Monday, June 4, 2018


 JIFUNZE KOZI HII YA UCHUNGAJI.
MASOMO HAYA YOTE UKIMALIZA UMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA UTUMISHI.



SOMO LA 1
MUNGU


1.1  Uwepo wa Mungu

“Mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kuwa yeye yupo  na
kwamba huwapa dhawabu wale  wamtafutao” ( Ebr 11:6). Lengo la
masomo haya ni kuwasaidia wale wanomwendea Mungu, wakiisha
mwamini “Kwamba yupo”; kwa sababu hii hatutajitia  kwenye
ushahidi usiothibitisha  imani ya kuwa Mungu hayuko.katika
kupima muundo wa miili yetu (Zab 139:14)  Ushahidi wa kielelezo
katika ua, Kukazia macho juu kwenye anga pana wakati wa usiku
kukiwa wazi  bila mawingu, haya na mengine yasiyohesabika,
Mawazo ya kangaliifu juu ya maisha,  hakika yanafanya imani ya
kutosadiki kuwa Mungu hayupo iwe ni ya kushangaza. Kusadiki
kuwa Mungu hayuko  hakika inahitajika imani zaidi  kuliko
kuamini yupo,pasipokuwepo Mungu mpangilio haupo, Kusudi au
kutoa maelezo ya asili  ya Ulimwenguni  basi hii itafikiriwa katika
maisha ya mtu asiyeamini kuwa Mungu yupo. Tukikumbuka hili,
siyo ajabu kuwa watu wengi  wanakiri kwa kiwango fulani  cha
kumwamini kuwa Mungu yupo hata katika jamii ambayo vitu vya
mwili  ni Mungu  anayeshinda maisha ya  watu.
   11


Lakini ipo tofauti pana kati ya kuwa na fikra isiyodhahiri ya
kwamba ipo nguvu ya juu, na hasa kweli kuwa na uhakika kwa kile
ambacho Mungu anampa mtu anayemtumikia kwa Uaminifu.
Waebrania 11:6  jambo hili tunasoma;

 “Yatupasa tuamini kuwa (Mungu )yupo na
 Kwamba huwapa thawabu  wale wamtafutao kwa bidii”

Maelezo mengi ya biblia ni historia ya watu wa  Mungu
Israeli; mara kwa mara neno limetolewa kwamba kukubali kwao
kuwa Mungu yupo hakukulingana  na imani zao kwa ahadi
zake.Waliambiwa na mkubwa kiongozi wao Musa'Kwa hiyo
ujue…….Ukaweke moyoni mwako, ya kuwa BWANA ndiye
Mungu  katika mbingu juu, na katika nchi chini,  hapana mwingine.
Basi, zishike sheria zake,  na amri zake  (Kum. 4:39:40).
Neno hili hili limetolewa  - ufahamu wetu katikati yetu ya
kuwa  Mungu yupo hakumaanishi kwamba tunakubalika mbele za
Mungu bila kufikiri.Ikiwa bila mchezo  tunakubali kwamba kwa
kweli tunaye  Muumba,'Kwa sababu hiyo tuzishike sheria na amri
zake’ Ni shabaha ya  mfululizo huu wa masomo kuelezea  amri hizi
jinsi zilivyo na namna ya kuzishika. Tunapochungunza maandiko
kwa kufanya hivi, tutakuta kwamba imani yetu kuwa Mungu  yupo
inatiwa nguvu.

