Wednesday, September 12, 2018

*FAHAMU NGUVU ZAKO ZA KUZALIWA KWA UFUNUO WA ROHO MTAKATIFU*

Kumb 33:1-9, Mwanzo 49:3-7, 1Kor 2:10
Kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu Aliye Hai, ameumbwa na nguvu maalumu kutoka mbinguni, ambayo ni mtaji wake maalumu; kiroho, kijamii na kiuchumi.

Mwanzo 49:3
Reubeni u mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na nguvu.

*1. MZALIWA WA KWANZA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amebeba nguvu nyingi za familia.
ii. Amebeba Baraka za aina mbalimbali za wadogo zake.
iii. Amebeba nguvu ya upendo ndani ya familia.
iv. Mzaliwa wa kwanza ni lango, Zab 24:7-9, ambapo Baraka zote za familia kutoka mbinguni zinapitia kwake na kuwafikia wadogo zake wote.
v. Amebeba ustawi wa familia kiroho na kimwili.

*2. MTOTO WA PILI KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Ni m’beba neno la uzima.
ii. Kipawa cha ualimu kinakaa vizuri sana ndani yake.
iii. Amepewa neno la uzima la kusaidia kanisa familia na nchi.

*3. MTOTO WA TATU KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Ni mtawala katika ulimwengu wa roho na wa mwili.
ii. Ni mtunga sheria popote atakapokuwa anaishi, anasoma au anafanya kazi.
iii. Amepewa mamlaka ya kusimamia jamii, kuiongoza na kuitawala.
iv. Anafaa kuwa mwanasheria au kiongozi popote aendapo.

*4. MTOTO WA NNE KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amepewa neema ya kumiliki utajiri wa nchi.
ii. Kama akijitambua na kusimama katika zamu yake, ajue amepewa neema na nguvu ya kuutawala uchumi vizuri sana.
iii. Amepewa nguvu ya kumiliki utajiri wa mbingu na dunia.

*5. MTOTO WA TANO KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amepewa neema ya kushinda changamoto.
ii. Amepewa stamina ya kushindana na majaribu kwa asili.
iii. Amepewa neema ya kutumika na upako wa juu sana, kama akiokoka na kujitambua, na kusimama katika zamu yake.

*6. MTOTO WA SITA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
Ni mtu wa ujuzi, na talanta. Na Amepewa nguvu ya ubunifu wa pekee.

*7. MTOTO WA SABA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amebeba uheri wa Mungu Mtakatifu.
ii. Yeye ni jubilee, yaani maachilio.
iii. Usithubutu kushindana naye maana hautafanikiwa.
iv. Ukimshitaki hauwezi kufanikiwa.
v. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.
vi. Anafaa kuwa hakimu kama ataamua kuichukua taaluma hii.
vii. Ukipata kesi yoyote na akakusindikiza ni lazima utashinda, maana utu wake wa ndani ameumbiwa neema hii.

*8. MTOTO WA NANE KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Amebeba nguvu ya utumishi.
ii. Amepewa neema ya kusaidia wengi kiuchumi, kiroho na kijamii, kama akijitambua na kusimama katika zamu yake.
iii. Akiokakoka na kuwa mtumishi kanisa lolote, atalisaidia sana kustawi, kwa kuwa ni mtu wa kutegemewa sana.
iv. Amepewa neema ya kuwa nguzo.
v. Ukimtambua katika kanisa lako na kumthamini, na kumtumia vizuri, utafanikiwa sana.

*9. MTOTO WA TISA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Ni m’beba karama.
ii. Akipokea kipawa anakitunza sana kwa muda mrefu.
iii. Amepewa nguvu ya umoja.
iv. Ni mtu anaweza kuinganisha jamii, nchi au familia na kuleta mshikamano.
v. Anafaa kuwa mwanasiasa endapo akijitambua na kusimama katika nafasi yake aliyokirimiwa na mungu.

*10. MTOTO WA KUMI KATIKA FAMILIA YOYOTE*
i. Yeye ni msamaha.
ii. Amekirimiwa nguvu ya msamaha.
iii. Amepewa uwezo wa kusuluhisha migogoro kwa ufanisi wa hali ya juu sana.
iv. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.

*11. MTOTO WA KUMI NA MOJA KATIKA FAMILIA YOYOTE*
Ni faraja kwa familia.
Kuna wakati anapata tatizo la kukataliwa, lakini ni mvumilivu sana.
Mkikaa naye kwa upendo mtabarikiwa sana.

*JiULIZE WEWE NI MTOTO WA NGAPI NAJEE UNAITENDEA VYEMA NAFASI YAKO?*

Friday, September 7, 2018


*KANUNI KUMI ZA KIBIBLIA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA:*
  Na: *PROPHET DERICDADY*
Biblia inatoa mwongozo mzuri wa usimamizi wa fedha ambao tukiufanyia kazi tuta punguza kwa asilimia kubwa matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo.Matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo yanachangiwa sana kwa namna moja au nyingine na usimimamizi mbaya wa fedha zetu,wengi wetu tatizo letu kubwa zaidi ni usimamizi wa fedha kuliko kuzalisha na kupata fedha.


usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini kama una usimamzi mbaya wa fedha  uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila  kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.


*1.       MUNGU NDIYE MMILIKI WA FEDHA ZETU*

Fedha ni Mali ya Bwana,sisi tu wasimamizi tu au mawakili,hivyo tunawajibika na vile tunatumia kila fedha tuliyoaminiwa na Mungu.( Mathayo 25:1-30 ; Zaburi 24:1,)


*2.       TAMBUA FEDHA NI SUALA LA KIROHO.*

Kwa mtu wa Mungu fedha ni suala la kiroho,fedha ina athiri na inagusa maisha yako ya kiroho pia.vile unavyo shughulika na fedha kuna sema zaidi juu ya hali yako ya moyo kuliko ushuhuda wako.vile unavyoshughulika na fedha zako ni kiashirio cha ukomavu wako kiriho.LUKA 16:10-11

Fedha inaweza kuwa mungu wako,fedha ina uwezo zaidi kutuvuta taratibu na kwa ujanja kutoka kwa Mungu kuliko kitu kingine chochote.MATH 6:24,Ina nguvu ya kuwa Bwana wetu.

