENZAKO” … Badala ya kumtenga alimwambia, “JUU YAKO NA UFUNUO HUU ULIOTOA NITALIJENGA KANISA LANGU WALA MALANGO YA KUZIMU HAYATALISHINDA”

(Mathayo 16).

Bado alipokamatwa “ALIMKANA MARA TATU” lakini alipofufuka, mtu wa kwanza kumtaja alikuwa Petro… Alisema, “Enenda ukawaambie wote pamoja na PETRO kuwa nawatangulia Galilaya”

Baba hamchoki mwana… Kama umechokwa, jua hakika hapo ulipo umekosea, huyo si baba yako!

Si mnakumbuka HABARI YA MWANAMPOTEVU (Luka 15) ?

Baba hakumchoka mwanae mbali ya kukiuka utaratibu na kutoka nje ya “mfumo wa familia”… Aliporudi, BABA ALIKUWA WA KWANZA KUKIMBIA KUMLAKI MWANA MPOTEVU… Ikiwa na maana Baba wa kiroho hawezi kutulia na kukaa na amani ilhali hamuoni mwanae… Je, wewe huyo Baba yako anajali asipokuona? Anajali akiona kiroho chako kimeyumba na unapotea nje ya imani?

Anakutenga au usingizi unamuisha mpaka aone umerudi?

Baba wa kiroho huamini katika wewe no matter what happens!

“Yesu alikaa na Yuda na alijua anamuibia na ajenda mbaya dhidi yake lakini hakumfukuza… Aliamini ana kitu… Aliamini atazaa matunda… Japo haikuwa hivyo”


4. Baba wa kiroho ana muda (hutengeneza muda kwa ajili ya wanae hata kama unabana kiasi gani);

“Asiyewatunza wa kwake hasa wale wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko asiyeamini na ameikana imani”

(1Timotheo 5:8).

Makusanyiko ya kiroho ni FAMILIA ZA KIROHO.

Baba yeyote anakuwa na muda na wale wa nyumbani kwake.

Hauwezi kumwambia kitu au jambo halafu akasema yuko “busy” anajua wewe ni sehemu ya familia yake, ni sehemu ya utumishi wake, anawajibika kwako na atakutolea hesabu mbele za Mungu.

Kama hana muda kwa ajili yako ni baba wa namna gani huyu?

Biblia inasema Yesu alikuwa na “general message” (mahubiri ya jumla) kwa ajili ya makutano, lakini alikuwa na “private time” ya kuchanganua message kwa wanafunzi wake.

A father must have time for His children.


5. Baba wa kiroho lazima awe na kile unachokitaka ili ufanikiwe.

Ni makosa ya aina yake kwa kinda la mwewe kujichanganya na vifaranga vya kuku.

Sikia hii:

Siku moja Yesu alipiga injili ngumu kidogo na watu wakatawanyika na kuondoka/ wakasusia huduma yake… Wakawa wamebaki wanafunzi wake tu, akawageukia na kuwauliza, “Na ninyi mnataka kuondoka kama hawa?”

Petro akajibu kwa niaba ya wengine:

“Twende wapi? Kwako kuna maneno ya uzima”

Akiwa na maana:

“Tumekuchunguza sana, tumekuelewa sana… Tunajua tunachokihitaji kutupeleka NEXT LEVEL kiko kwako, twende wapi tuache PACKAGE zetu?”

Nisikilize:

Kama hana kile unachohitaji kukupeleka unakotaka kufika kiroho, achana naye.

“Wanafunzi wa Yohana walipomuona Yesu, na wakajua ana kile ambacho wanakitafuta, walimuacha wakamfuata Yesu”

(Yohana 1:35-39).

Usikae mahali ambapo ukiangalia kile unachokitafuta hakiko pale.

Mfano:

Unataka kuwa tajiri halafu mtumishi uliye naye anapinga masuala ya utajiri na mafanikio… Unapoteza muda hapo!

Unataka kuwa kiongozi mkubwa na mleta mageuzi; Halafu huyo mtumishi uliye chini yake hana hata team ya uongozi anayoiongoza (hana leadership structure)… Yeye ni kila kitu na anafanya yote… Hapa hapakufai!

Unaamini katika ishara, maajabu na miujiza na unataka Mungu akutumie kwa viwango vya ajabu… Lakini huyo uliye chini yake anapinga masuala ya miujiza, ishara na maajabu kiasi cha kusimama madhabahuni kupinga au kuwasema watumishi wanaotenda miujiza, ishara na maajabu, hakika hapo si kwako… Umechanganya!

Mfano unaamini kwenye utajiri:

Hakikisha baba yako wa kiroho naye ni mtu anayeamini katika utajiri.

Note:

Anaweza asiwe tajiri wa vitu bado, LAKINI anaamini katika utajiri, anafundisha kuhusu utajiri, anauzungumza utajiri na kuukataa umasikini, anaamini kwenye utele, mafanikio na anatarajia hayo tu na si upande wa pili.

Huyu ni mtu sahihi… Ni tajiri ambaye anasubiri muda tu utajiri uonekane nje!

Baba lazima awe na unachokitaka… Kwenye lugha yake… Kwenye mafundisho yake… Kwenye matarajio yake nakadhalika!

Nitaendelea….

Monday, March 7, 2022

AINA ZA UPENDO NA NABII ALPHA 1

 

AINA ZA UPENDO.



1.     UPENDO AGAPE - UPENDO WA MUNGU. (Godly Love) 
Agape ni aina ya upendo wa ki-Munguutendao kazi ndani ya mtu pasipo masharti yoyote au sababu yoyote. Ni upendo usioangalia hali ya
nje ya mtu. Ni  nguvu au uwezo wa mvuto wa Ki-Mungu utendao kazi ndani ya mtu, kumwonyesha mtu mwingine wema wa Mungu bila kujali hali yake yoyote. Ni upendo usio na sababu yoyote; unampenda mtu kwasababu tu unatakiwa kumpenda, nukta. Hakuna sababu nyingine. Kwa kingereza wanasema unconditional love.

Aina hii ya upendo; agape, ni kama ule aliotuonyesha Mungu kwa kutupenda. Neno la Mungu linasema ‘Mungu alitupenda tungali wenye dhambi’ (Rum 5:8) ili atuokoe na mauti itokanayo na uasi kwa Mungu. Imeandikwa katika biblia kwamba Mungu aliupenda ulimwengu wenye kila aina ya uovu, uasi na uchafu (Yoh 3:16, Rum 1:28-32) na akamtoka Kristo afe kwa ajili yetu, ili tuokolewe. Kwahiyo, alitupenda bila kujali uchafu na uasi tuliokuwa nao. Huo ndio upendo wa agape.

Mfano; Upendo wa Msamaria mwema. (Luka 10:29-37)
Msamaria mmoja alimkuta mtu mmoja asiyemfahamu, ameanguka barabarani kwasababu amepigwa ma majambazi. Huyu Msamaria aliamua kumsaidia huyu mhanga kwa kumsafisha vidonda vyake na kumchukua katika punda wake na kumpeleka katika nyumba ya wagonjwa na si hivyo tu, bali alijitolea hata kumlipia gharama za matibabu, kwa huyu mtu asiyemjua kabisa. Huu ndio upendo wa ki-Mumgu ndani ya mtu. Hauangalii hali ya nje wala hauna masharti; bali mtu huamua kuuachilia tu kwa mtu, kawasababu Mungu ameumimina ndani yake kwa ajili ya mtu/watu wengine.

Lakini tunasoma kuwa, kabla ya huyu Msamaria kupita pale njiani na kumwuoka huyu mhanga, walipita watu wengine wawili ambao wanaaminika kuwa ni watumishi wa Mungu. Kwanza alipita kuhani wa Mungu, lakini hakutaka kumsaidia, labda kwasababu hamjui. Neno linasema, alijipitisha kando akaenda zake bila kumsaidia. Kisha akapita Mlawi, amabye pia ni mtumishi wa Mungu, lakini naye pia alijipitisha kando kabisa, akaenda zake bila kutoa msaada kwa huyu mtu, kwasababu tu ni mtu asiyemfahamu. Pamoja na udini waliokuwa nao, tunasoma kuwa, hawakuweza kumsaidia huyu mtu aliyejeruhiwa vibaya na majambazi. Ni aidha, hawakuwa kabisa na upendo agape ndani yao, au hawakuuachilia upendo agape utoke, uhudumie mtu.
Lakini cha kushangaza, akaja Msamaria (amabye ni mtu wa kabila lisilohesabika kuwa la wacha Mungu) ndiye aliyeweza kuuruhusu upendo wa Mungu wa agape umhudumie yule mhanga wa ujambazi japo hamjui kabisa. Akamsafisha viWale watumishi wa Mungu walishindwa kuuruhusu upendo agape kutoka ndani yao, kumhudumia huyu mhanga. Hawa watumishi wa Mungu tuliowasoma, walitawaliwa na upendo wenye masharti na unaoangalia kwanza hali ya nje ya mtu. Upendo agape hautakiwii kuangalia hali ya nje ya mtu, wala hautakiwi kuwa na masharti yoyote. Ni upendo wa Mungu mwenyewe alitumiminia mioyoni mwetu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Rum 5:8)

Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa ki-Mungu (Agape).
       i.            Hauangalii hali ya mtu ya nje.
     ii.            Hauna masharti yoyote ya kupenda.
  iii.            Hauna kipimo au kiwango cha kupenda.
  iv.            Hauna mwisho au kikomo cha kupenda.


2.     UPENDO PHILEO – UPENDO WA KIRAFIKI. (Friendship Love)
Phileo ni upendo wa kirafiki. Huu ni pendo tofauti kidogo na upendo wa agape. Phileo ni upendo wenye sababu. Kiingereza wanasema ‘conditional love’. Ni upendo wenye sababu. Huu ndio upendo unaokuwepo kati ya marafiki. Phileo ni upendo unaoshikiliwa na kishikizo/kifungo cha ‘masharti’ fulani au ‘sababu’ fulani.  Mtu huwa rafiki wa mtu fulani ‘kwasababu’ fulani. Kuna mazingra yamewafanya watu fulani kuwa marafiki. Mazingira hayo au mashrti fulani yakivunjika kati yao, basi upendo ulio kati yao huyeyuka na urafiki wao huvunjika.

Aina hii ya upendo wa phileo ni kama ile ambayo Yesu anaisema katika kitabu cha Yohana 14:21,23. Anasema kwamba ‘mtu akinipenda, Baba atampenda, nami na Baba tutakuja kufanya makoa ndani yake’. Huu ni upendo tofauti na ule unaotajwa katika Yohana 3:16 na Warumi 5:8 ambao unasema Mungu alitupenda tungali wenye dhambi pasipo masharti yoyote. Yaani, kwa upendo agape, Mungu hakujali hali zetu za nje wala masharti yoyote. Lakini kwa upendo phileo, Mungu anaangalia kwanza kama mtu atatimiza masharti aliyoyaweka, kisha ndipo na yeye Mungu  anaachilia upendo phileo kwa mtu huyo, anakuwa rafiki yake.     

Mahali pengine Yesu alisema kwa wanafunzi wake kuwa ‘siwaiti ninyi tena watumwa bali marafiki.’ Hilo neno ‘tena’ linamaanisha kwamba, baada ya kukaa na wanafunzi wake kwa muda fulani, waliweza kufikia kiwango Fulani cha masharti alichokitaka Bwana, hata sasa wamefika katika ngazi wa kuwa marafiki wa Yesu na sio watumwa tena. Ndio maana imeandikwa pia katika kitabu cha Mithali 8:17 kuwa, ‘ninawapenda wale wanipendao …’ Hivyo phileo ni upendo wenye masharti na sababu.  Rafiki wa mtu husema ‘nampenda mtu Fulani, rafiki yangu kwasababu …’ Labda kwasababu wanasoma wote au kwasababu alimsaidia katika eneo fulani au kwasababu anatabia fulani au kwasababu wanatoka kijiji kimoja, n.k.