‘Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la
Mungu’ (Rum 10:17). Vile vile,(Isaya 43:9-12) yaonyesha namna
ya kufahamu unabii wa  Mungu kuhusu wakati ujao - Unabii
unatufanya tujue'kuwa mimi ndiye’ (Isa. 43:13)- yaani  hilo jina la
Mungu, 'Mimi niko ambaye NIKO’ kwa ukamilifu ni kweli (Kut.
3:14.)  Mtume Paulo alifika kwenye mji unaoitwa Beroya, eneo hili
kwa sasa liko kaskazini mwa Uyunani ( Ugiriki) kama kawaida,
12

akahubiri injili (Habari njema) ya Mungu; lakini badala ya watu
kusikia neno la Paulo alilokuwa anasema, tunasoma kwamba, “
Walilipokea kwa kusikia neno (la Mungu, sio la Paulo) kwa
uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone
kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Basi watu wengi miongoni
mwao wakaamini  ( mdo 17:11,12)

Imani yao ilikuja kwa kuwa mioyo yao ilikuwa wazi, sawa
sawa (‘ Kila siku’)  na kwa utaratibu wa (‘mambo hayo’)
waliyachunguza katika Biblia, Basi  kupata imani ya kweli haikuwa
Mungu aliwafanya wawe nayo ghafla kwa aina fulani ya upasuaji
wa moyo wa kiroho,  pasipo kujihusisha na neno la Mungu. Ni jinsi
gani basi watu wa Ulimwengu  wanaweza kufuata kwa moyo
pigano juu ya  maovu  la Bill Graham au  uamsho wa mikutano ya
wapentekoste kisha wanahama  tena  kama'Waamini’ ? Ni muda
gani wameendelea katika masuala haya  wakiwa wanachunguza
maandiko kila siku ?  Kwa kweli kukosekana huku kwa imani
ambayo msingi wake upo kwenye Biblia bila shaka kunaonyesha
utupu wa'Waongofu’  hawa na kujikuta  baadae kwa wanayopata
Wakristo,  na ni kwa sababu gani wengi wanaondoka  kutoka
kwenye Ushirika  wa Madhehebu ya wa-Injilisti.
 
Masomo haya  lengo lake ni kukupa mjengo wa  utaratibu
wako mwenyewe  kuchunguza maandiko, ili kwamba nawe pia
uweze  basi kuamini muunganiko kati ya kusikia  Injili ya kweli na
kuwa na imani  ya kweli mara  nyingi kumejitokeza wazi  katika
taarifa ya kuhubiri injili.

• “Wakorintho wengi waliposikia waliamini wakabatizwa”
(mdo 18:8)
• Watu wasikie neno la Injili, waamini ( mdo 15:7)
• Ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini'(1 Kor. 15:11)
   13

• ‘Mbegu’  Kwenye mfano wa mpanzi  ni neno la Mungu
(Luka 8:11) wakati katika huo wa mti wa haradali  ni imani ( Luka
17:6) kwa kuona kwamba imani huja  kutokana na kupokea'Neno
kwa imani’ ( Rum 10:8) “Maneno ya imani,  na mafundisho
mazuri” ( 1Tim 4:6), katika moyo ambao upo  wazi kumwamini
Mungu  na neno lake  (Gal 2:2, Ebr 4:2)

• Mtume Yohana anaisema taarifa  iliyoandikwa ya maisha
ya Bwana  kuwa anasema' kweli ( Yaani ukweli) ili nanyi mpate
kusadiki’ ( Yohana 19:35).Basi neno la Mungu  limeitwa
‘Kweli’(Yoh:17:17) ili mpate  kuamini.

1.2 Nafsi yake Mungu

Ni mwenye enzi, Mungu aliyeandikwa katika Biblia  na
kwamba ni kweli, mtu wa kugusika, naye yupo katika umbo.
Vilevile ni mafunzo ya kwanza  ya Ukristo  kuwa Yesu ni mwana
wa Mungu. Ikiwa Mungu hana umbo , basi  haiwezekani yeye
kuwa na mwana  ambaye alikuwa ni 'Chapa ya nafsi yake' (Ebr 1:3)
Tena  inakuwa vigumu kuendeleza  maisha ya uhusiano wake na
mungu  ikiwa Mungu  ni wazo lililo kwenye akili zetu,
Mkusanyiko wa roho  mahali popote juu katika  anga lisilo na kitu.
Ni huzuni  kusikia kwamba dini za watu wengi  zina wazo lisilo la
kweli  lisilotambulika kuhusu Mungu. Yeye akiwa mkubwa mno
kuliko sisi,  inaeleweka ya kwamba imani  ya watu wengi imeweka
kikwazo kwenye ahadi  dhahiri  kuwa mwishowe tutamwona
Mungu. Israeli  walikosa imani ya kumwona Mungu  alivyo  (Yoh.
5:37) ni dhahiri ana umbo halisi, Imani hii huja kutokana na
kumjua Mungu kwa kuamini neno lake