Katika mifano 38 ya Yesu,16 inahusu fedha,katika agano jipya fedha imezungumzwa zaidi kuliko habari za mbinguni na kuzimu vikiunganishwa pamoja.mara tano zaidi imezungumzwa kuhusu fedha kuliko maombi,kuna mistari zaidi ya 1500 inayohusu maombi na imani,wakati kuna zaidi ya mistari 2000 inayohusu fedha na mali.Aslimia 15% ya Biblia  ni kuhusu fedha.


*3.       TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA*

Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki,nini nina dai,nini nina daiwa,natuamiaje(MITHALI 27:23-24, 23:23,)


*4.       FANYA TATHIMINI  YA MARA KWA MARA YA FEDHA ZAKO:*

ni muhimu kufanya tathimini kwa uaminifu kuhusu uchumi wako,mapato yako,madeni,vitega uchumi vyako n.k. hii itakusadia kufanya marekebisho unayoyahitaji na  kukusaidia kuishi kwa mpango,kama huwezi kutathimini hutaweza kupanga,ukishindwa kupanga,tayari umeshindwa kusimamia fedha yako.(MITHALI 21:5  LUKA 14:28)



*5.       JIWEKEE  MFUMO WA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA:*

Bajeti kirahisi nikuandika  katika karatasi nini unategemea kupata kama mapato na njisi gani unategemea kutumia.panga matumizi yako.Ni mpango wa jinsi gani utatumia rasilimali  fedha ambazo unatarajia kupata ,bajeti inapaswa ijumuishi vyanzo vya mapato  pia mpango wa matumizi wa mapato mf.mpango wa chakula,kodi,zaka,utoaji,akiba n.k(Mithali 21:5, Mithali 21:20)


*6.       JIWEKEE  UTARATIBU WA KUWEKA AJIRA*

Weka Akiba, kwaajili ya dharura,akiba kwaajili malengo maalumu, (Mithali 21:20a ;13:11)

Mithali 6. Tenga kiasi cha kuweka akiba anza na kiasi kidogo kwanza.


*7.       JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU-*

(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni tofauti,kadiri unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa  kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.


*8.       TUMIA FEDHA YAKO KWA HEKIMA NA RIDHIKA NA ULICHO NACHO:*

Zingatia vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)


*9.       TUNZA VITU NA MALI AMBAVYO UMEVIGHARIMIA FEDHA.*

Vitu,mali ni fedha,usipovitunza utatoa fedha tena kununua. Tunza visiharibike ovyo,vitumike kwa uangalifu ili kuokoa gharama ya matengenezo au kununua upya.


*10.   EPUKA MADENI.*

biblia haijakataza moja kwa moja kuhusu kukopa,ila kwa uwiano wa maandiko Haiti moyo madeni,bali inakatisha tamaa kukopa.inazungumza zaidi madhara ya kukopa.Unapokuwa katika deni unakuwa katika kifungo,Madeni yana haribu uhusiano.usitumie fedha zaidi ya ile unayozalisha utaishia kwenye madeni.weka akiba kidogo kidogo badala ya kukopa.

MITHALI 22:26-27,ZABURI 37:21,MITHALI 22:7


*HITIMISHO:*

Pengine umekuwa unapitia katika kipindi kigumu cha kifedha,uchumi wako umeyumba,kabla ya kuhitaji fedha zaidi unahitaji kuzifanyia kazi kanuni hizi za usimamizi wa fedha.Mungu anakusubiri ujifunze na kuzingita kanuni hizi za fedha ili akufungulie mlango mkubwa zaidi wa kifedha,ni jukumu lako kutii kanuni hizi na hali yako ibadilike au ubaki katika hali uliyo nayo.Mungu akubaliki unapochukua uamuzi wa kusimamia fedha zako kama wakili mwaminifu.MUNGU akubariki sana

*son of Alpha and Omega*
   0712412170
*PROPHET DERICDADY*

Monday, September 3, 2018

*IJUE NGUVU YA MAONO KATIKA MAISHA YAKO*
  *SON OF ALPHA AND AND OMEGA*
  _NA: PROPHET DERICDADY_
*0712412170*

*The man doesn’t make the vision; the vision makes the man*.
– Pastor Yonggi Cho

Maono: Ni ule uwezo wa kuyaona maisha ya baadae kwa wakati uliopo, {mtazamo wa maisha yajayo}; maono humfanya mtu ajizuie kutenda maovu kwa ajili ya kulinda na kuyaponya maisha yake na ya kundi zima kwa ujumla.

Kwani “pasipo maono watu huacha kujizuia”

·       Maono hutofautiana kati ya mtu na mtu kulingana na kitu anachokihitaji maishani na kipo ndani yake wakati huu: Kwa mfano:-

·       Maono ya kiongozi ni tofauti na ya mfanyabiashara, ni tofauti kabisa na msomi katika fani yake.

·       Maono ya mchungaji ni kulitunza kundi lisitawanyike na lipate mahitaji yake.

·       Maono ya mwinjilisti ni watu wengi kuokoka

·       Maono ya Askofu ni kuwa mwangalizi wa kundi zima.

Maono huendana na wito wa mtu, na kama biblia inavyosema kuwa “Mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo.” [Efeso 4:1b-2]. Ndivyo mtu anavyotakiwa kuenenda sawa sawa na picha anayoiona mbele yake kila wakati na kila mahali ili aifikie na kuifanikisha katika maisha alisia.

“Tena Neno la Bwana likanijia, kusema, Yeremia waona nini? Nikasema, naona ufito wa mlozi. Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema, Kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize. Neno la Bwana likanijia mara ya pili kusema, waona nini?  Nikasema, naona sufuria yenye maji yatokotayo, na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini….” [Yeremia 1:11-13]

Vijana wengi sana wamejiharibu nafsi zao kwa tamaa za mwili zipitazo hata kuipoteza ile nguvu ya maono iliyokuwa inatenda kazi kwa namna ya pekee sana ndani yao.

Weka mikakati ya kuyatimiza maono hayo kwa wakati muafaka. Historia imejaa watawala waliokuwa tayari kumwaga damu za watu wengi ili watimize maono yao ya kupanua utawala wao. Mkuu katika hao atakuwa ni yule anayetajwa kama Mnyama katika Ufu 13: 5

Katika mwisho wa historia ya ulimwengu huu inaonekana Mungu atampa mtu huyu ambaye pia anaitwa mpinga Kristo mamlaka juu ya mataifa yote duniani.Maono yake yatakuwa ni kuwa mkuu wa wote. Atafungua mdomo na kumkafiri Mungu mwenyewe. Ndiyo maana anaitwa mpinga Kristo. Anafanya yote kinyume na Kristo. Anapinga yale yote yanaoupendeza moyo wa Mungu. Lakini ni wa mwisho na mwenye nguvu zaidi tu katika mlolongo mrefu wa viongozi katika historia waliopinga mpango wa Mungu. Na Mungu atavunja mamlaka yake baada ya muda mfupi.