Mfano; Urafiki wa Jonathan na Daudi. (1Samweli 18:1-4)
Tunaona Jonathan anampenda sana Daudi baada ya kugundua vipawa vilivyo ndani ya Daudi. Tunasoma kwamba Daudi alikuwa anajua sana kupiga muziki (zeze) na kuimba zaburi kwa Mungu, kitu kilichofanya Daudi awe karibu sana na Mungu na kufunikwa na utukufu wa Mungu (upako). Hivyo Jonathan alimpenda sana Daudi kwasababu Daudi ana upako, uliomsaidia babake (mfalme) Sauli kufunguka kutoka katika nguvu za giza mara kwa mara. Hivyo Daudi akawa mtu wa msaada sana kwa familia ya Mfalme na katika serikali yake. Pasipo Daudi kuwepo karibu, mambo yote ya ofisi ya Mfalme na nyumba yake yanaharibika. Hicho kilimfanya Jonathan kumpenda sana Daudi. Na Daudi naye akampenda sana Jonathan kwasababu Jonathan alimpenda yeye kwanza, na pia kwasababu Jonathan alikuwa mototo wa mkuu wa nchi, mtoto wa Mfalme. Kukajengeka upendo mkubwa sana wa kirafiki kati ya Daudi na Jonathan, upendo Phileo. Hivyo, Phileo ni upendo wenye sababu au masharti.

Mfano Mwingine; Urafiki wa Yesu na Lazaro, Mariam na Martha. (Yohana 11:5, 35-36)
Japo biblia haielezi wazi wazi sababu za urafiki wao, lakini maandiko yanaonyesha wazi kuwa, uhusiano wa Yesu na kina Lazaro, Martha na Mariam, ulikuwa wa karibu sana ingawa hawakuwa ndugu zake wala wanatimu wake, bali marafiki zake. Angalia inavyoelezwa katika msatri wa 5; Neno la Mungu linasema, 5Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake (dada yake, ambaye ni Mariam) na Lazaro (kaka yao). Hebu jiulize, kwanini Roho Mtakatifu alimwongoza Yohana kutanguliza kumuandika Martha kwanza, kabla ya Lazaro au Mariam? Hii ni wazi kwamba, Yesu alikuwa na uhusiano wa kirafiki, tena wa karibu sana na hii familia, na hasa Martha (nionavyo mimi, kulingana na maandiko). Tuangalie zaidi mazingira haya kama ilivyoandikwa.

Yohana 11:20; Martha aliposikia kwamba hatimaye Yesu amefika msibani japo kwa kuchelewa, alikwenda kumlaki (kumpokea) lakini Mariam hakutoka, alibaki ndani. Unadhani kwanini? Baada ya kuongea na Yesu kwa muda Fulani, ndipo tunamuona Martha akiamua kwenda kumuita na Mariam, atoke ndani kwenda kumsalimia Yesu (mstari wa 28-32) Hii inaonyesha ukaribu uliokuwepo kati ya Yesu na Martha. Walikuwa na upendo mkubwa sana wa kirafiki, Phileo. Wasomaji wa Biblia nakumbuka hata wakati Yesu alipotembelea familia yao siku moja, ni Martha aliyeonyesha kumjali Yesu sana hata kujituma jikoni ili kumuandalia chakula, wakati Mariam hakuwa hata na pressure, bali alijiketisha miguuni pa Yesu kusikiliza Neno la Mungu. Japo badaye Martha alishushuliwa na Yesu, lakini ndiye aliyeonyesha kumjali (kum-care) Yesu zaidi, ndiye aliyeonyesha kusumbuka kwa ajili ya Yesu zaidi kuliko Mariam. Soma hii katika kitabu cha Luka 10:38-42.

Mimi naamini urafiki wa Martha kwa Yesu ulijengeka katika mazingira ya Martha kuthamini wema na baraka alizotendewa na Yesu, kwasababu utakumbuka kwamba, Martha ndiye yule mwanamke kahaba, ambaye siku moja alisikia injili katika mkutano ambao Yesu alikuwa anahubiri na akatubu dhambi zake, akatua mzigo wake na akamsamehewa kabisa uovu wake wote. Kwa furaha aliyokuwa nayo, akaenda nyumbani kwake, akachukua chupa ya perfume (marhamu) safi tena ya bei kubwa, akaja mahali ambapo Yesu alialikwa chakulani nyumbani kwa Farisayo aitwaye Simon.

Kwa utaratibu wa kiyahudi, ni mwiko kabisa mwanamke kuingia katika kikao cha wanaume wala kumgusa mwanaume bila utaratibu. Lakini kwa jinsi alivyokuwa na msukumo mkubwa moyoni, alishindwa kujizuia, akapenya mpaka mahali walipokuwa wamekaa chakulani, akasimama nyuma ya Yesu, akadondosha machozi katika miguu ya Yesu (kwasababu wayahudi hukaa chini kwenye zulia, na hii ina maana kwamba, Yesu alikuwa amekunja miguu kwa nyuma, ndio maana machozi yakamwangukia miguuni).  Ndipo alipoinama na kuvunja ile ya marhamu safi, nyumba yote ikajaa harufu nzuri. Martha akaipaka miguu ya Yesu mafuta yale mazuri, akachukua nywele zake ndefu na kuipangusa vizuuuri miguu ya Yesu. Mwisho akamalizia kwa kuibusu sana miguu ya Yesu mpaka mafarisayo wakakwazika na kunung’unika; lakini Yesu akamtetea Martha na kusema ‘mwacheni! Huyu amesamehewa dhambi nyingi kuliko ninyi, ndio maana amenipenda zaidi sana kuliko ninyi wote. Kwa habari kamili, soma Luka 7:36-50.

Pengine kwa sababu ya unyenyekevu wa Martha, ndipo upendo wa kirafiki (phileo) ulipozaliwa kati ya Yesu na Martha. Tunasoma hatimaye siku nyingine, Martha akamualika Yesu chakulani nyumbani kwao (Luka 10:38-42). Kitendo hicho kilimtabulisha Yesu kwa familia ya Lazaro. Biblia inasema Yesu akawapenda sana Martha, Mariam na Lazaro kirafiki - phileo (Yoh 11:1-5). Baada ya hapo, ndipo Lazaro alipougua sana hata Martha akatuma watu kwa Yesu kumwomba aje kumponya kaka yao ambaye pia ni rafiki sana wa Yesu. Mpaka Lazaro anakufa, Yesu alikuwa hajatokea.

Siku Yesu anafika, walikuwa wameshamzika Lazaro siku nne zilizopita, tayari ananuka, ameharibika. Habari ziliposikika kwamba Yesu amefika msibani, ni Martha peke yake aliyetoka kwenda kumlaki Yesu. Baada ya muda, Martha kuongea na Yesu kwa muda, ndipo akarudi ndani kwenda kumwita Mariam atoke kwenda kumsalimia Yesu kule nje. Mariam akatoka, naye alipomwona Yesu, alilia kwa uchungu sana na kujibwaga miguu pa yesu na kulalama ‘Yesu kama ungekuja mapema, kaka yetu asingekufa, ungemponya’. Yesu alipomwona Mariam analia, na wayahudi waliofuatana naye wanalia, Yesu akaugua sana moyoni, akafadhaika, na mstari wa 35 unasema “Yesu akalia machozi”. Hata wayahudi walipomuona Yesu analia, wakasema, “angalia jinsi alivyompenda (Lazaro)”. Hii inaonyesha kwamba, kulikuwa na upendo mkubwa sana wa kirafiki kati ya Yesu na Lazaro na dada zake. Baada ya hayo, tunaona kwamba Yesu alienda kumfufua rafiki yake Lazaro kutoka mautini.

Ndipo katika sura inayofuata (Yoh 12:1-8) baada ya wakati fulani kupita tangu Yesu amfufue Lazaro, tunaona familia ya Lazaro wanamwandalia Yesu karamu (sherehe au party), pengine ilikuwa ni ibada ya shukurani ya kufufuka kwa Lazaro. Siku hiyo, Martha akaanda chakula kizuri, halafu wote wakiwa wameketi chakulani, Martha akarudia tena kumvunjia Yesu kibweta cha marashi safi, kumbuka hii ni mara ya pili anamfanyia Yesu tendo hili la upendo. Martha akamvunjia Yesu kibweta kingine cha marashi (perfume) safi ya bei kubwa; akampaka tena Yesu marhamu safi kwa nywele zake. Ilikuwa ni ratili ya mafuta safi ya marhamu yenye thamani nyingi. Safari hii Yuda ndiye aliyekwazika (soma mwenyewe utajua sababu). Lakini tunamwona Yesu akimtetea tena Martha na kusema ‘mwacheni, kwa kitendo hiki, ananiandaa kwa maziko yangu’. Hii inatuonyesha jinsi Yesu alivyokuwa na urafiki wa Karibu sana na Martha. Martha alimpenda sana Yesu kwa wema usioelezeka, ambao Yesu alimtendea yeye na familia yake. Upendo uliokuwa katikati yao ni upendo phileo, Upendo wa kirafiki, upendo wenye sababu.

Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa kirafiki (Phileo).
       i.            Unaangalii hali ya mtu ya nje.
     ii.            Una masharti yoyote ya kupenda.
  iii.            Una kiwango au kipimo cha kupenda.
  iv.            Una mwisho au kikomo cha kupenda.


3.                             UPENDO EROS – UPENDO WA KIMAPENZI AU MAHABA. (Romantic/Sexual  Love)
Eros ni upendo wa kimapenzi au kimahaba unaokuwa kati ya watu fulani kusababisha watu hao kuwa na uhusiano wa kimapenzi (mahaba) kati yao. Kwa utaratibu wa Mungu na jamii zilizo ‘sawa sawa’, Eros ni aina ya upendo unaotakiwa kuwa kati ya watu wenye uhusiano wa ki-ndoa, yaani mtu mke na mume au kati ya watu wanaoelekea katika uhusiano wa ki-ndoa wa mume na mke. Aina zote za upendo zinahusisha moyo (nafsi) wa mtu, lakini Eros huwa na sifa ya kuwa na hisia zenye nguvu zaidi toka moyoni kuliko aina zingine zote za upendo. Eros  ni aina ya upendo wenye nguvu kali sana ya hisia za binadamu.

Tunaona Neno la Mungu (katika kitabu chake maalum kinachohusu mahaba ya wapenzi wawili) kitabu cha Wimbo Ulio Bora 8:6, Neno la Mungu  linasema kwamba Upendo (Eros) huwa na nguvu sana, kama mauti. Nguvu hiyo ya upendo huunganisha nafsi (fikra,hisia na maamuzi) za wapenzi wawili kuwa kitu kimoja katika fikra, hisia na maamuzi yao kwasababu ni upendo uliolenga kujenga ndoa nzuri na familia bora.

Mfano; Upendo wa Yakobo kwa Raheli. (Mwanzo 29:10-30)
Yakobo alipomkimbia kaka yake Esau, alikimbilia nchi ya mbali, nchi ya mama yake, kwa mjoba wake Labani. Labani alikuwa na binti wawili, mkubwa aliitwa Lea na mdogo waliitwa Raheli. Biblia inasema Lea alikuwa na macho mazito, yaani ukimwangalia, utadhani amelala, kumbe ndio anakuona. Na Raheli alikuwa na umbo zuri la mwili na sura nzuri ya usoni. Na Biblia inasema kwamba, Yakobo alimpenda Raheli. (Mwa 29:16-20). Labani akamwabia Yakobo atumike kuchunga wanyama wake kwa miaka saba (kama mahari), ndipo atampa Raheli kuwa mke wake. Yakobo akapendezwa na hilo, na akakubali kutumika na kuchapa kazi za Labani kwa miaka saba ili ampate Raheli. Na Neno la Mungu linasema, kwa jinsi Yakobo alivyompenda Raheli (kwa Eros - kimapenzi kuwa mke wake), alichapa kazi sana na kwa bidii kiasi kwamba, ile miaka saba ilionekana michache sana.