14

 Heri walio safi wa moyo, Maana watamwona Mungu (Math
5:8)
Na watumwa wake (Mungu) watamtumikia, nao watamwona
uso wake, na jina   lake(Jina la Mungu ) litakuwa katika vipaji vya
nyuso zao (Uf 22:3-4)

Tumaini hili la ajabu kama kweli tunaliamini litaonyesha
matokeo ya matendo  kwenye maisha yetu:

• Tafuteni kwa  bidii kuwa na amani  na watu wote  na huo
utakatifu, ambao hakuna mtu atakaye mwona  Bwana asipokuwa
nao (Ebr 12:14)
• Tusiape, kwa kuwa  aapaye kwa mbingu,  Huapa kwa kiti
cha  Mungu na kwa yeye  na kwa yeye aketiye juu yake  ( Math
23:22) hii itakuwa haina maana ikiwa Mungu  sio mtu mwenye
mwili.
• Tutamwona kama alivyo (akidhihirika katika kristo ) na kila
mwenye matumaini  haya katika yeye  hujitakasa, kama yeye
alivyo mtakatifu (1 Yoh 3:2,3)

Katika maisha yetu haya kumfahamu Mungu wetu wa
mbinguni,  hakujakamilika sana. Tunaweza kutazama mbele,
kupitia giza linalotatanisha la maisha haya hadi mwisho wa
kukutana naye. Kumwona kwa macho yetu hapana shaka kutakuwa
sawa na kumfahamu kwa akili  zaidi. Kutoka vina vya masumbufu
ya mwanadamu. Ayubu aliweza kufurahia  uhusiano wake wote na
Mungu  ambao utimilifu wake  atauona mwisho wa siku.

Na  baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi (Yaani katika
mauti),Lakini pasipokuwana mwili wangu  (Yaani pasipo mwili
unaoharibika ) nitamwona Mungu;Nami nitamwona mimi nafsi
yangu,na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine (Ayubu
   15

19:26,27). Mtume Paulo aliyatazamia maisha mengine  yasiyo
machungu  yasiyo na msukosuko: “Maana wakati wa sasa tunaona
kwa kioo kwa jinsi  ya fumbo; Wakati ule tutaona uso kwa  uso” (
1Kor 13:12)

USHAHIDI WA  AGANO  LA  KALE
Ahadi hizi  zilizo katika Agano Jipya  zimejengwa juu kwenye
ushahidi wa mambo yake makubwa  ya  Agano la kale, Kuwa ni
Mungu aliye na mwili. Ushahidi hauwezi kukaza zaidi  lakini ni
mwanzo wa kukubali  hali ya Mungu kama tunataka kuwa  na
ufahamu wa kweli  yoyote  kuhusu dini ambayo msingi wake  upo
kwenye Biblia. Agano la Kale lina mazungumuzo ya Mungu kuwa
ni mtu na mtu uhusiano wa mtu na mtu pamoja  Mungu, ambao
Agano la Kale na Jipya linausema  ni wa pekee kwa  tumaini la
Ukristo  wa kweli. Yafuatayo ni majadiliano ya nguvu  kwa ajili
yake, Mungu aliye na mwili.

“Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura
yetu” (Mwa. 1:26) Hivyo mtu amefanywa kwa mfano  na sura ya
Mungu, Kama ilivyodhihirika kupitia Malaika. Yakobo 3:9
anasema … Wanadamu waliofanywa kwa mfano  wa Mungu.
Maneno haya hayatumiki kutaja  mfano wa akili ya mwanadamu,
kwa kuwa hali ya fikra zetu  zipo mbali kabisa toka zake Mungu na
katika njia nyingi  kwa kikubwa  zimepingana na haki
yake.”Maana  mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si
njia zangu, asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu  zilivyo
juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu  zi juu sana  kuliko njia
zenu, na mawazo yangu  kuliko mawazo yenu” ( Isa 55:8 - 9 ).
Kwa hiyo mfano na sura, tunavyoshirikiana naye Mungu, inabidi
uwe ni mfano wa mwili- Lakini yeye hana wa dhambi.
 
16

Popote Malaika  walipoonekana duniani wamesemwa kuwa
wana umbo la watu, kwa mfano, Abrahamu aliwakaribisha malaika
bila kujua, akizania kuwa walikuwa watu wa kawaida. Sisi jinsi
tulivyoumbwa kwa mfano wa Mungu kwa kweli maana yake ni
kwamba tunaweza kufahamu  jambo lingine kuhusu mtu halisi,
ndivyo tulivyo, lakini tunafanana. Basi,  Mungu tunaye mshabihi
siyo mtu mwingine asiyedhahiri ambaye hatuwezi kumfikiria.

“Wao wenyewe Malaika wanafanana na Mungu. Hivyo
Mungu aliweza kumsema Musa, “Kwake nitanena mdomo kwa
mdomo, maana wazi wazi wala si kwa mafumbo. Na umbo la
Bwana yeye ataliona” (Hesabu 12:8) Haya yalikuwa yanamtaja
Musa, akifunzwa na Malaika  aliye kuwa na jina la Bwana (Kut.
23:20:21) Ikiwa Malaika alikuwa na umbo la Bwana, Inaonyesha
kuwa Mungu amefanana na Malaika  Yaani - Kimwili  ana umbo la
Mwanadamu. “BWANA alisema na Musa uso kwa uso  kama vile
mtu asemavyo na rafiki yake. (Kut. 33:11: Kum. 34:10 ). Bwana
alijidhihirisha katika Malaika wake, ambaye uso na kinywa
alifanana na Bwana mwenyewe.

 “Kwa maana yeye anatujua umbo letu,  (Zab. 103:14).Ana
tutaka yeye,  tumfikirie kuwa ni mtu, Baba ambaye tunaweza
kuunganishwa naye.Huyu ataelezwa kwa ushahidi mwingi  wa
mikono ya Mungu, Viganja,Macho  n.k. Ikiwa Mungu alikuwa ni
furushi la Nafsi mahali fulani katika mbingu, ambazo inabidi ziwe
Mungu, ni wazo letu kama tukitaka utu wake;  basi ushahidi huu
unatupotosha kukuza  kusudi lolote.

 “Maelezo ya sehemu ya makao ya Mungu, Wazi wazi
yanaonyesha kwamba “Mungu” ana mahali pake; “Mungu yuko
Mbinguni”( Mhubiri 5:2);Maana ametazama toka patakatifu pake
pa juu, toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi (Zab 102:19,20);
   17

“Usikie huko mbinguni, Makao yako” (1Fal. 8:39). Lakini kwa
kupambanua zaidi kuliko hivi tunasoma kwamba Mungu ana “Kiti
cha Enzi” (2 Nya. 9:8, Zab 11:4; Isa. 6:1,66:1).Lugha kama hii ni
ngumu  kuitumia nafsi isiyo wazi  kabisa, inayokaa katika milki ya
Kimbingu. Mungu amesemwa kuwa “Ameshuka kuja chini”
wakati mwenyewe anapojidhihirisha. Hapa panadokeza  makao ya
Mungu yaliyo mbinguni. Inakuwa vigumu kueleza wazo  la
udhihirisho wa Mungu  bila kukubali hali ya umbo la Mungu. Isaya
45 ina ushahidi tele wa Mungu  kujihusisha kwake  katika mambo
ya watu  wake: “Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine …..,
mimi ni  BWANA anayetenda haya yote …., Mimi, BWANA
nimeiumba Ole  wake ashindanaye na Muumba wake … Mimi,
naam, mikono yangu mimi,  imezitanda mbingu …, niangalieni
mimi mkaokolewe, enyi ncha zote  za  dunia. mstari hasa kweli huu
wa mwisho  unaonyesha uwepo wake Mungu - Anawataka watu
wamwangalie yeye, Kuwaza uwepo wake  halisi pamoja na jicho la
imani.