*You can’t pocess beyond what you see* (Mwanzo 13:14-18), [Huwezi kumiliki zaidi ya pale unapopaona, “Maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo” [Mithali 9:1]. Unapo muuliza mtoto mdogo kuwa anataka kuwa nani maishani, unakua unamfanya akueleze kuwa anaona nini katika maisha yake yajayo; yaani anapicha gani inayomfanya asitulie mpaka ameifikia hiyo picha ya maisha yake yajayo. Ndio maana anasema, nataka kuwa mwalimu, au daktari, au dereva n.k vivyo hivyo Mungu anakuuliza leo hii kuwa unaona nini?  Hatuwezi kujifunza juu ya kufanikiwa katika maono kama hatujui tunaona nini? Na hatujui nguvu iliyomo katika hayo maono.

*IGEUKIE NGUVU YA MAONO*

“Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; Na wana wenu, waume Kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, Na vijana wenu, wataona maono” [Yoeli 2:28]

·       Wazee wenu wataota ndoto-Ndoto huja kutokana na shughuli nyingi za siku hiyo [Mhubiri5:3a], na wazee wameishi miaka mingi kiasi ambacho shughuli zote walizozifanya katika maisha yao mpaka sasa huwapelekea kuota ndoto, na kazi kubwa ya wazee katika maisha ni kutoa ushauri na kuwashirikisha vijana hekima  na maarifa ambayo wameikusanya kwa miaka mingi na Maono ya wazee ni kufa katika uzee mwema ili wakamwone Mungu, ndio maana mazungumzo yao mengi yanahusu uzima wa milele na namna ya kuilinda imani yao. Wazee wengi wamesha timiza maono yao.

·       Vijana wenu wataona maono-Maono hutokana na mtazamo wamaisha yajayo ambayo mtu anatamani kuyafikia lakini bado hajafanikiwa kuyafikia. Ndio maana ya vijana kuona maono. Mtazamo huu hutegemeana na fikra na utashiwa mtu binafsi na namna anavyo enenda katika kusudi la yeye kuishi hapa duniani. Ndio maana vijana wanatakiwa kuona maono kwa kuwamaono yanahitaji nguvu na mikakati thabiti ya kuitimiza ili kupata kinachohitajika.

Nguvu ya maono ipo ndani ya mmbeba maono mwenyewe, na yeye ndiye anayejua afanye nini ili afikie maono yake, tunaposema “Igeukie nguvu ya maono”tuna maanisha ufanye mambo yako kulingana na kile unacho kitarajia maishani, na hii ina maana sawa na ile ambayo mtume Paulo anaelezea kuwa “Mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa” [Efeso 4:1b].

Mungu ameweka nguvu (uwezo) ndani ya kila mwanadamu inayo mwezesha kuishi hapa duniani Kwa kupata mahitaji yake ya kila siku. Njia pekee ni kufanya kazi ili kupata chakula na mahitaji mengine na “… ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula” [2 Thesalonike 3:10c]. Unapoigeukia nguvu ya maono unakuwa umechukua hatua ya kuyafanyia kazi malengo yako na ile mikakati uliyojiwekea ili kuyafanikisha maono ya maisha yako.

Nguvu hii haionekani, lakini ipo ndani yako, ni nguvu ya kipekee inayokufanya usome kwa bidii, uwe mkulima hodari, ufanye kazi kwa moyo wote, ni nguvu inayokuwezesha kuzaa na kutunza watoto, ni nguvu ya ajabu inayokufanya ujitambue kuwa umekua mtu mzima na unawajibika kwa nafasi yako kama baba au mama, kama kijana ama mzee; ni nguvu isiyoonekana kwa macho haya ya nyama lakini tunaishi nayo ndani yetu.

Uwezo wa kufikiri, uwezo wa kuwaza, uwezo wa kubaini na kujua mema na mabaya, uwezo huu ndio nguvu yenyewe inayopelekea kufanikiwa katika maisha haya kwa kuyafanikisha maono yako katika uhalisia wake. Igeukie nguvu hii ili uyafanikishe maono yako, tafakari na chukua hatua, kwani hakuna mtu wa kumlaumu katika maisha haya zaidi yako mwenyewe. Nataka ujue kuwa Mungu ametuwekea nguvu hii na ujuzi huu ndani yetu ili kupunguza idadi ya maombi yanayopelekwa mbele zake kila wakati.

Kuna mambo mengine yanahitaji tutumie ujuzi tulionao na sio maombi, sina maana ya kuwa maombi hayana umuhimu lakini nina maana ya kuyajua na kuyatumia maarifa tuliyokirimiwa na Mungu wetu. Mungu anaposema kuwa “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” [Hosea 4:6a] ana maana ya kuwa kuna ujuzi ambao tunatakiwa kuwa nao kwa kujifunza ama kwa kukirimiwa na Yeye, ambao tunatakiwa kuutumia ili tuweze kuishi sawasawa na mapenzi yake.

MAONO HUENDANA NA MUDA/WAKATI MAALUM

*If you think you can, you can; and if you think you can’t, you can’t; you are always right.*

Siku zote za maisha yako uwe na ndoto za mafanikio, hii itakufanya siku moja uketi pamoja na wakuu wa nchi. Kubali kupokea Baraka kutoka kwa wengine na uwe mtu wa shukrani.

Tumia muda wako vizuri kupanga mambo ya kimaendeleo. Kumbuka watu waliokabiliana na matatizo makubwa ndio walioweza kufikia mafanikio makubwa kiroho, kiuchumi na kisiasa, kwa kuwa wanazikubali changamoto katika maisha, Leo tutaangalia jinsi ya kutokufuata mawazo ya wale wanaotaka kukurudisha nyuma kimaendeleo.

Miongoni mwa jamii tunazoishi, huwa kuna baadhi ya watu ambao hufurahia wenzao wanaposhindwa kutimiza malengo waliojiwekea, Ama huwa na tabia ya kuwakatisha tamaa wanaopenda kujikwamua kutoka katika hatua moja na kuelekea hatua nyingine.
Watu hao mara zote huwakatisha tamaa wenzao kwa jambo fulani, kwa kuwaambia kuwa, wasijaribu kulifanya kwa kuwa hawatafanikiwa. Kumbe watu hao, ilitakiwa kuwatia moyo wale wanaotaka kujikwamua kiuchumi kwa kuwaambia kuwa, wajaribu kufanya jambo walilolikusudia.