Hiyo ni nguvu ya upendo Eros. Yakobo alikamatwa katika upendo eros kwa Raheli. Ilikuwa kali sana. Nakwambia eros ina uwezo wa kumfanya mtu asione ugumu wa kazi, asione machungu, asione umbali wa mwendo, asione ukali wa jua, asione aibu wala woga mbele za watu wengine; Eros ina nguvu sana juu ya mtu mwenye nayo, hata kutawala utu wake wote. Eros ina nguvu ya fikra, hata kutawala mawazo ya mtu; eros ina nguvu ya hisia, hata kutawala kuhisi/kujisikia kwa mtu; eros ina nguvu ya maamuzi, hata kutawala matendo ya mtu kabisa. Unaweza ukamkuta kijana siku hizi ni msaaaafi kuliko tunavyomjua, kumbe ni kwasababu tayari amekamatwa kwa mwanamwali binti ‘Labani’ kama Yakobo alivyodakwa. Wee acha bwana! Tehetehetehetehe (kicheko).

Yakobo alijaa Raheli katika mawazo yake yote! Kila saa alibaki kumuwaza Raheli kwa muda mrefu; Yakobo alijaa Raheli katika hisia zake kiasi cha kutosikia machungu ya ile kazi na hata akaona miaka saba kwa si kitu kikubwa; Yakobo alijaa Raheli katika maamuzi yake hata kumfanya afanye kazi kwa nguvu kama trekta au katapila, ili tu kumpata Raheli. Raheli ndiye aliyekuwa nguvu na hamasa ya Yakobo kudamka alfajiri na mapema kwenda kulisha mifugo ya mjomba wake Labani.Upendo Eros una nguvu kama mauti. Wee acha tu.

Upendo wa kimapenzi au mahaba - Eros. (Romantic Love or Sexual Love)
Upendo wa kimapenzi huwa kati ya watu wawili wanaoelekea katika uhusiano wa kudumu wa mume na mke. Mungu hakukusudia upendo huu wa kimapenzi uwe wa kujaribu na kuacha, kwasababu eros ni upendo wenye nguvu sana ya hisia (nafsi), hivyo huathiri sana moyo, ufahamu, hisia za mtu na pengine hata afya ya mwili wa mtu kabisa, kama hatajua namna ya kuutawala ipasavyo. Hivyo Eros si upendo wa kuingia na kutoka utakavyo, kama mtu abadilishaye nguo (labda kama kuna cha kujifunza; nitaeleza baadaye maana ya hii sentensi), bali eros ni upendo uliokusudiwa kukaa kati ya watu wawili tu, kwa maisha yao yote yaliyobaki hapa duniani (permanently for life), sio kuingia na kutoka, kwasababu una uwezo wa kujeruhi sana moyo wa mtu na kumwachia vidonda na makovu ya moyoni. Tena nasisitiza, eros ni kwa ajili ya watu wawili tu, na sio watatu au zaidi, laa sivyo huo hautakuwa upendo, bali tamaa (lust and not love). Na tena eros, ni upendo kwa ajili ya watu wawili wa jinsia tofauti tu, na sio jinsia moja.


Mfano; Upendo wa Isaka kwa mkewe Rebecca. (Mwa 26:1-11)
Isaka alikuwa akiishi katika nchi ya Wafilisti. Watu wale wakamwona Rebeka, wakavutiwa na uzuri wake, hata wakamtamani. Wakamuuliza Isaka, ‘ee bwana ee, huyu msichana tunayemwona katika boma lako na wakati mwingine unaambatana naye, ni nani kwako? Isaka akaogopa kusema ni mke wake, kwa maana wangeweza kumuua ili wamchukue Rebeka, kwa jinsi alivyokuwa mzuri wa kuvutia. Isaka akasema ‘ni dada yangu’. Basi wakamwacha. Lakini kumbe wale watu walitumwa na Mfalme Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, ili kupeleleza na kujua uhusiano wao, kwasababu Mfalme alivutiwa sana na uzuri wa Rebeka, akataka kumuao.

Siku moja, Mfalme Abimeleki alipokuwa akiptia pita mitaani, akakatiza mtaa ambao nyumba ya Isaka ilikuwepo. Biblia inasema  “8Abimeleki Mfalme akachungulia dirishani, akawona Isaka akicheza-cheza na Rebeka mkewe” (kimahaba/romantically). Mfalme Abimeleki akamwita Isaka, akamwambia, kwa jinsi nilivyowaona mnchezeana vile, haaaaata! lazima huyu ni mkeo, huwezi kucheza-cheza vile na dadako, sasaaaa, mbona uliniambia kuwa huyu ni ndugu yako (dadako)? Isaka akajibu ‘niliogopa nisije nikauwawa kwa ajili yake’. Basi Abimeleki akamlaumu Isaka, kwa kusema, mtu mmoja wetu angelala na Rebeka bila kufikiri ni mkeo, kwasababu ulisema mwenyewe ni dadako. Ndipo Mfalme akaamuru watu wote wasimguse Isaka wala mkewe Rebeka; akasema “11amgusaye mtu huyu  au mkewe, lazima atauawa”.

Baadhi ya Dalili na Sifa za Upendo wa Kimapenzi (mahaba) - Eros (Romantic Love).
1)    Mvuto kwa Haiba yake na kuchukuliana nayo. (Mwonekano na tabia).
2)    Kukaa mawazoni kwa mtu anayependa. (Kujaa moyoni)
3)    Shauku kubwa ya kuwa pamoja kila wakati. (Kuambatana)
4)    Heshima kubwa kwa mtu apendwae (Utii na Uaminifu)
5)    Kumjali na kumtanguliza mtu apendwae. (Kipaumbele)
6)    Zawadi na gharama kwa mtu apemdwae. (Kujitoa/Sacrifice)
7)    Furaha na Amani kutawala moyoni. (Kuridhika)

Baadhi ya maandiko yanayotaja upendo eros. (Upendo wa kimapenzi)
(Waefeso 5:25.) Enyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake. (Mhubiri 9:8-9.) 8Mavazi yako yawe meupe siku zote; wala kichwa chako kisikose marhamu. 9Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili uliyopewa chini ya jua. (Wimbo Ulio Bora 7:1-10) 10Mimi ni wake mpendwa (mpenzi) wangu na shauku yake ni juu yangu. (Wimbo Ulio Bora 4:1-7) 1Tazama, u mzuri mpenzi wangu, u mzuri, macho yako…nywele zako… 7Mpenzi wangu u mzuri pia, wala ndani yako hamna hila.

4.                             UPENDO STORGE – UPENDO WA KIFAMILIA. (Family Love)
Upendo storge ni upendo wa kifamilia, ni upendo unaotokana na damu moja ya undugu. Ndugu wa damu moja hata kama hawapatani au wemegombana, bado ndani yao kuna upendo wa kindugu. Fikiria; mtu na mdogo wake wakiwa wamegombana sana na kutupiana mito ya makochi na vitabu vyote vya kwenye shelfu za kabati, baadaye, mmoja akimkuta ndugu yake anaonewa au anagombana au anapigwa na muuza machungwa wa mtaani, huyu ndugu yake kwa vyovyote ataguswa tu, ataonyesha kujali tu au anaweza hata kuweka tofauti zao pembeni na kuingilia kumsaidia. Msukumo huo au mvuto huo, ni mvuto unaotokana na viini vya upendo wa kifamilia unaowafungamanisha watu wa damu ya familia moja au ukoo mmoja.

Mfano; Upendo wa Musa kwa Mwebrania mwenzake. (Kutoka 2:11-12)
Musa aliona mwebrania mwenzake akipigwa na mmrisri. Kwasababu na yeye alikuwa mwembrania, ndani yake kukachemka mvuto wa kindugu, kuliwaka moto wa upendo wa kifamilia. Akainuka na kwenda kumpigania. Musa akamuua yule mmisri na akamwokoa yule mwebrania. Japo hawajazaliwa tumbo moja, lakini waote wana damu za kiebrania, na viini vile vya asili yao, viliwafungamanisha katika pendo la kindugu (kifamilia) hata wakasaidiana. Upendo huo ulimnyima Musa kujikausha wakati ndugu yake anaonewa, anapigwa na anataka kuuwawa. Si ajabu wakati anayatazama yale maonezi kwa mbali, hata alipojidai kuondoka bila kumsaidia, yamkini miguu yake ilishindwa kutembea, nafsi yake ikakamatwa kurudi kumsaidia ndugu yake. Hiyo ni nguvu ya upendo storge, upendo wa kindugu.

Mfano; Upendo wa Baba kwa Mwana mpotevu. (Luka 15:11-32)
Tunasoma jinsi mwana huyu mdogo wa baba tajiri alivyoomba sehemu ya urithi wake na kutokomea nchi za mbali kwenda kutafuta maisha. Lakini maandiko yanaeleza jinsi alivyovutwa na dunia na kuharibu mtaji wake wote wa mali alizopewa na babaye.neno la Mungu linasema, kijana huyu alijiingiza katika anasa za dunia na mwishowe alifilisika kabisa. Baada ya muda wa mahangaiko alipata kibarua cha kulisha nguruwe wa mtu mmoja. Hali yake ya kimaisha ilikuwa mbaya sana hata akatamani kula chakula cha nguruwe. Lakini akili zikamrudia na akaona anateseka bure wakati kule kwao, baba yake ana watumishi wanaokula vizuri kuliko yeye. Ndipo alipoamua kurudi nyumbani kwa toba. Kwa hali ya mzazi wa kawaida, huyu kijana angepewa adhabu kali sana; lakini kinyume chake, baba yake mzazi alimpokea kwa shangwe na furaha. Akamvika na mavazi mazuri, akamchinjia na ng’ombe mnono na kumfanyia sherehe kuuuubwa ya kufana. Hiyo ni nguvu ya upendo wa kindugu. Japo alichofanya si cha kupendeza, lakini nguvu ya upendo wa kindugu unaweza kufunika uovu wooooote uliotendwa na ndugu yenu. Watu wanaweza kuamua kusamehe au kufumbia macho makosa yaliyotendwa na ndugu yao kwasababu ya nguvu ya upendo wa kindugu, unaitwa kwa kiebraia storge.

Upendo wa kindugu, storge  unafanana kwa sehemu na ule upendo wa ki-Mungu wa agape.
       i.            Hauangalii hali ya nje ya mtu.
     ii.            Hauna masharti ya kupendwa.
  iii.            Hauna kikomo au mwisho wa kupendwa.

Tofauti yake moja kubwa na upendo wa agape ni kwamba, upendo wa kindugu una kiwango au kipimo cho kupenda. Ndugu wanapendana lakini kwa viwango tofauti; upendo wao haulingani. Tofauti ningine kubwa ni kwamba, kwasababu huu upendo wa kindugu unatokana na binadamu, basi ni lazima hautakosa madhaifu mengi. Ingawa ndugu wanaweza kuwekeana masharti fulani fulani ya kitabia ili kuweka uelewano kati yao, hata masharti hayo yakivunjwa, na baadhi ya ndugu wakasema wamefika mwisho, hawataki tena kumsaidia, lakini mwishoni, baada ya hasira kutulia na muda kupita, utaona ndugu wanainuka, wanajikongoja, kwenda kumsaidia tu ndugu yao. Hiyo ndiyo nguvu ya upendo wa kindugu au kifamilia.


NAMNA YA KUPATA MWENZI MZURI WA MAISHA.
(HOW TO FIND/GET A GOOD MARRIAGE PARTNER)
*Mithali 19:14, 21

1.     Mweleze Mungu vizuri, zile haja za moyo wako. (*Fil 4:6-7)
Mungu ameahidi kuwa atakupa mtu wa kufanana na wewe (Mwa 2:18). Kwa hiyo ni muhmusana ujijue wewe ukoje, kisha ndipo utaweza kumweleza Mungu na kumwomba akupe mtu wa haja ya moyo wako. Hivyo ni muhiu sana kujijua, kujitambua na kujielewa kwa jinsi ulivyo na ni aina gain ya watu ambao wewe unaendana nao (mnaiva). Hii ni kwasababu, watu tuko tofauti. Unaweza kuishi na mtu yoyote duniani, lakini hutaweza kuishi vizuri na kila mtu. Maisha mazuri yanakuja  kwa kukutana na mtu ambaye mnaelewana na mnaendana. Ndio maana Mungu alimwambia Adam kwamba, mwenzi wako wa maisha, atafanana na wewe.