“Mawazo ya watu kama hao wasiopenda mafanikio ya wengine mara zote ni sumu ya maendeleo”. Hivyo unapokutana na watu kama hao, unachotakiwa kukifanya, ni kujiwekea mazingira ya kujikinga pale wanapokujia na kutaka kukulisha sumu hiyo.
Lakini kwa upande mwingine, wewe unayependa kupiga hatua kimaisha, unaweza kuyapokea mawazo ya wale wanaowakatisha tamaa wenzao, kama ni njia mojawapo ya kukutoa hapo ulipo na kupiga hatua zaidi.

Kamwe usiruhusu watu hao wasiopenda maendeleo yako kukukatisha tamaa kiasi cha kuharibu ratiba na mipango yako ya kimaendeleo uliyojiwekea. Kwa kuwa, watu wa namna hiyo wapo kila mahali, na kazi yao ni kuharibu mipango mizuri ya maendeleo ya wengine.
Huweza kutumia wengine kuyabeza mafanikio yako, kukucheka, na pengine huweza kukukopa baadhi ya bidhaa zako na kukuletea usumbufu katika malipo, ili mradi wewe uchukie na kuamua kuacha kufanya biashara uliyoianza.

Hizo ni changamoto zilizopo katika maisha yetu ya kila siku cha msingi, ni kusonga mbele na kufanya kile ulichokusudia bila kuangalia wengine wanasemaje juu yako ya kukurudisha nyuma. Wapinzani wa maendeleo ya wengine wapo kila mahali. Wengi wao ni wavivu hivyo wanashindwa kukabiliana na ugumu wa maisha, hupenda kuwakatisha tamaa wengine ambao wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika kufikia mafanikio wanayoyataka.
Usifanye makosa katika malengo yako.Kwa kuwa hata katika eneo lako la kazi, iwe ni ofisini ama kwenye biashara wapo wanaokukatisha tamaa ya kuendelea na mipango yako.


Kwa kuwa, katika hali halisi tumetofautiana kifikra na kimaendeleo.Miongoni mwetu wapo wale wenye mipango ya kupenda kupiga hatua kila wakati za kimaisha, na wapo wale ambaohupenda kuangalia wengine wanafanya nini na kuwabeza. Katika hilo, usikate tamaa. Piga hatua zaidi katika kufanikisha malengo yako kwa kuwa na mkakati wa kujiwekea kanuni ya kutafuta ushauri kutoka kwa watu wenye mafanikio zaidi yako. Ukijijengea tabia ya kuuliza maswali pale unaposhindwa, ni sawa na kutibu ugonjwa wa kansa unaokusumbua.

Vile vile ujue kuwa, katika maisha mafanikio yako pia yanategemea msaada wa kimawazo kutoka kwa wengine. Huwezi ukawa na mipango yako mwenyewe na mawazo yako mwenyewe ukafanikiwa bila kuomba ushauri kwa wengine walio mbali zaidi yako kimaendeleo, wale unaoweza kuonana nao na kuongea nao bila matatizo.

Changamoto za mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mafanikio. Bila kufanya kazi kwa bidii ni vigumu kupata mafanikio katika maisha. Njia mojawapo ya kufikia mafanikio hayo ni kuainisha malengo yako unayotaka kuyafikia.


*UPANGAJI MALENGO YAKO*

Jinsi unavyoweza kupanga malengo makubwa katika maisha yako. Watu wengi hushindwa kufikia malengo makubwa kwa kuwa, mara zote hujikatisha tamaa kuwa hawawezi kufanya jambo kubwa la kimaendeleo, kabla ya kujaribu kulifanya. Tabia ya baadhi ya watu hao wanaokuwa na malengo madogo katika mazingira wanayoishi, ina maanisha eneo hilo hakuna ushindani wa kimaendeleo,ama wao wenyewe hawana jitihada za dhati za kupiga hatua zaidi mbele

Lakini ikumbukwe kuwa, katika kutafuta mafanikio hayo ili uwe na maisha bora, usimwangalie mtu jinsi alivyo, kwamba ana urefu gani, ana pesa kiasi gani, digrii aliyonayo ama kuangalia historia ya maisha yake, bali hupimwa kwa uwezo wa kufikiri kwake. Watu wengi wanaofikiria kuwa na malengo makubwa ya mafanikio, katika maisha yao ni kutokana na matarajio waliyonayo.

Inakupasa kila mara ujitahidi kupanua mawazo yako na kubuni mbinu mpya za kukutoka hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi kimaendeleo. Hivyo utambue kuwa, unapotaka kufanya mambo makubwa inakupasa ujijue wewe ni nani na una thamani gani.Kwa maelezo mengine usijishushe hadhi yako kwa kuona kuwa huwezi kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo yatakutoa hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi.

MFANO

Tuangalie mfano wa kijana mmoja aliyeshindwa kupiga hatua mbele baada ya kujishusha hadhi yake na kujiona hawezi.Kijana huyo, aliona tangazo la kazi katika gazeti. Kazi aliyokuwa anapenda kuifanya na pia ameisomea. Lakini hakufanya jitihada za dhati za kuomba nafasi ile, kwa kuwa alijiona hawezi kuipata hata kama angeomba. Aliona kuliko ajitaabishe ni heri aache kuomba nafasi hiyo. Mfano huo si mzuri kwa mtu anayetaka kupiga hatua kimaisha.

Usijishushe hadhi yako ama usikatishwe tamaa kwa hali yoyote ile. Ni vema kujaribu kile unachokipenda na unachokihitaji katika maisha yako, kuliko kuacha kujaribu kwa kuogopa kuwa hautafanikiwa. Kwani matokeo huja baadaye, hata utakaposhindwa, utakuwa na nguvu ya kujaribu tena sehemu nyingine. Wengi wetu, tumekuwa tukijikatisha tamaa katika shughuli mbalimbali tuzifanyazo ama tunazotaka kuzifanya.

Yawezekana umeanzisha biashara kwa lengo la kukuinua kiuchumi, lakini matokeo yake, biashara hiyo haiendi kama vile ulivyotarajia. Jambo la msingi, inakupasa kukaa chini na kujitathmini, kuangalia ni sehemu gani unayokosea. Ama kuangalia, kama una washindani wengi katika eneo hilo, ili uweze kufanya vizuri zaidi yao, kwa kuweka kjvitu vingi tofauti na kuboresha eneo la biashara yako.

*UBUNIFU-CREATIVITY*

Kuwa mbunifu katika biashara yako kutakupa wateja wengi, na utafanikiwa zaidi. Cha msingi usikate tamaa katika kufikia malengo unayoyakusudia. Kutokana na hali ya kujikatisha tamaa, miongoni mwa watu wengi, wanasaikolojia mbalimbali wamekuwa wakishauri ni vema, watu wajijue vile walivyo ili waweze kujirekebisha pale penye upungufu na kusonga mbele kimaisha.
-Hali ya kujikatisha tamaa ni mbaya sana, ni sawa na ugonjwa usiopona katika mwili wako. Ili kuutibu ugonjwa huo, inakupasa ujielewe wewe ni nani, na una upungufu gani, pamoja na kukubali mabadiliko.

Tatizo kubwa lililopo kwa watu wengi, hawajui kuwa, wao wana uwezo mkubwa tofauti na wanavyojifikiria.Hivyo ni vema kuweka mawazo yako kwenye kipimo halisi, uyachuje na kuchukua yale yaliyo na thamani. Penda kufikiri mambo makubwa. Usijishushe hadhi yako kwa kujiwekea au kufikiri malengo madogo. Anza sasa kuwaza mambo makubwa ili uwe mtu mwenye ndoto njema ya maendeleo.

Kutokana na hali hiyo ya watu kujikatisha tamaa, wale ambao wamewahi kufanya biashara na kufilisika, wengi wao wamekuwa wakisema kuwa hawatarudia tena kufanya biashara hiyo.
Lakini kumbe, haikuwapasa kukata tamaa, bali kujipa moyo, na kuelewa kuwa pamoja na hali hiyo ya kushindwa inawapasa kujaribu tena. Kamwe usikate tamaa katika jambo lolote unaloliwaza ama kulifanya. Kwa kuwa, upo msemo mmoja unaosema, penye nia pana njia.

*MAFANIKIO HUTOKANA NA IMANI YAKO*

Ili kuwa mtu wa mafanikio ni vema kutumia mbinu ya ufikiri kwa ubunifu kile unachotaka kukifanya. Ni vizuri kuwa na imani, unaweza kufanya jambo lako na likafanikiwa, kwani unapoamini litafanikiwa, akili yako itazidi kutafuta njia ya kulifanikisha zaidi.

Kuamini kuwa unaweza kufanya jambo kubwa, kunafungua njia ya mafanikio. Kamwe usiseme ama kufikiri kuwa huwezi kufanya jambo fulani katika maisha yako, badala yake, jaribu kufanya kile unachofikiri kuwa huwezi. Usiruhusu mambo ya mila na desturi ama utamaduni uliouzoea kutawala akili yako. Kuwa mtu wa kupokea mambo na mawazo mapya kila wakati, kisha uyafanyie kazi.

Kila wakati jaribu njia mpya katika kufanikisha mambo yako, pamoja na kuwa mfuatiliaji wa shughuli zako unazozifanya. Iulize nafsi yako, inakupasa kufanya nini ili kuweza kufanya vizuri zaidi? Wakati unajiuliza swali hilo, unakuwa tayari umeshapata jibu, cha msingi ni kulifanyia kazi jibu hilo ulilolipata bila kuchelewa. Pia jiulize ni kwa vipi unaweza kufanya vizuri zaidi?

Pia ni vema ukawa na mazoea ya kusikiliza na kuuliza kwa wengine,kuhusu mambo unayotaka kuyafanya kwani utapata mawazo mengi usiyoyajua kutoka kwa wengine.
Yapanue mawazo yako, kwa kujichanganya na watu mbalimbali wakiwamo wenye ujuzi wanaoweza kukupa mawazo na njia mpya za kufanya mambo. Moja ya kanuni ya mtu anayependa au mwenye mafanikio ni kuwa na muonekano mzuri mbele ya jamii, kuanzia anavyozungumza hadi mavazi yake.

Unaweza usikubaliane nami, lakini ukweli ni kuwa, kama wewe ni mfanyabiashara wa nguo, jinsi unavyokuwa mtanashati mbele za watu, ndivyo watakavyopenda kuja katika duka lako na kununua bidhaa zako hizo. Lakini, kama utakuwa haujijali kwa upande wa mavazi, halafu ukawa mfanyabiashara wa bidhaa hiyo, utapata wateja wale wasiokujua na wanaokujua wachache.

Utanashati unavutia biashara yako, si tu kwa biashara ya nguo, bali hata katika shughuli zako nyingine unazozifanya, uwe ni mwanasheria, mwalimu ama mpishi wa chakula, vile unavyoonekana ndivyo unavyozidi kuimarisha biashara yako. Kumbuka watu wanakutathmini kutokana na muonekana ulio nao. Hebu tuangalie mfano huu kuwa, mtu anafanya biashara ya nyanya, anazipanga mafungu mafungu na kuziuza. Mwingine anafanya biashara hiyo hiyo, na kuziweka nyanya zile katika mfuko wenye kuonyesha bidhaa iliyopo ndani yake na kufunga vizuri.

Biashara hizo zikiwa katika eneo moja, watu wengi watanunua zile zilizofungwa vizuri kwenye mfuko wakiamini kuwa ni salama zaidi. Mfano huo ni sawa na muonekana ama utanashati wako kwa watu katika shughuli yoyote ile unayoifanya. Uvaaji mzuri na wa heshima kwenye jamii, unakufanya uheshimike na kuaminika kuwa unaweza kufanya mambo makubwa unayoyapanga.

Ni vizuri kuboresha mawazo yako kila siku, kama watu maarufu wanavyokuwa.
Kuboresha mawazo, kufikiri na utendaji wako kutakuletea mafanikio katika mipango yako yote.
Hivyo ni vema, kula vizuri ili uweze kufikiri vizuri katika mambo unayoyafanya.
Endapo hautakula mlo kamili, akili yako haitakuwa na uwezo wa kufikiri vizuri, utabakia kuwa mtu wa kushindwa. Kama mtu anakula vizuri, anajilinda na magonjwa mbalimbali, mwili wake unakuwa na afya pamoja na akili yake kuwaza mambo makubwa.