Usimfiche Mungu moyo wako. Kumbuka, yeye ni Baba yetu na sisi tu watoto wake vipenzi. Hivyo Mungu anaheshimu sana haja za moo wako ambazo zitakupa wewe furaha ya maisha. Mathayo 7:7-11 inasema, Ombeni nanyi mtapewa. Mwana akiomba mkate, hapewi jiwe, akiomba samaki, hapewi nyoka. Anapewa alichoomba. Lakini pia ni muhimu ujue kwamba, mwana akiomba mkate, hapewi jiwe, lakini pia hapewi keki hata kama ndani ya nyumba kuna keki. Mwana akiomba samaki, hapewi nyoka, lakini pia hapewi kuku, hata kama ndani ya nyumba kuna kuku wengi. Hii ni kwasababu, Mungu anaheshimu sana matakwa na mahitaji ya watoto wake, maana anapenda kuiona furaha ya watoto wake. Soma Zab 145:17-18 na Isa 45:11 uone. Pia  1Kor 7:39.

Maombi yako ya bidii yatampa Mungu kumchonga, kumuandaa. Kila mtu huumbwa na Mungu vizuri, lakini Neno linasema kwamba, dhambi iliharibu utaratibu mwingi sana wa Mungu duniani. Soma Mwa 6:5-8 na Rum 1:28-32. Dhambi imevuruga mambo mengi sana, nafsi za watu wengi ziko corrupted (zimeharibiwa na kuvurugwa) na dhambi. kwahiyo, maombi yako yatamfanya Mungu kuanza kumshughulikia na kumtengeneza huyo mwenzi wako, popote alipo duniani. Na Biblia inasema kwamba, maombi ya mwenye haki yanafaa sana, mt akiomba kwa bidii. Soma  Yak :16,  Luk 18:1,  Kol 4:2.
2.     Mwombe Mungu akuonyeshe au akukutanishe na mwenzi wako. (*Yer 33:3)
Kila mmoja wetu ambaye Mungu amempangia kuwa na mwenzi, ana mwenzi huyo mahali Fulani hapa duniani. Pointi ya kwanza inahusu kufanya maombi ya kumwmba Mungu kumchonga na kumfinyanga huyo mwenzi wako popote alipo. Point hii ya pili inahusu kumwomba Mungu kusababisha mazingira ambayo yatawakutanisha na mtatambuana baada ya kupata ufahamu wa Mungu kwamba ‘you belong together’ yaani mnaendana, mnafanana, mnafaana na hivyo mnaweza kuishi pamoja vizuri. Hiyo ndiyo maana halisi ya kufunuliwa au kuonyeshwa. Japo Mungu anaweza kukupa maono katika ndoto au katika maombi, lakini si lazima iwe hivyo. Si kila mtu anaweza kupata maono kuhusu mwenzi wake. Soma Efe 1:15-19, Zab 32:8,  Isa 43:26,  Isa 45:11

3.     Tengeneza marafiki. (*Mith 18:24, Mith 17:17)
Watu wengi humwomba Mungu kwa uaminifu sana ili wapate mwenzi wa maisha. Lakini wanafanya makosa ya kujifungia katika kisiwa cha upekee. Ni ngumu sana kuonekana na kujulikana tabia na utu wako wa ndani kama hutachangamana na jumuiya za marafiki. Mungu ndiye chanzo cha urafiki. Hata Yesu alikuwa na marafiki wa kiume na wa kike pia. (Yoh 11:5).  Jithidi kufanya marafiki mbalimbali ila mwombe Mungu akupe marafiki wazuri.

Kuna aina nyingi za marafiki; Kuna marafiki wa mbali (peer friends), marafiki wa kawaida (casual friends), marafiki wa karibu (close friends or best friends) na marafiki wa moyoni (intimate friends). Unaweza ukawa na marafiki wa kawaida wengi uwezavyo, haina shida. Lakini unahitaji marafiki wa karibu wachache (Mith 18:24). Katika wingu kubwa la marafiki zako, Mungu ataanza kukuongoza nawe utawachuja na kuwaweka katika ngazi hizo mbalimbali. Katika hali ya kawaida, Mungu atakukutanisha na mwenzi wako wa maisha kati ya marafiki zako na watu unaofahamiana nao. Kwa maombi unayofanya, Mungu atasababisha mkutane, mfahamiane, mtambuane na mpatane.




4.     Thibitisha moyo wako kwamba unampenda kikweli.  (*Mhubiri 9:8-9a)
Kadri unavyoendelea na maisha ya uaminifu katika wokovu, maombi, kujifunza neno la Mungu na kumtumikia Mungu kwa namna mbalimbali, Mungu atasababisha ukutane na mtu anayefanana sana na haja za moyo wako kuhusu mwenzi wa maisha. Utahitaji usikivu mkubwa wa rohoni ili kuambua ni aina gani ya upendo unaingia moyoni mwako kuelekea kwake (kwasababu kuna aina nne za upendo). Upendo wa Mungu, Upendo wa Kindugu, Upendo wa Kirafiki, Upendo wa Kimapenzi (mahaba).

Katika ya watu unaofahmiana nao, yupo mmoja ambaye atakuwa wa tofauti sana ndani yako. Mungu atampa kuonekana watofauti sana kuliko wengine wote wanaokuzunguka. Hivyo kabla ya kwenda kusema naye na kumshirikisha uonavyo wewe moyoni mwako, thibitisha kimaombi tena na tena kwamba ndani yako kuna upendo wa kweli kwa ajli yake.  Mk 5:25 – (30) – 34; inasema, wengi walimgusa Yesu na kumsukuma-sukuma, lakini ni mmoja tu ambaye atakuwa na mguso wa tofauti katika moyo wako.

ISHARA ZA KUTAMBUA (UPENDO WA) PENZI LA KWELI.
1.     Mtu huyo atakamata umakini wako na atakuvutia (attention).
2.     Atajaa moyoni na mwazoni mwako kuliko kawaida na wengine.
3.     Utatamani sana uwepo wake wakati wote (kuwa naye).
4.     Utapenda kuwasiliana naye mara kwa mara (kama hamko wote).
5.     Utakuwa na moyo wa kumjali, wema, zawadi na kujitoa sana kwa ajili yake.
6.     Utakuwa na heshima ya juu sana, adabu, utii na uaminifu sana kwake.
7.     Utakuwa na maneno mazuri, maneno laini, na maneno ya upendo kwake.
8.     Utakuwa na moyo/uwezo wa kumvumilia au kuchukuliana naye vile alivyo.
9.     Utakuwa na hamu ya kumgusa au kumshika kwa upendo (si tamaa).
10.                        Utakuwa na moyo na utayari wa kumlinda na kumhifadhi.
11.                        Uhusiano wenu utapendeza mbele za watu wengi (si lazima wote)
12.                        Utakuwa na amani na furaha ya ajabu moyoni mwako/mwenu.


Mungu alisema kwa mkono wa Mtume Paulo kuuelezea Upendo kwa namna hii;
1 Cor 13 : 4-8(a)
*         Upendo huvumilia/subira  (Love is patient)
*         Upendo hufadhili/hufanya wema (Love is kind)
*         Upendo hauna husuda (Love doesn’t Envy)
*         Upendo haujivuni (Love is not proud)
*         Upendo haukosi adabu (Love is not rude)
*         Upendo hauna ubinafsi (Love is not selfish)
*         Upendo hauna uchungu (Love is not easily angered)
*         Upendo hauhesabu mabaya (Love doesn’t count wrongs)
*         Upendo haufurahii uovu (Love doesn’t rejoice with evil)
*         Upendo hufurahia ukweli (Love rejoices in truth)
*         Upendo unalinda (love always protects)
*         Upendo huamini yote (Love always trusts)
*         Upendo hutumaini (Love always hopes)
*         Upendo hustahimili (Love always perseveres)

5.  Omba ushauri kwa watu wanaokujua/wanaomjua huyo umpendaye.
2Kor 13:1; Zab 73:24; Mith 15:22
Ushauri kutoka kwa watu werevu wanaomjua Mungu na wanaowajua ninyi wawili utakuhibitishia kwamba ulichsikia mooni juu ya huyo mtu ni sahihi. Wakati mwingi (si wakati wote) watu wa pembeni huwa na uwezo wa kuona vizuri zaidi mambo kuliko watu mlio ndani. Wanaweza kuona vitu ambavyo ninyi mlio ndani ya urafiki hamuoni bado.washauri wanaweza kutumiwa na Mungu kuthibitisha mawazo uliyo nayo na mipango uliyonayo. Mashauri ya watu yanaweza kukusaidia kufanya maamuzi magumu nay a muhimu. (Math 18:16;   1Tim 5:19;   Ebr 10:28)

Mwombe Mungu akuongoze kwa watu wazuri wenye hekina watakaokushauri. Lakini la muhimu kuliko vyote ni wewe mhusika kubaki na uamuzi wa mwisho. Washauri wabaki washauri na sii waamuzi; wewe ndiwe uwe mwamuzi wa mwisho. Ni muhimu kupima ushauri wote unaopewa kwa maombi na uongozi wa Mungu. Wakati mwingine, Mungu anaweza kukuongoza kitu ambacho hakuna mtu mwingine anakiona ukionavyo wewe. Neno la Mungu linasema, amani ya Kristo itakusaidia kufanya maamuzi mazuri.
Soma; Fil 4:6-7, Kol 3:15 na Isa 55:12

6.  Mwendee na Useme naye kwa hekima.   (*Wimbo 3:1-4)
Baada ya maombi na subira, Mungu akuongoze kusema naye kwa wakati utakaoongozwa na Mungu. Uwe jasiri na muwazi. Lakini usemi wako uwe wa kawaida (simple). Usichague maneno magumu wala misamiati wala mafumbo. Uwe wazi na wa kawaida. Usitumie maneno ya kiroho saaaaana ili kumtisha au kumfunga mtoto wa watu. Kwa mfano; usitumie maneno kama, ‘Mungu ameniambia’ au ‘Asema Bwana wa majeshi’ maneno kama haya, yanamfunga mtu kusema “ndiyo” (kama atashitushwa nayo na kuogopa) lakini kama ni mtu jasiri na hajakupenda/hajakukubali, mtapambana. Huo sasa si mwelekeo mzuri.

Kijana mmoja alipoataliwa, akaanza kuporomosha maneno makali mfano ‘nakuzungushia ukuta wa moto, hutaolewa na mtu mwingine ila mimi, na ukikataa, Bwana atakutandika’. Hii si hekima ya Mungu. Mungu hatumii nguvu bwana. Ikiwa kwenda mbinguni tuu, Mungu halazimishi watu, Je itakuwa ndoa? Wewe ukishasema mameno rahisi; Kwa mfano; ‘nimeomba kwa muda, na hivi ndivyo ninavyosikia moyoni mwangu kwamba, nakupenda sana, na ikiwa itampendeza Mungu na wewe pia, basi uwe mwenzi wangu wamaisha’. Ukishamwambia maneno hayo rahisi (au yanayofanana na hayo) amini kwamba kama ni mpango wa Mungu muwe wote maishani, maombi yako na neema ya Mungu vitamsaidia kufanya uamuzi mzuri kwa ajili yenu wawili. Unaweza kupata jibu la ‘ndiyo’ au ‘hapana’ au ‘subiri’. Mtu wa Mungu huongozwa na Mungu, halazimishi wala hakasiriki ovyo kwa kitu kama hiki. Maana yangu ni kwamba, hauhitaji kutumia nguu ya mwili wala akili (kuwaza sana). Baada ya kuongea na kutua mzigo wako kwake, pumzika naumwachie Mungu kumalizia kazi.
    
Mkumbuke Mariam mama wa Yesu, japo alijua ana mchumba, lakini malaika aliposema naye kuhusu kupata ujauzito kabla ya ndoa, hakukurupuka mbio kwenda kwa Yusufu na kuanza kumwelesha, bali alimwachia Mungu kuongea na Yusufu. Mimi binafsi naamini Mariam alimwombea sana Yusufu. Lakini kwasababu ulikiwa mpango wa Mungu wa kuwa pamoja maishani, Mungu hakuongea na Mariam peke yake; aliongea na Yusifu pia. Mungu ni Mungu wa utaratibu, usimfundishe kazi. Jifunze kupumzika ndani ya Mungu na kutokuwa na wasiwasi. Huko ndiko kukua kiroho. Amani ya Kristo ikuhifadhi.