*Akili yako huwezi kuilisha chakula unachokula, bali chakula chake ni mazingira yanayokuzunguka.* Mtu yeyote anayetembea katika nchi ama mikoa mbalimbali, huwa na mazingira ya tofauti, kila anapokwenda hujifunza kitu kitakachomsaidia. Mazingira ya eneo ulilopo yanaifanya akili yako ifikiri zaidi ufanye kitu gani cha mafanikio katika eneo hilo ulilopo kitachokupatia maendeleo.Ukubwa wa jinsi unavyowaza, malengo yako, mazingira yako au vile unavyoonekana, ni kutokana na mazingira uliyopo.

Unapokuwa na watu wenye mawazo ya kuchelewa kufanikisha mambo, nawe utakuwa mtu wa kuchelewa kufikia malengo uliyojiwekea. Kwa maana nyingine, kushirikiana na watu wenye mawazo makubwa kunakufanya uwaze mambo makubwa ya maendeleo.
Pia kukaa karibu na watu wenye malengo ama maono ya mafanikio, kunakufanya nawe uwe katika hali hiyo.Kuna msemo usemao  *nionyeshe rafiki zako, namimi nitakuambia wewe ni nani*

_NB: Katika jamii tunayoishi, kumekuwa na watu wenye tabia zilizogawanyika katika makundi matatu._

Kundi la kwanza, ni la watu wale ambao wameona kuwa hawawezi kufanya jambo likafanikiwa kabisa. Wamekuwa na ujuzi na kukubali ujuzi huo katika eneo moja, yaani wameridhika na hali hiyo. Kama, Mungu amekupa ujuzi wako mzuri na ukabahatika kupata kazi sehemu nzuri, pamoja na kufanya kazi ile, utumie ujuzi wako katika maeneo mengine.
Unaweza kufungua ofisi yako na kuanzisha kitu chako mwenyewe huku ukiendelea na kazi yako.

Kamwe usijikatishe tamaa kwa kuona kuwa huwezi kufanya hivyo, kudhani kuwa, wewe umeumbwa kwa ajili ya kufanya kazi za wengine tu. Kuna watu wenye malengo makubwa na waliopanga kuyatimiza lakini kutokana na ushindani uliopo hufika mahali na kushindwa kuendelea na mikakati waliyojiwekea.Tunaweza kusema, wamekata tamaa na kuacha kuyafanyia kazi malengo yao, mwishoni hupoteza mwelekeo kabisa.

Kundi hili, wamejijengea tabia ya hofu, hofu ya kushindwa kutimiza malengo yao, hofu ya ulinzi, hofu katika jamii inayomzunguka na kupoteza kila wanalicho nacho.
Kundi la watu hawa, kamwe hawatafanikiwa kwani wameshajiweka kwenye kundi la kushindwa ingawa lina watu wenye akili, vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Kundi la tatu ni la watu wale ambao hawako tayari kukatishwa tamaa, hawa ni asilimia ndogo sana katika jamii.

Kundi hili pamoja na kukatishwa tamaa, katika mipango yao, wamekuwa wakijitahidi kufanya jitihada mbalimbali ili wajikwamue katika hali hiyo waliyonayo na kuwa katika hatua nyingine.
Mara zote hupumua mafanikio katika maisha yao. Kundi hili pia lina furaha kwa kuwa limeshakamilisha baadhi ya malengo waliyojiwekea. Wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali, lakini wamezishinda, wamekuwa wakiangalia siku mpya ikianza na jambo jipya. Ni ukweli usiopingika kuwa, kila mmoja wetu anapenda kuwa katika kundi la tatu, ambalo kila mwaka wanapata mafanikio, wanaofanya mambo mbalimbali na matokeo yake yanaonekana.


*MATOKEO YA MAONO* (The Impact of Vision)

*Katika maisha kuna nyakati tunapaswa kupanda katika vilele vya milima yetu binafsi ili tuweze kuuona mustakabali wetu (our future) kutokea katika kile kiwango cha juu tulikosimama*         (Dr. John Tibane)

*Mafanikio katika maisha ni safari, ila kuweza kukaa katika safari hii kunahitaji msukumoKatika maisha kunanyakati tunapaswa kupanda katika vilele vya milima yetu binafsi ili tuweze kuuona mustakabali wetu (our future) kutokea katika kile kiwango cha juu tulikosimama.* (Dr John Tibane).

Mafanikio katika maisha ni safari, ila kuweza kukaa katika safari hii kunahitaji msukumo wa ndani  pamoja na ujasiri. Bila vitu hivi muhimu wengi wetu hukata tamaa njiani na kuiahirisha kwa urahisi safari yao kuelekea mafanikio. Ni kwa jinsi unavyoupenda mustakabali wako na ni kwa jinsi unavyoipenda kesho yako ndiko kutakakokupa msukumo wa ndani pamoja na ujasiri. Ili kuweza kuiona kesho yako au mustakabali wako pasipo vizuizi inahitaji msaada wa kimungu (divine assistance) katika hali ya rohoni.

Kati ya siri mojawapo inayoweza kukusaidia ni kuandika katika karatasi nini unachokiona katika kesho yako, je unaona uzuri, furaha, amani, utajiri, mafanikio, au afya? Andikainawezekana kuwa ni kwenye chumba chako cha sala au sehemu unayopenda kuitumia kufikiria au kuwaza kiundani mambo ya maisha yako (meditation space).


Ili sasa kuianza safari yako kuelekea nchi yako ya ahadi, inakupasa kushuka chini kutoka mlimani ulikokuwa na kuja ardhini (In reality). Kumbuka kuwa kilakitu unachokiona huku chini katika ardhi kinaweza kuwa ni tofauti kabisa na vile ulivyoviona ukiwa juu katika kilele cha mlima, sasa unalazimika kuendelea kushika vema yale maono yako ya kweli uliyoyaona ukiwa juu, hata kama uhalisi unaoonekana huku chini ni tofauti. Utaanza kuishi na kutembea katika kuyafikia maono yako ukiwa hapa chini lakini si kama unavyoyaona mambo ukiwa chini bali kama ulivyoyaona ukiwa pale kileleni juu. Hii ndiyo tunayoiita ‘imani’  hakika ya mambo yatarajiwayo na bayana ya yale yasiyo onekana katika uhalisi hapa chini bali kama yalivyoonekana tukiwa kileleni pale juu.


Pasipo maono watu huangamia, maisha ya watu huharibika kabisa, watu huishi kihasara hasara tofauti na walivyo tazamiwa kuishi. Wanakosa uwezo wa kujitawala na kuwa na kiasi, wanakuwa watu wasiotawalika na waharibifu. Maono ya kweli  yanatupa kujiweza, kujitawala wenyewe, kuvumilia na kuwa na matazamio mema. Msukumo wa ndani na ujasiri huzaliwa kutoka katika maono ya kweli.


*Faida za maono .*

1.    
       *1. Maono ya kweli huyatia nguvu maisha yako.*

Maono ya kweli hukupa sababu na maana ya kwanini unaishi. Unatiwa msukumo, unahamasishwa, ni kama vile simu inapokosa chaji inalazimika kuwekwa katika umeme ili iweze kuongeza uwezo wa kufanya kazi. Maono ya kweli ni kama nguvu ya umeme ndani yetu. Maisha yako yanakuwa yaliyojaa, huna muda wa kupoteza kuanza kuongelea watu na kuchunguza maisha ya watu wengine na kamwe hutopata tatizo la kujihisi mpweke usiye na chakufanya.


2.      *2. Maono ya kweli huzikutanisha pamoja nguvu au nishati zilizopo ndani yako.*

Ndani yako una nguvu na nishati mbalimbali kama vile nguvu za kiroho, kimwili, kihisia, kiakili na nyingine nyingi. Nishati hizi ni kama vile miale ya mwanga ambayo inachomoza kutoka kwako. Maono ya kweli yanakuwa kama kioo kinachokuza (magnifying glass) kinachokutanisha miale yote hii katika sehemu moja, na hapa ndipo nguvu zako au nishati zako huweza kutumika katika kiwango cha juu zaidi cha ufanisi na matokeo bora zaidi.


3.     *3.Maono ya kweli hurekebisha tabia zetu*

Kile ulichoweza kukiona ukiwa pale kileleni mwa mlima wako binafsi kinauwezo wa kubadilisha tabia zako. Kinakufanya ushindwe kufanya kitu chochote cha kipuuzi ambacho kinaweza kuiharibu kesho yako nzuri uliokwisha iona ukiwa pale juu, kinakufanya uwe makini sana katika maamuzi unayoyafanya kila siku. Jinsi unavyo fikiri, jinsi unavyo zungumza na hata kutenda inakuwa kama vile tayari umeshafika kwenye ile nchi ya ahadi uliyoiona ukiwa pale juu. Maisha na mizunguko yako ya kilasiku yanaongozwa na maono yako ya kweli.


4.      *4. Maono ya kweli yanazishinda hofu zako.*

Kwa kawaida kitu chochote unachokiangalia kwa mkazo hupanuka na kuwa kikubwa. Kama utayatilia mkazo  matatizo yako basi yataongezeka na kuonekana makubwa na hatimaye kukuogopesha. Unapoogopeshwa au kutishwa na tatizo fulani unakata tamaa katika kulitafutia ufumbuzi na kuendelea mbele. Watu waliofanikiwa kamwe hawachagui kuyatazama matatizo yao (kama yanavyoonekana wakiwa chini ya mlima) bali huzitazama fursa mbalimbali za mustakabali wao (kama zilivyoonekana wakiwa kileleni). Kwa jinsi utakavyozidi kuyatazama mafanikio, fursa zitapanuka na zitaongezeka na kukushawishi katika kuendelea na safari yako ya mafanikio. Upendo wa kweli kupitia maono ya kweli huziweza hofu zote.


5.      *5. Maono ya kweli yana uwezo  wa kuvuta msaada.*

Maono ya kweli wakati wote yanauwezo wakushawishi kila aina ya msaada uhusianao na maono hayo kuja, kama ni watu, fedha, vibali, na vitendea kazi vingine. Wako watu wanakila kitu lakini wamekosa tu maono, wanasubiri vile walivyo navyo vivutwe kwa sumaku ya maono ya kweli ili viende kutumika kule kuliko sahihi.  Wako watu wamezaliwa ili tu wawe msaada wa maono uliyonayo. Wanasubiri kwa hamu wewe uyaandike maono yako.


Ili kuhesabiwa pamoja na waliofanikiwa inakudidi uweze kuyaangalia mambo katika kiwango cha juu zaidi ili uweze kupata maono ya kweli ambayo yatazaa uwezo wa wewe kuipenda kesho yako.

*son of Alpha and Omega*
*0712412170*
*PROPHET DERICDADY*

Saturday, September 1, 2018

*NJIA ZA KUEPUKA HASIRA.*

1: *Epuka Mabishano*: Mara nyingi hasira hupandishwa na mabishano baina ya mtu na mtu/watu.
Njia kubwa na rahisi ya kuepuka kupandwa na hasira, ni kwa kuepuka kubishana na mtu au watu, hasa wale wanao onekana wagumu kuelewa.
Penda kuepuka kujibizana au kumjibu  mtu kwa ukali.

2: *Penda kujishusha*: Unapogundua umemkwaza mwenzako, na akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu na yenye ukali, basi penda kujishusha na kuzungumza kwa utaratibu, au kuomba radhi.
Hii husaidia kumshusha hasira mwenzio, kushuka kwa hasira kwa mwenzio husaidia kushusha yako pia.

3: *Jifunze kuwa na matumizi mazuri ya kinywa*:
Mara nyingi kinachompandisha mtu hasira huwa ni kauli chafu.
Jifunze kuwa na kauli njema itakusaidia kuepuka migogoro ambayo itakufanya upandwe na hasira au umpandishe mwenzio hasira.
Hasa kauli zenye kujaa matusi, kejeli, au dharau hupandisha mtu hasira.
Na sauti yenye ukali, kukoroma, au ukaripiaji, humpandisha mtu hasira.

4: *Penda kudharau watu*:
Dharau tunayo izungumzia hapa sio ile dharau ya kumbinulia mtu mdomo, wala kumshusha na kumpandisha macho.
Hapana, kudharau means "Humpi mtu attention anayoitaka ili kugombana na wewe "

Ukiona mtu anakutusi, analeta kejeli, au hata kuleta shari.
Njia pekee ya kumuepuka ni kwa kumdharau kama mtu asiye na akili, aliyekosa heshima na maadili.
Hivyo hujibizani nae, wala kumpa attention anayoitaka.

5: *Penda kuheshimu upeo wa mtu*:
Binadamu tumetofautiana upeo wetu wa kutafakari, kuelewa, na kujibu jambo, hivyo sio kila wakati mtu atakujibu au kufikiria kama ulivyotaka akuelewe.
Ukiona umemuambia mtu kitu halafu akakujibu hovyo, basi chukulia kama ndipo uwezo wake kufikiri ulipoishia.
Kama unaweza kumrekebisha basi tumia lugha safi, na sauti iliyojaa upole, na umueleweshe kwa hoja zilizo jaa hekima na busara.
Kumjibu hovyo pia huweza kuleta mtafaruku kati yenu.