7.    Thibitisha uhusiano wako/wenu (kiofisi).  (*Wimbo 3:4)
Baada ya kuongea na kulitafakari pamoja kwa muda mtakaoona unatosha au unafaa, ni muhimu sana sasa mpelekane mbele, katika mamlaka zenu za kifamilia na kikanisa. Uhusiano mzuri usiwe wa mafichoni. Tunaona huyu mpenzi katika kitabu cha Wimbo anasema, anataka kumtafuta mpenzi wake, amshike mkono, wapelekane kwa wazazi. Huo ndio utaratibu mzuri kibiblia. Familia na kanisa watawasaidia kufuata taratibu za kiutamaduni na kiroho ili mhalalishwe kuwa mume na mke. Ndipo ndugu na marafiki mtawashirikisha mipango yote ili kuandaa harusi na makazi.  

Saturday, October 12, 2019

*NGUVU YA MAFUTA YA KINABII*
SHULE YA UNABII KWA MANABII
NA.ALPHA 1 DERICDADY
       SON OF ALPHA AND OMEGA

   Nimhimu kujua mafuta yanamaanisha nini katika ofisi ya kinabii,samweli alimtia mafuta sauli kuwa mfalme na samweli Huyo huyo alimtia mafuta Daudi kwanini hakumuwekea mikono akamtia mafuta?

   Mafuta kibiblia yamebeba uweza wa utendaji na kufungua milango iliyozuiliwa kwa lugha nyepesi mafuta ilikuwa ni steppingstone kwa Sauli na Daudi,yalifungua mlango wao kuwa watawala ndiposa nachelea kusema hata Yehu ilimpasa apakwe mafuta na Nabii wa Bwana ili awe Nabii mafuta yanayotoka kwa Nabii ni uweza wa ki Mungu wapekee kufungua milango iliyozuiliwa ndio maana kwa *kutiwa mafuta nira huondoka* nira ilimzuia Daudi kuja kuwa Mfalme ndio màana Daudi akampaka mafuta,samweli alifungua milango juu ya Daudi kwa mafuta kwanini Yale mafuta asipakwe na Baba yake akapakwa na Nabii samweli nikwasababu Baba wa samweli hakuwa na nguvu ya kinabii ambayo nguvu ya kinabii ni sheria maana kinywa cha Nabii kimejaa maneno ya kutunga sheria za Rohoni samweli alikuwa anatengeneza sheria Daudi kuwa mfalme wa israel.

   Baba wa Daudi akampaka mafuta Daudi angeishia kuwa kiongozi wa familia yake tu lakini asingewatawala Israel yote.
   Mafuta ya kinabii ndio ufunguo wa Daudi kuwa mfalme,Nabii akiwa vizuri katika ofisi yake ya kinabii kila jambo linawezekana na ifahamike iko Tofauti kati ya Nabii na mwonaji Nabii na Mwenye karama ya kinabii

Mwonaji kibiblia anafahamika kama *Hozeh au Roeh* yaani mwonaji ambapo huyu kazi yake kuu ni kuona tu na awezi kutoa massage from God yeye ni miwani itazamayo pekee wakati Nabii anafahamika kama *Ish ha el-rohim* yaani Mtu wa Mungu ambaye yeye kazi yake kuu ni kuchukua ujumbe wa Mungu na kuleta kwa wanadamu ikumbukwe Nabii atumwi na wanadamu Bali na Mungu pekee Nabii anafahamika kama Nabi kwa kiarabu na kwa kiratini ni *prophemi* ambaye ndani yake anakuwa na upako wa aina 3
1.DUNAMIST(uweza wa kutenda miujiza na ishara)
2.EXSION (KAVASH AND SHAMAR)kumiliki na kutawala
3.EPIKAIZO(overshadow anointing)
 Ambapo Nabii au nabi anakuwa yeye anauwezo wa kumuweka wakfu mtu kutawala anakuwa na uwezo wa kuzima nguvu ya vita kwa kutumia Epikaizo

    Tunaona kwa habari ya Musa alikuwa na epikaizo power mpaka Mungu anamkumbusha musa musa panda Mlimani musa anauliza Mungu anajibu ili ukafe,kwasababu ya Too much anointing anakumbushwa mda wake wa kufa,Elisha inabidi Mungu amtumie gari la moto sababu ya epikaizo,inabidi Bwana amtwae Enoko sababu ya Too much power.

Nabii akiijua ofisi yake anakuwa na uweza wa kutenda mambo Mkuu chini ya jua na mwonaji yeye anaweza ona kitu asikusaidie akaishia kusema umefungwa tu kichawi kwisha ila Nabii uwa na majibu maana ametumwa na Mungu.

  Na itambulike Mwenye karama tu ya kinabii ni mtu kama mbashiri yaani upata neno la hekima au maarifa wakati wa service peke yake na baada ya hapo uwa anabaki kama yeye tu wakawaida.

   Nabii sio mtu wa fashion kimatendo Bali huangalia sana kusudi la Mungu kulitimiza pekee.


*MAFUTA YA KINABII HUTOKA KWA NABII NA KWENDA KWA NABII*
   Nabii Mwenye mafuta ya kinabii Siku zote uwa na Chuo cha kinabii ambacho mafuta utoka kwa Nabii na kutengeneza wana wa kinabii ambao kesho uwa manabii badara yake kama Eliya na Elisha na Musa na Joshua mafuta hutoka kwa Baba na kwenda kwa mwana wa kinabii,ili uwe nabii kuna mambo mawili ama umezaliwa Nabii au umejifunza unabii kama unajifunza sababu unayo karama kuna lazima baba ambaye ni Nabii akupake mafuta ya kinabii ili uzidi kuinuliwa kinabii na kama ulizaliwa wewe ni Nabii inatakiwa uwe na mwangalizi tu maaana wewe vyote unajua tayari uitaji mwalimu


*LINDA KARAMA YAKO KWA NGUVU YA MAFUTA YA OFISI YAKO*

*Alpha 1 prophet dericdady*
0679008354
dericglory@gmail.com
Uliza maswali

Wednesday, September 12, 2018

*FAHAMU NGUVU ZAKO ZA KUZALIWA KWA UFUNUO WA ROHO MTAKATIFU*

Kumb 33:1-9, Mwanzo 49:3-7, 1Kor 2:10
Kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu Aliye Hai, ameumbwa na nguvu maalumu kutoka mbinguni, ambayo ni mtaji wake maalumu; kiroho, kijamii na kiuchumi.

Mwanzo 49:3
Reubeni u mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na nguvu.

*1. MZALIWA WA KWANZA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amebeba nguvu nyingi za familia.
ii. Amebeba Baraka za aina mbalimbali za wadogo zake.
iii. Amebeba nguvu ya upendo ndani ya familia.
iv. Mzaliwa wa kwanza ni lango, Zab 24:7-9, ambapo Baraka zote za familia kutoka mbinguni zinapitia kwake na kuwafikia wadogo zake wote.
v. Amebeba ustawi wa familia kiroho na kimwili.

*2. MTOTO WA PILI KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Ni m’beba neno la uzima.
ii. Kipawa cha ualimu kinakaa vizuri sana ndani yake.
iii. Amepewa neno la uzima la kusaidia kanisa familia na nchi.

*3. MTOTO WA TATU KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Ni mtawala katika ulimwengu wa roho na wa mwili.
ii. Ni mtunga sheria popote atakapokuwa anaishi, anasoma au anafanya kazi.
iii. Amepewa mamlaka ya kusimamia jamii, kuiongoza na kuitawala.
iv. Anafaa kuwa mwanasheria au kiongozi popote aendapo.

*4. MTOTO WA NNE KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amepewa neema ya kumiliki utajiri wa nchi.
ii. Kama akijitambua na kusimama katika zamu yake, ajue amepewa neema na nguvu ya kuutawala uchumi vizuri sana.
iii. Amepewa nguvu ya kumiliki utajiri wa mbingu na dunia.

*5. MTOTO WA TANO KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amepewa neema ya kushinda changamoto.
ii. Amepewa stamina ya kushindana na majaribu kwa asili.
iii. Amepewa neema ya kutumika na upako wa juu sana, kama akiokoka na kujitambua, na kusimama katika zamu yake.

*6. MTOTO WA SITA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
Ni mtu wa ujuzi, na talanta. Na Amepewa nguvu ya ubunifu wa pekee.

*7. MTOTO WA SABA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amebeba uheri wa Mungu Mtakatifu.
ii. Yeye ni jubilee, yaani maachilio.
iii. Usithubutu kushindana naye maana hautafanikiwa.
iv. Ukimshitaki hauwezi kufanikiwa.
v. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.
vi. Anafaa kuwa hakimu kama ataamua kuichukua taaluma hii.
vii. Ukipata kesi yoyote na akakusindikiza ni lazima utashinda, maana utu wake wa ndani ameumbiwa neema hii.

*8. MTOTO WA NANE KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amebeba nguvu ya utumishi.
ii. Amepewa neema ya kusaidia wengi kiuchumi, kiroho na kijamii, kama akijitambua na kusimama katika zamu yake.
iii. Akiokakoka na kuwa mtumishi kanisa lolote, atalisaidia sana kustawi, kwa kuwa ni mtu wa kutegemewa sana.
iv. Amepewa neema ya kuwa nguzo.
v. Ukimtambua katika kanisa lako na kumthamini, na kumtumia vizuri, utafanikiwa sana.

*9. MTOTO WA TISA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Ni m’beba karama.
ii. Akipokea kipawa anakitunza sana kwa muda mrefu.
iii. Amepewa nguvu ya umoja.
iv. Ni mtu anaweza kuinganisha jamii, nchi au familia na kuleta mshikamano.
v. Anafaa kuwa mwanasiasa endapo akijitambua na kusimama katika nafasi yake aliyokirimiwa na mungu.

*10. MTOTO WA KUMI KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Yeye ni msamaha.
ii. Amekirimiwa nguvu ya msamaha.
iii. Amepewa uwezo wa kusuluhisha migogoro kwa ufanisi wa hali ya juu sana.
iv. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.

*11. MTOTO WA KUMI NA MOJA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
Ni faraja kwa familia.
Kuna wakati anapata tatizo la kukataliwa, lakini ni mvumilivu sana.
Mkikaa naye kwa upendo mtabarikiwa sana.

*JiULIZE WEWE NI MTOTO WA NGAPI NAJEE UNAITENDEA VYEMA NAFASI YAKO?*

Friday, September 7, 2018


*KANUNI KUMI ZA KIBIBLIA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA:*
  Na: *PROPHET DERICDADY*
Biblia inatoa mwongozo mzuri wa usimamizi wa fedha ambao tukiufanyia kazi tuta punguza kwa asilimia kubwa matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo.Matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo yanachangiwa sana kwa namna moja au nyingine na usimimamizi mbaya wa fedha zetu,wengi wetu tatizo letu kubwa zaidi ni usimamizi wa fedha kuliko kuzalisha na kupata fedha.


usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini kama una usimamzi mbaya wa fedha  uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila  kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.


*1.       MUNGU NDIYE MMILIKI WA FEDHA ZETU*

Fedha ni Mali ya Bwana,sisi tu wasimamizi tu au mawakili,hivyo tunawajibika na vile tunatumia kila fedha tuliyoaminiwa na Mungu.( Mathayo 25:1-30 ; Zaburi 24:1,)


*2.       TAMBUA FEDHA NI SUALA LA KIROHO.*

Kwa mtu wa Mungu fedha ni suala la kiroho,fedha ina athiri na inagusa maisha yako ya kiroho pia.vile unavyo shughulika na fedha kuna sema zaidi juu ya hali yako ya moyo kuliko ushuhuda wako.vile unavyoshughulika na fedha zako ni kiashirio cha ukomavu wako kiriho.LUKA 16:10-11

Fedha inaweza kuwa mungu wako,fedha ina uwezo zaidi kutuvuta taratibu na kwa ujanja kutoka kwa Mungu kuliko kitu kingine chochote.MATH 6:24,Ina nguvu ya kuwa Bwana wetu.