6: *Jifunze kuishi na watu:*
Binadamu tumetofautiana historia zetu, kuendana na jamii tulizo ishi na aina ya maisha tunayopitia.

Kuna watu ukali, kupenda ugomvi, hasira za karibu, gubu/ulalamishi, ndio tabia zao.
Hata ukizungumza jambo la kawaida huwa wanalikuza.
Hivyo ni vyema kujifunza kuishi na watu wa aina hii, na njia pekee ni kuepuka kujibizana nao.

7: *Penda kusoma mood ya mtu:*
Ukiona mwenzio kapandwa na hasira, usijibizane nae.
Ukiona yuko na uchovu, usipende kumsumbua wala kumlalamikia jambo.
Ukiona yuko na stress, mpe tulizo, usimsumbue wala kumkaripia.
Ukiona yuko na hofu kupindukia, usimtishe kwa lengo la kumcheka, mpe tulizo.
Ukiona ana huzuni aidha amefeli jambo, au amefungwa team yake, au ameondokewa na kitu, au kakikosa, basi ni vyema kumfariji badala ya kumtamkia maneno ya kukera, kuudhi, dharau, au kejeli.
Hii itakusaidia kuepuka kugombana nae.

8: *Penda kuelimisha:* Wengi wetu tunapenda kuwa walalamikaji, ukaripiaji, na ndio tunachukulia kama njia sahihi za kutoa madukuduku yetu.
Tunakosea sana, hapo lazima utamkera mtu.
Njia nzuri ni kujifunza kumuelimisha mwenzio pale anapokosea, kumshauri, na yote yatumie sauti tulivu na kauli nzuri.
Hii itasaidia kuepuka ugomvi, achana na tabia ya kumtukana, kumlaumu, kumkaripia mwenzio.
Hii itampandisha hasira, na itakupandisha hasira wewe pia pindi ukijibiwa hovyo.

Hizo ni njia ya kuepuka wewe kupata hasira, pamoja na kuepuka kumpandisha hasira mwenzio.

*NJIA ZA KUTIBU HASIRA YAKO.*
- Ukiona ushaanza kupandwa na hasira ni vyema kukaa kimya, epuka kujibizana na mtu ili kuepuka ugomvi, au kuepuka asikujibu mambo yatakayo kupandisha hasira zaidi.
Au kama unaweza basi badilisha mada, au kama haiwezekani, endelea kunyamaza ili kuepusha shari.

- Jifunze jinsi ya kukaa na mtu mwenye gubu, lawama, ukiona kashaanza lawama tu basi shusha sauti yako haraka sana, au nyamaza, au omba udhuru utoke mara moja.

- Mtu anapokuudhi jifunze kubeba maumivu,  vumilia na ujishushe sababu kuendelea kujibu kwa ukali hukufanya uzidi kupandisha hasira.
Hii itakusaidia kipindi uko kwenye sehemu ambayo huwezi kuondoka karibu na aliyekuudhi...mfano: Kwenye daladala.

- Ukiona ushaanza kukasirika basi ondoka mahali penye mabishano.

- Ukipandwa na hasira, epuka kukaa karibu na aliyekuudhi, au kukaa karibu na silaha yeyote.

- Pata glass moja ya maji pindi unapoona hasira zimekupanda.

- Ukijijua una hasira kali zinazoweza leta madhara, ni vyema ukajizuia kufanya maamuzi yoyote.
Na njia sahihi ni wewe kukaa mbali na eneo la tukio.

- Kusali/kuswali husaidia kushusha hasira.

- Kuna nyakati inakuwa ngumu kuzizuia hasira sababu uko katika mazingira ambayo huwezi kuondoka, na huwezi kuvaa earphone ili usimsikilize sababu ni mtu unaye muheshimu.
Hapa ndipo unapotakiwa kujifunza kuwa kuidhibiti hasira huanzia ndani ya nafsi yako mwenyewe.
Nyamaza kimya, msikilize yeye.
Anza kujenga mawazo ya kitu kingine tofauti "Mfano: Dah lile pilau la jana".
Hii itakusaidia kuufanya ubongo wako usitafsiri zile kelele zake zinazopita masikioni mwako.
Na kuufanya ubongo uwe na mawazo tofauti kabisa.

Unadhani hii inafanyaje kazi???
Hebu fikiria, ulishawahi kuwa darasani,  mwalimu anafundisha, lakini mawazo yako mbaali.

Mwisho unastukia kipindi kimeisha na hujui kilichofundishwa.

*MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.*

- Epuka kubaki na kinyongo au chuki kati yenu, jifunze kusamehe pale hasira zinapoisha.
Na kama ni mtu wa karibu, basi ni vyema mkaya suluhisha au kusameheana bila kuombana msamaha.
Chuki huzalisha madhara mengi zaidi.

- Epuka kununa nuna baada ya hasira kuisha, hii itakusaidia kukuacha huru bila stress za mtu yeyote.
Onyesha tabasamu pale hasira zinapoisha.

NB: Wanaume ni vyema kujifunza kuwa mpenzi wako akikununia baada ya kukorofishana, haimaanishi kuwa ndo hataki kuwa na wewe tena.
Wengine hununa kwa nia ya kutaka kubembelezwa, anahitaji kuiona thamani yake kwako.
.
Hata hivyo, hizi ni njia ambazo wewe utazitumia kuendana na eneo ulilopo, na ukubwa wa tukio.
Mara nyingi ukifatilia wanaopandwa na hasira huwa inatokana na wao kupenda kujibizana na mtu, tena kwa maneno ya kukera, na sauti ya juu.
Hapa lazima utapandwa tu na hasira, na mwenzio atapandwa na hasira.
Mwisho mnapigana.
.
Ukitazama sana watu wanaoudhi wenzao, utagundua ni kwasababu hawajui kusoma mood za wenzao, hawajui kutumia vinywa vyao vizuri ili kuwasilisha jambo.
Wanapenda kulalamika sana na kutumia kauli chafu na sauti kali.
.
Mungu awabariki sana na kuwafanyia wepesi.
Amen.

*Jifunze kuwa kimya HASIRA  inatibika*

*son of Alpha and Omega*
   0712412170