Katika mifano 38 ya Yesu,16 inahusu fedha,katika agano jipya fedha imezungumzwa zaidi kuliko habari za mbinguni na kuzimu vikiunganishwa pamoja.mara tano zaidi imezungumzwa kuhusu fedha kuliko maombi,kuna mistari zaidi ya 1500 inayohusu maombi na imani,wakati kuna zaidi ya mistari 2000 inayohusu fedha na mali.Aslimia 15% ya Biblia  ni kuhusu fedha.


*3.       TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA*

Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki,nini nina dai,nini nina daiwa,natuamiaje(MITHALI 27:23-24, 23:23,)


*4.       FANYA TATHIMINI  YA MARA KWA MARA YA FEDHA ZAKO:*

ni muhimu kufanya tathimini kwa uaminifu kuhusu uchumi wako,mapato yako,madeni,vitega uchumi vyako n.k. hii itakusadia kufanya marekebisho unayoyahitaji na  kukusaidia kuishi kwa mpango,kama huwezi kutathimini hutaweza kupanga,ukishindwa kupanga,tayari umeshindwa kusimamia fedha yako.(MITHALI 21:5  LUKA 14:28)



*5.       JIWEKEE  MFUMO WA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA:*

Bajeti kirahisi nikuandika  katika karatasi nini unategemea kupata kama mapato na njisi gani unategemea kutumia.panga matumizi yako.Ni mpango wa jinsi gani utatumia rasilimali  fedha ambazo unatarajia kupata ,bajeti inapaswa ijumuishi vyanzo vya mapato  pia mpango wa matumizi wa mapato mf.mpango wa chakula,kodi,zaka,utoaji,akiba n.k(Mithali 21:5, Mithali 21:20)


*6.       JIWEKEE  UTARATIBU WA KUWEKA AJIRA*

Weka Akiba, kwaajili ya dharura,akiba kwaajili malengo maalumu, (Mithali 21:20a ;13:11)

Mithali 6. Tenga kiasi cha kuweka akiba anza na kiasi kidogo kwanza.


*7.       JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU-*

(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni tofauti,kadiri unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa  kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.


*8.       TUMIA FEDHA YAKO KWA HEKIMA NA RIDHIKA NA ULICHO NACHO:*

Zingatia vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)


*9.       TUNZA VITU NA MALI AMBAVYO UMEVIGHARIMIA FEDHA.*

Vitu,mali ni fedha,usipovitunza utatoa fedha tena kununua. Tunza visiharibike ovyo,vitumike kwa uangalifu ili kuokoa gharama ya matengenezo au kununua upya.


*10.   EPUKA MADENI.*

biblia haijakataza moja kwa moja kuhusu kukopa,ila kwa uwiano wa maandiko Haiti moyo madeni,bali inakatisha tamaa kukopa.inazungumza zaidi madhara ya kukopa.Unapokuwa katika deni unakuwa katika kifungo,Madeni yana haribu uhusiano.usitumie fedha zaidi ya ile unayozalisha utaishia kwenye madeni.weka akiba kidogo kidogo badala ya kukopa.

MITHALI 22:26-27,ZABURI 37:21,MITHALI 22:7


*HITIMISHO:*

Pengine umekuwa unapitia katika kipindi kigumu cha kifedha,uchumi wako umeyumba,kabla ya kuhitaji fedha zaidi unahitaji kuzifanyia kazi kanuni hizi za usimamizi wa fedha.Mungu anakusubiri ujifunze na kuzingita kanuni hizi za fedha ili akufungulie mlango mkubwa zaidi wa kifedha,ni jukumu lako kutii kanuni hizi na hali yako ibadilike au ubaki katika hali uliyo nayo.Mungu akubaliki unapochukua uamuzi wa kusimamia fedha zako kama wakili mwaminifu.MUNGU akubariki sana

*son of Alpha and Omega*
   0712412170
*PROPHET DERICDADY*

Monday, September 3, 2018

*IJUE NGUVU YA MAONO KATIKA MAISHA YAKO*
  *SON OF ALPHA AND AND OMEGA*
  _NA: PROPHET DERICDADY_
*0712412170*

*The man doesn’t make the vision; the vision makes the man*.
– Pastor Yonggi Cho

Maono: Ni ule uwezo wa kuyaona maisha ya baadae kwa wakati uliopo, {mtazamo wa maisha yajayo}; maono humfanya mtu ajizuie kutenda maovu kwa ajili ya kulinda na kuyaponya maisha yake na ya kundi zima kwa ujumla.

Kwani “pasipo maono watu huacha kujizuia”

·       Maono hutofautiana kati ya mtu na mtu kulingana na kitu anachokihitaji maishani na kipo ndani yake wakati huu: Kwa mfano:-

·       Maono ya kiongozi ni tofauti na ya mfanyabiashara, ni tofauti kabisa na msomi katika fani yake.

·       Maono ya mchungaji ni kulitunza kundi lisitawanyike na lipate mahitaji yake.

·       Maono ya mwinjilisti ni watu wengi kuokoka

·       Maono ya Askofu ni kuwa mwangalizi wa kundi zima.

Maono huendana na wito wa mtu, na kama biblia inavyosema kuwa “Mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo.” [Efeso 4:1b-2]. Ndivyo mtu anavyotakiwa kuenenda sawa sawa na picha anayoiona mbele yake kila wakati na kila mahali ili aifikie na kuifanikisha katika maisha alisia.

“Tena Neno la Bwana likanijia, kusema, Yeremia waona nini? Nikasema, naona ufito wa mlozi. Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema, Kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize. Neno la Bwana likanijia mara ya pili kusema, waona nini?  Nikasema, naona sufuria yenye maji yatokotayo, na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini….” [Yeremia 1:11-13]

Vijana wengi sana wamejiharibu nafsi zao kwa tamaa za mwili zipitazo hata kuipoteza ile nguvu ya maono iliyokuwa inatenda kazi kwa namna ya pekee sana ndani yao.

Weka mikakati ya kuyatimiza maono hayo kwa wakati muafaka. Historia imejaa watawala waliokuwa tayari kumwaga damu za watu wengi ili watimize maono yao ya kupanua utawala wao. Mkuu katika hao atakuwa ni yule anayetajwa kama Mnyama katika Ufu 13: 5

Katika mwisho wa historia ya ulimwengu huu inaonekana Mungu atampa mtu huyu ambaye pia anaitwa mpinga Kristo mamlaka juu ya mataifa yote duniani.Maono yake yatakuwa ni kuwa mkuu wa wote. Atafungua mdomo na kumkafiri Mungu mwenyewe. Ndiyo maana anaitwa mpinga Kristo. Anafanya yote kinyume na Kristo. Anapinga yale yote yanaoupendeza moyo wa Mungu. Lakini ni wa mwisho na mwenye nguvu zaidi tu katika mlolongo mrefu wa viongozi katika historia waliopinga mpango wa Mungu. Na Mungu atavunja mamlaka yake baada ya muda mfupi.

*You can’t pocess beyond what you see* (Mwanzo 13:14-18), [Huwezi kumiliki zaidi ya pale unapopaona, “Maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo” [Mithali 9:1]. Unapo muuliza mtoto mdogo kuwa anataka kuwa nani maishani, unakua unamfanya akueleze kuwa anaona nini katika maisha yake yajayo; yaani anapicha gani inayomfanya asitulie mpaka ameifikia hiyo picha ya maisha yake yajayo. Ndio maana anasema, nataka kuwa mwalimu, au daktari, au dereva n.k vivyo hivyo Mungu anakuuliza leo hii kuwa unaona nini?  Hatuwezi kujifunza juu ya kufanikiwa katika maono kama hatujui tunaona nini? Na hatujui nguvu iliyomo katika hayo maono.

*IGEUKIE NGUVU YA MAONO*

“Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; Na wana wenu, waume Kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, Na vijana wenu, wataona maono” [Yoeli 2:28]

·       Wazee wenu wataota ndoto-Ndoto huja kutokana na shughuli nyingi za siku hiyo [Mhubiri5:3a], na wazee wameishi miaka mingi kiasi ambacho shughuli zote walizozifanya katika maisha yao mpaka sasa huwapelekea kuota ndoto, na kazi kubwa ya wazee katika maisha ni kutoa ushauri na kuwashirikisha vijana hekima  na maarifa ambayo wameikusanya kwa miaka mingi na Maono ya wazee ni kufa katika uzee mwema ili wakamwone Mungu, ndio maana mazungumzo yao mengi yanahusu uzima wa milele na namna ya kuilinda imani yao. Wazee wengi wamesha timiza maono yao.

·       Vijana wenu wataona maono-Maono hutokana na mtazamo wamaisha yajayo ambayo mtu anatamani kuyafikia lakini bado hajafanikiwa kuyafikia. Ndio maana ya vijana kuona maono. Mtazamo huu hutegemeana na fikra na utashiwa mtu binafsi na namna anavyo enenda katika kusudi la yeye kuishi hapa duniani. Ndio maana vijana wanatakiwa kuona maono kwa kuwamaono yanahitaji nguvu na mikakati thabiti ya kuitimiza ili kupata kinachohitajika.

Nguvu ya maono ipo ndani ya mmbeba maono mwenyewe, na yeye ndiye anayejua afanye nini ili afikie maono yake, tunaposema “Igeukie nguvu ya maono”tuna maanisha ufanye mambo yako kulingana na kile unacho kitarajia maishani, na hii ina maana sawa na ile ambayo mtume Paulo anaelezea kuwa “Mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa” [Efeso 4:1b].

Mungu ameweka nguvu (uwezo) ndani ya kila mwanadamu inayo mwezesha kuishi hapa duniani Kwa kupata mahitaji yake ya kila siku. Njia pekee ni kufanya kazi ili kupata chakula na mahitaji mengine na “… ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula” [2 Thesalonike 3:10c]. Unapoigeukia nguvu ya maono unakuwa umechukua hatua ya kuyafanyia kazi malengo yako na ile mikakati uliyojiwekea ili kuyafanikisha maono ya maisha yako.

Nguvu hii haionekani, lakini ipo ndani yako, ni nguvu ya kipekee inayokufanya usome kwa bidii, uwe mkulima hodari, ufanye kazi kwa moyo wote, ni nguvu inayokuwezesha kuzaa na kutunza watoto, ni nguvu ya ajabu inayokufanya ujitambue kuwa umekua mtu mzima na unawajibika kwa nafasi yako kama baba au mama, kama kijana ama mzee; ni nguvu isiyoonekana kwa macho haya ya nyama lakini tunaishi nayo ndani yetu.

Uwezo wa kufikiri, uwezo wa kuwaza, uwezo wa kubaini na kujua mema na mabaya, uwezo huu ndio nguvu yenyewe inayopelekea kufanikiwa katika maisha haya kwa kuyafanikisha maono yako katika uhalisia wake. Igeukie nguvu hii ili uyafanikishe maono yako, tafakari na chukua hatua, kwani hakuna mtu wa kumlaumu katika maisha haya zaidi yako mwenyewe. Nataka ujue kuwa Mungu ametuwekea nguvu hii na ujuzi huu ndani yetu ili kupunguza idadi ya maombi yanayopelekwa mbele zake kila wakati.

Kuna mambo mengine yanahitaji tutumie ujuzi tulionao na sio maombi, sina maana ya kuwa maombi hayana umuhimu lakini nina maana ya kuyajua na kuyatumia maarifa tuliyokirimiwa na Mungu wetu. Mungu anaposema kuwa “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” [Hosea 4:6a] ana maana ya kuwa kuna ujuzi ambao tunatakiwa kuwa nao kwa kujifunza ama kwa kukirimiwa na Yeye, ambao tunatakiwa kuutumia ili tuweze kuishi sawasawa na mapenzi yake.

MAONO HUENDANA NA MUDA/WAKATI MAALUM

*If you think you can, you can; and if you think you can’t, you can’t; you are always right.*

Siku zote za maisha yako uwe na ndoto za mafanikio, hii itakufanya siku moja uketi pamoja na wakuu wa nchi. Kubali kupokea Baraka kutoka kwa wengine na uwe mtu wa shukrani.

Tumia muda wako vizuri kupanga mambo ya kimaendeleo. Kumbuka watu waliokabiliana na matatizo makubwa ndio walioweza kufikia mafanikio makubwa kiroho, kiuchumi na kisiasa, kwa kuwa wanazikubali changamoto katika maisha, Leo tutaangalia jinsi ya kutokufuata mawazo ya wale wanaotaka kukurudisha nyuma kimaendeleo.

Miongoni mwa jamii tunazoishi, huwa kuna baadhi ya watu ambao hufurahia wenzao wanaposhindwa kutimiza malengo waliojiwekea, Ama huwa na tabia ya kuwakatisha tamaa wanaopenda kujikwamua kutoka katika hatua moja na kuelekea hatua nyingine.
Watu hao mara zote huwakatisha tamaa wenzao kwa jambo fulani, kwa kuwaambia kuwa, wasijaribu kulifanya kwa kuwa hawatafanikiwa. Kumbe watu hao, ilitakiwa kuwatia moyo wale wanaotaka kujikwamua kiuchumi kwa kuwaambia kuwa, wajaribu kufanya jambo walilolikusudia.

“Mawazo ya watu kama hao wasiopenda mafanikio ya wengine mara zote ni sumu ya maendeleo”. Hivyo unapokutana na watu kama hao, unachotakiwa kukifanya, ni kujiwekea mazingira ya kujikinga pale wanapokujia na kutaka kukulisha sumu hiyo.
Lakini kwa upande mwingine, wewe unayependa kupiga hatua kimaisha, unaweza kuyapokea mawazo ya wale wanaowakatisha tamaa wenzao, kama ni njia mojawapo ya kukutoa hapo ulipo na kupiga hatua zaidi.

Kamwe usiruhusu watu hao wasiopenda maendeleo yako kukukatisha tamaa kiasi cha kuharibu ratiba na mipango yako ya kimaendeleo uliyojiwekea. Kwa kuwa, watu wa namna hiyo wapo kila mahali, na kazi yao ni kuharibu mipango mizuri ya maendeleo ya wengine.
Huweza kutumia wengine kuyabeza mafanikio yako, kukucheka, na pengine huweza kukukopa baadhi ya bidhaa zako na kukuletea usumbufu katika malipo, ili mradi wewe uchukie na kuamua kuacha kufanya biashara uliyoianza.

Hizo ni changamoto zilizopo katika maisha yetu ya kila siku cha msingi, ni kusonga mbele na kufanya kile ulichokusudia bila kuangalia wengine wanasemaje juu yako ya kukurudisha nyuma. Wapinzani wa maendeleo ya wengine wapo kila mahali. Wengi wao ni wavivu hivyo wanashindwa kukabiliana na ugumu wa maisha, hupenda kuwakatisha tamaa wengine ambao wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika kufikia mafanikio wanayoyataka.
Usifanye makosa katika malengo yako.Kwa kuwa hata katika eneo lako la kazi, iwe ni ofisini ama kwenye biashara wapo wanaokukatisha tamaa ya kuendelea na mipango yako.


Kwa kuwa, katika hali halisi tumetofautiana kifikra na kimaendeleo.Miongoni mwetu wapo wale wenye mipango ya kupenda kupiga hatua kila wakati za kimaisha, na wapo wale ambaohupenda kuangalia wengine wanafanya nini na kuwabeza. Katika hilo, usikate tamaa. Piga hatua zaidi katika kufanikisha malengo yako kwa kuwa na mkakati wa kujiwekea kanuni ya kutafuta ushauri kutoka kwa watu wenye mafanikio zaidi yako. Ukijijengea tabia ya kuuliza maswali pale unaposhindwa, ni sawa na kutibu ugonjwa wa kansa unaokusumbua.

Vile vile ujue kuwa, katika maisha mafanikio yako pia yanategemea msaada wa kimawazo kutoka kwa wengine. Huwezi ukawa na mipango yako mwenyewe na mawazo yako mwenyewe ukafanikiwa bila kuomba ushauri kwa wengine walio mbali zaidi yako kimaendeleo, wale unaoweza kuonana nao na kuongea nao bila matatizo.

Changamoto za mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mafanikio. Bila kufanya kazi kwa bidii ni vigumu kupata mafanikio katika maisha. Njia mojawapo ya kufikia mafanikio hayo ni kuainisha malengo yako unayotaka kuyafikia.


*UPANGAJI MALENGO YAKO*

Jinsi unavyoweza kupanga malengo makubwa katika maisha yako. Watu wengi hushindwa kufikia malengo makubwa kwa kuwa, mara zote hujikatisha tamaa kuwa hawawezi kufanya jambo kubwa la kimaendeleo, kabla ya kujaribu kulifanya. Tabia ya baadhi ya watu hao wanaokuwa na malengo madogo katika mazingira wanayoishi, ina maanisha eneo hilo hakuna ushindani wa kimaendeleo,ama wao wenyewe hawana jitihada za dhati za kupiga hatua zaidi mbele

Lakini ikumbukwe kuwa, katika kutafuta mafanikio hayo ili uwe na maisha bora, usimwangalie mtu jinsi alivyo, kwamba ana urefu gani, ana pesa kiasi gani, digrii aliyonayo ama kuangalia historia ya maisha yake, bali hupimwa kwa uwezo wa kufikiri kwake. Watu wengi wanaofikiria kuwa na malengo makubwa ya mafanikio, katika maisha yao ni kutokana na matarajio waliyonayo.

Inakupasa kila mara ujitahidi kupanua mawazo yako na kubuni mbinu mpya za kukutoka hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi kimaendeleo. Hivyo utambue kuwa, unapotaka kufanya mambo makubwa inakupasa ujijue wewe ni nani na una thamani gani.Kwa maelezo mengine usijishushe hadhi yako kwa kuona kuwa huwezi kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo yatakutoa hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi.

MFANO

Tuangalie mfano wa kijana mmoja aliyeshindwa kupiga hatua mbele baada ya kujishusha hadhi yake na kujiona hawezi.Kijana huyo, aliona tangazo la kazi katika gazeti. Kazi aliyokuwa anapenda kuifanya na pia ameisomea. Lakini hakufanya jitihada za dhati za kuomba nafasi ile, kwa kuwa alijiona hawezi kuipata hata kama angeomba. Aliona kuliko ajitaabishe ni heri aache kuomba nafasi hiyo. Mfano huo si mzuri kwa mtu anayetaka kupiga hatua kimaisha.

Usijishushe hadhi yako ama usikatishwe tamaa kwa hali yoyote ile. Ni vema kujaribu kile unachokipenda na unachokihitaji katika maisha yako, kuliko kuacha kujaribu kwa kuogopa kuwa hautafanikiwa. Kwani matokeo huja baadaye, hata utakaposhindwa, utakuwa na nguvu ya kujaribu tena sehemu nyingine. Wengi wetu, tumekuwa tukijikatisha tamaa katika shughuli mbalimbali tuzifanyazo ama tunazotaka kuzifanya.

Yawezekana umeanzisha biashara kwa lengo la kukuinua kiuchumi, lakini matokeo yake, biashara hiyo haiendi kama vile ulivyotarajia. Jambo la msingi, inakupasa kukaa chini na kujitathmini, kuangalia ni sehemu gani unayokosea. Ama kuangalia, kama una washindani wengi katika eneo hilo, ili uweze kufanya vizuri zaidi yao, kwa kuweka kjvitu vingi tofauti na kuboresha eneo la biashara yako.

*UBUNIFU-CREATIVITY*

Kuwa mbunifu katika biashara yako kutakupa wateja wengi, na utafanikiwa zaidi. Cha msingi usikate tamaa katika kufikia malengo unayoyakusudia. Kutokana na hali ya kujikatisha tamaa, miongoni mwa watu wengi, wanasaikolojia mbalimbali wamekuwa wakishauri ni vema, watu wajijue vile walivyo ili waweze kujirekebisha pale penye upungufu na kusonga mbele kimaisha.
-Hali ya kujikatisha tamaa ni mbaya sana, ni sawa na ugonjwa usiopona katika mwili wako. Ili kuutibu ugonjwa huo, inakupasa ujielewe wewe ni nani, na una upungufu gani, pamoja na kukubali mabadiliko.

Tatizo kubwa lililopo kwa watu wengi, hawajui kuwa, wao wana uwezo mkubwa tofauti na wanavyojifikiria.Hivyo ni vema kuweka mawazo yako kwenye kipimo halisi, uyachuje na kuchukua yale yaliyo na thamani. Penda kufikiri mambo makubwa. Usijishushe hadhi yako kwa kujiwekea au kufikiri malengo madogo. Anza sasa kuwaza mambo makubwa ili uwe mtu mwenye ndoto njema ya maendeleo.

Kutokana na hali hiyo ya watu kujikatisha tamaa, wale ambao wamewahi kufanya biashara na kufilisika, wengi wao wamekuwa wakisema kuwa hawatarudia tena kufanya biashara hiyo.
Lakini kumbe, haikuwapasa kukata tamaa, bali kujipa moyo, na kuelewa kuwa pamoja na hali hiyo ya kushindwa inawapasa kujaribu tena. Kamwe usikate tamaa katika jambo lolote unaloliwaza ama kulifanya. Kwa kuwa, upo msemo mmoja unaosema, penye nia pana njia.

*MAFANIKIO HUTOKANA NA IMANI YAKO*

Ili kuwa mtu wa mafanikio ni vema kutumia mbinu ya ufikiri kwa ubunifu kile unachotaka kukifanya. Ni vizuri kuwa na imani, unaweza kufanya jambo lako na likafanikiwa, kwani unapoamini litafanikiwa, akili yako itazidi kutafuta njia ya kulifanikisha zaidi.

Kuamini kuwa unaweza kufanya jambo kubwa, kunafungua njia ya mafanikio. Kamwe usiseme ama kufikiri kuwa huwezi kufanya jambo fulani katika maisha yako, badala yake, jaribu kufanya kile unachofikiri kuwa huwezi. Usiruhusu mambo ya mila na desturi ama utamaduni uliouzoea kutawala akili yako. Kuwa mtu wa kupokea mambo na mawazo mapya kila wakati, kisha uyafanyie kazi.

Kila wakati jaribu njia mpya katika kufanikisha mambo yako, pamoja na kuwa mfuatiliaji wa shughuli zako unazozifanya. Iulize nafsi yako, inakupasa kufanya nini ili kuweza kufanya vizuri zaidi? Wakati unajiuliza swali hilo, unakuwa tayari umeshapata jibu, cha msingi ni kulifanyia kazi jibu hilo ulilolipata bila kuchelewa. Pia jiulize ni kwa vipi unaweza kufanya vizuri zaidi?

Pia ni vema ukawa na mazoea ya kusikiliza na kuuliza kwa wengine,kuhusu mambo unayotaka kuyafanya kwani utapata mawazo mengi usiyoyajua kutoka kwa wengine.
Yapanue mawazo yako, kwa kujichanganya na watu mbalimbali wakiwamo wenye ujuzi wanaoweza kukupa mawazo na njia mpya za kufanya mambo. Moja ya kanuni ya mtu anayependa au mwenye mafanikio ni kuwa na muonekano mzuri mbele ya jamii, kuanzia anavyozungumza hadi mavazi yake.

Unaweza usikubaliane nami, lakini ukweli ni kuwa, kama wewe ni mfanyabiashara wa nguo, jinsi unavyokuwa mtanashati mbele za watu, ndivyo watakavyopenda kuja katika duka lako na kununua bidhaa zako hizo. Lakini, kama utakuwa haujijali kwa upande wa mavazi, halafu ukawa mfanyabiashara wa bidhaa hiyo, utapata wateja wale wasiokujua na wanaokujua wachache.

Utanashati unavutia biashara yako, si tu kwa biashara ya nguo, bali hata katika shughuli zako nyingine unazozifanya, uwe ni mwanasheria, mwalimu ama mpishi wa chakula, vile unavyoonekana ndivyo unavyozidi kuimarisha biashara yako. Kumbuka watu wanakutathmini kutokana na muonekana ulio nao. Hebu tuangalie mfano huu kuwa, mtu anafanya biashara ya nyanya, anazipanga mafungu mafungu na kuziuza. Mwingine anafanya biashara hiyo hiyo, na kuziweka nyanya zile katika mfuko wenye kuonyesha bidhaa iliyopo ndani yake na kufunga vizuri.

Biashara hizo zikiwa katika eneo moja, watu wengi watanunua zile zilizofungwa vizuri kwenye mfuko wakiamini kuwa ni salama zaidi. Mfano huo ni sawa na muonekana ama utanashati wako kwa watu katika shughuli yoyote ile unayoifanya. Uvaaji mzuri na wa heshima kwenye jamii, unakufanya uheshimike na kuaminika kuwa unaweza kufanya mambo makubwa unayoyapanga.

Ni vizuri kuboresha mawazo yako kila siku, kama watu maarufu wanavyokuwa.
Kuboresha mawazo, kufikiri na utendaji wako kutakuletea mafanikio katika mipango yako yote.
Hivyo ni vema, kula vizuri ili uweze kufikiri vizuri katika mambo unayoyafanya.
Endapo hautakula mlo kamili, akili yako haitakuwa na uwezo wa kufikiri vizuri, utabakia kuwa mtu wa kushindwa. Kama mtu anakula vizuri, anajilinda na magonjwa mbalimbali, mwili wake unakuwa na afya pamoja na akili yake kuwaza mambo makubwa.

*Akili yako huwezi kuilisha chakula unachokula, bali chakula chake ni mazingira yanayokuzunguka.* Mtu yeyote anayetembea katika nchi ama mikoa mbalimbali, huwa na mazingira ya tofauti, kila anapokwenda hujifunza kitu kitakachomsaidia. Mazingira ya eneo ulilopo yanaifanya akili yako ifikiri zaidi ufanye kitu gani cha mafanikio katika eneo hilo ulilopo kitachokupatia maendeleo.Ukubwa wa jinsi unavyowaza, malengo yako, mazingira yako au vile unavyoonekana, ni kutokana na mazingira uliyopo.

Unapokuwa na watu wenye mawazo ya kuchelewa kufanikisha mambo, nawe utakuwa mtu wa kuchelewa kufikia malengo uliyojiwekea. Kwa maana nyingine, kushirikiana na watu wenye mawazo makubwa kunakufanya uwaze mambo makubwa ya maendeleo.
Pia kukaa karibu na watu wenye malengo ama maono ya mafanikio, kunakufanya nawe uwe katika hali hiyo.Kuna msemo usemao  *nionyeshe rafiki zako, namimi nitakuambia wewe ni nani*

_NB: Katika jamii tunayoishi, kumekuwa na watu wenye tabia zilizogawanyika katika makundi matatu._

Kundi la kwanza, ni la watu wale ambao wameona kuwa hawawezi kufanya jambo likafanikiwa kabisa. Wamekuwa na ujuzi na kukubali ujuzi huo katika eneo moja, yaani wameridhika na hali hiyo. Kama, Mungu amekupa ujuzi wako mzuri na ukabahatika kupata kazi sehemu nzuri, pamoja na kufanya kazi ile, utumie ujuzi wako katika maeneo mengine.
Unaweza kufungua ofisi yako na kuanzisha kitu chako mwenyewe huku ukiendelea na kazi yako.

Kamwe usijikatishe tamaa kwa kuona kuwa huwezi kufanya hivyo, kudhani kuwa, wewe umeumbwa kwa ajili ya kufanya kazi za wengine tu. Kuna watu wenye malengo makubwa na waliopanga kuyatimiza lakini kutokana na ushindani uliopo hufika mahali na kushindwa kuendelea na mikakati waliyojiwekea.Tunaweza kusema, wamekata tamaa na kuacha kuyafanyia kazi malengo yao, mwishoni hupoteza mwelekeo kabisa.

Kundi hili, wamejijengea tabia ya hofu, hofu ya kushindwa kutimiza malengo yao, hofu ya ulinzi, hofu katika jamii inayomzunguka na kupoteza kila wanalicho nacho.
Kundi la watu hawa, kamwe hawatafanikiwa kwani wameshajiweka kwenye kundi la kushindwa ingawa lina watu wenye akili, vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Kundi la tatu ni la watu wale ambao hawako tayari kukatishwa tamaa, hawa ni asilimia ndogo sana katika jamii.

Kundi hili pamoja na kukatishwa tamaa, katika mipango yao, wamekuwa wakijitahidi kufanya jitihada mbalimbali ili wajikwamue katika hali hiyo waliyonayo na kuwa katika hatua nyingine.
Mara zote hupumua mafanikio katika maisha yao. Kundi hili pia lina furaha kwa kuwa limeshakamilisha baadhi ya malengo waliyojiwekea. Wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali, lakini wamezishinda, wamekuwa wakiangalia siku mpya ikianza na jambo jipya. Ni ukweli usiopingika kuwa, kila mmoja wetu anapenda kuwa katika kundi la tatu, ambalo kila mwaka wanapata mafanikio, wanaofanya mambo mbalimbali na matokeo yake yanaonekana.


*MATOKEO YA MAONO* (The Impact of Vision)

*Katika maisha kuna nyakati tunapaswa kupanda katika vilele vya milima yetu binafsi ili tuweze kuuona mustakabali wetu (our future) kutokea katika kile kiwango cha juu tulikosimama*         (Dr. John Tibane)

*Mafanikio katika maisha ni safari, ila kuweza kukaa katika safari hii kunahitaji msukumoKatika maisha kunanyakati tunapaswa kupanda katika vilele vya milima yetu binafsi ili tuweze kuuona mustakabali wetu (our future) kutokea katika kile kiwango cha juu tulikosimama.* (Dr John Tibane).

Mafanikio katika maisha ni safari, ila kuweza kukaa katika safari hii kunahitaji msukumo wa ndani  pamoja na ujasiri. Bila vitu hivi muhimu wengi wetu hukata tamaa njiani na kuiahirisha kwa urahisi safari yao kuelekea mafanikio. Ni kwa jinsi unavyoupenda mustakabali wako na ni kwa jinsi unavyoipenda kesho yako ndiko kutakakokupa msukumo wa ndani pamoja na ujasiri. Ili kuweza kuiona kesho yako au mustakabali wako pasipo vizuizi inahitaji msaada wa kimungu (divine assistance) katika hali ya rohoni.

Kati ya siri mojawapo inayoweza kukusaidia ni kuandika katika karatasi nini unachokiona katika kesho yako, je unaona uzuri, furaha, amani, utajiri, mafanikio, au afya? Andikainawezekana kuwa ni kwenye chumba chako cha sala au sehemu unayopenda kuitumia kufikiria au kuwaza kiundani mambo ya maisha yako (meditation space).


Ili sasa kuianza safari yako kuelekea nchi yako ya ahadi, inakupasa kushuka chini kutoka mlimani ulikokuwa na kuja ardhini (In reality). Kumbuka kuwa kilakitu unachokiona huku chini katika ardhi kinaweza kuwa ni tofauti kabisa na vile ulivyoviona ukiwa juu katika kilele cha mlima, sasa unalazimika kuendelea kushika vema yale maono yako ya kweli uliyoyaona ukiwa juu, hata kama uhalisi unaoonekana huku chini ni tofauti. Utaanza kuishi na kutembea katika kuyafikia maono yako ukiwa hapa chini lakini si kama unavyoyaona mambo ukiwa chini bali kama ulivyoyaona ukiwa pale kileleni juu. Hii ndiyo tunayoiita ‘imani’  hakika ya mambo yatarajiwayo na bayana ya yale yasiyo onekana katika uhalisi hapa chini bali kama yalivyoonekana tukiwa kileleni pale juu.


Pasipo maono watu huangamia, maisha ya watu huharibika kabisa, watu huishi kihasara hasara tofauti na walivyo tazamiwa kuishi. Wanakosa uwezo wa kujitawala na kuwa na kiasi, wanakuwa watu wasiotawalika na waharibifu. Maono ya kweli  yanatupa kujiweza, kujitawala wenyewe, kuvumilia na kuwa na matazamio mema. Msukumo wa ndani na ujasiri huzaliwa kutoka katika maono ya kweli.


*Faida za maono .*

1.    
       *1. Maono ya kweli huyatia nguvu maisha yako.*

Maono ya kweli hukupa sababu na maana ya kwanini unaishi. Unatiwa msukumo, unahamasishwa, ni kama vile simu inapokosa chaji inalazimika kuwekwa katika umeme ili iweze kuongeza uwezo wa kufanya kazi. Maono ya kweli ni kama nguvu ya umeme ndani yetu. Maisha yako yanakuwa yaliyojaa, huna muda wa kupoteza kuanza kuongelea watu na kuchunguza maisha ya watu wengine na kamwe hutopata tatizo la kujihisi mpweke usiye na chakufanya.


2.      *2. Maono ya kweli huzikutanisha pamoja nguvu au nishati zilizopo ndani yako.*

Ndani yako una nguvu na nishati mbalimbali kama vile nguvu za kiroho, kimwili, kihisia, kiakili na nyingine nyingi. Nishati hizi ni kama vile miale ya mwanga ambayo inachomoza kutoka kwako. Maono ya kweli yanakuwa kama kioo kinachokuza (magnifying glass) kinachokutanisha miale yote hii katika sehemu moja, na hapa ndipo nguvu zako au nishati zako huweza kutumika katika kiwango cha juu zaidi cha ufanisi na matokeo bora zaidi.


3.     *3.Maono ya kweli hurekebisha tabia zetu*

Kile ulichoweza kukiona ukiwa pale kileleni mwa mlima wako binafsi kinauwezo wa kubadilisha tabia zako. Kinakufanya ushindwe kufanya kitu chochote cha kipuuzi ambacho kinaweza kuiharibu kesho yako nzuri uliokwisha iona ukiwa pale juu, kinakufanya uwe makini sana katika maamuzi unayoyafanya kila siku. Jinsi unavyo fikiri, jinsi unavyo zungumza na hata kutenda inakuwa kama vile tayari umeshafika kwenye ile nchi ya ahadi uliyoiona ukiwa pale juu. Maisha na mizunguko yako ya kilasiku yanaongozwa na maono yako ya kweli.


4.      *4. Maono ya kweli yanazishinda hofu zako.*

Kwa kawaida kitu chochote unachokiangalia kwa mkazo hupanuka na kuwa kikubwa. Kama utayatilia mkazo  matatizo yako basi yataongezeka na kuonekana makubwa na hatimaye kukuogopesha. Unapoogopeshwa au kutishwa na tatizo fulani unakata tamaa katika kulitafutia ufumbuzi na kuendelea mbele. Watu waliofanikiwa kamwe hawachagui kuyatazama matatizo yao (kama yanavyoonekana wakiwa chini ya mlima) bali huzitazama fursa mbalimbali za mustakabali wao (kama zilivyoonekana wakiwa kileleni). Kwa jinsi utakavyozidi kuyatazama mafanikio, fursa zitapanuka na zitaongezeka na kukushawishi katika kuendelea na safari yako ya mafanikio. Upendo wa kweli kupitia maono ya kweli huziweza hofu zote.


5.      *5. Maono ya kweli yana uwezo  wa kuvuta msaada.*

Maono ya kweli wakati wote yanauwezo wakushawishi kila aina ya msaada uhusianao na maono hayo kuja, kama ni watu, fedha, vibali, na vitendea kazi vingine. Wako watu wanakila kitu lakini wamekosa tu maono, wanasubiri vile walivyo navyo vivutwe kwa sumaku ya maono ya kweli ili viende kutumika kule kuliko sahihi.  Wako watu wamezaliwa ili tu wawe msaada wa maono uliyonayo. Wanasubiri kwa hamu wewe uyaandike maono yako.


Ili kuhesabiwa pamoja na waliofanikiwa inakudidi uweze kuyaangalia mambo katika kiwango cha juu zaidi ili uweze kupata maono ya kweli ambayo yatazaa uwezo wa wewe kuipenda kesho yako.

*son of Alpha and Omega*
*0712412170*
*PROPHET DERICDADY*