Mungu amejifunua  kwetu akiwa ni mwenye kusamehe
anayesema, maneno kwa watu. Hata hivyo msamaha  na usemi
unaweza  tu kutoka kwa mtu: ni matendo ya akili, Hivyo Daudi
alikuwa ni mtu  aliyeupendeza moyo wa Mungu  (1 Sam 13: 14),
inaonyesha kwamba Mungu ana moyo, unaoweza kunakiliwa kwa
kiwango kidogo na mtu, ingawa mwanadamu wa mwili
haupendezi moyo wa Mungu. Mafungu ya maneno kama  BWANA
akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu  duniani akahuzunika
moyo (Mwa. 6:6), hufunua hisia ya Mungu, mwenye ufahamu
kuliko kuwa kishindo cha roho  ya kuwazika katika hewa. Hapa
tunasaidiwa tukubali  jinsi  kwa kweli tunaweza pande zote mbili
kumpendeza na kutokumpendeza,  Kama mtoto anavyoweza  kwa
baba wa mwili.

18

IKIWA MUNGU SI MTU MMOJA
Kama  Mungu si wa kweli, mmoja mwenye kuwepo, Basi
wazo la kupenda  mambo ya roho ni vigumu  kushikana nayo.
ikiwa Mungu ni mwenye haki kabisa  lakini si mtu mwenye umbo,
basi kwa kweli hatuwezi kuiwazia  haki yake ilivyodhihirika kwa
watu. Pande zote mbili, Ukristo uliokenguka na wayahudi  wana
wazo la kwamba haki ya Mungu  inaingia katika maisha ya watu
kwa njia ya
‘Roho Mtakatifu’  Asiyedhahiri  ambaye kwa namna
isiyoeleweka tunafanywa  mfano kwenye akili ya  Mungu, na
kukubalika kwake. Kwa maneno mengine, mara tukitambua ya kwa
mba yupo  mtu mwenyewe aitwaye Mungu, basi tunaweza
kurekebisha tabia  yetu kufuata atakavyo, Kwa msaada wake
utokao  kwenye ushawishi wa neno lake  na kwa kuleta  sifa
inayoonyesha tabia ya  Mungu katika utu wetu.

Lengo la Mungu ni kujidhihirisha mwenyewe  katika mkutano
wa watu waliotukuzwa. Jina la kumbukumbu yake, YEHOVA
ELOI, linamaanisha hivi ( Atakaye kuwa kwa wenye nguvu ni
tafsiri  iliyo karibu sahihi.)  ikiwa Mungu si mtu mwenye umbo,
basi thawabu ya waaminifu  katika ufalme wa Mungu  ujao duniani
inaonyesha ya kwamba  watakuwa nayo wazi tena dhahiri
wakiwepo  katika mwili, Ingawa hawatakuwa katika udhaifu  wa
mwili wa Mwanadamu tena. Ayubu alitamani' Siku ya mwisho’
atakapofunguliwa na mwili wake ( Ayubu 19:25:27); Abrahamu
itabidi awe mmojawapo  wa wale wengi wa hao  walalao katika
mavumbi ya nchi ambao wataamka…… Kwa uzima wa Milele wa
nchi ya Kanani (Dan. 12:2) hivyo basi  ataweza kupata ahadi ya
urithi wa milele  wa nchi ya kanaani, Sehemu inayoonekana katika
dunia hii
(Mwa. 17:8.)  “ Na wataua wake watashangilia….. waimbe
kwa sauti  kuu  vitandani mwao….. ili  kufanya kisasi juu ya
   19

mataifa  (Zab 132: 16; 149: 5,7) Kushindwa kwa watu wote wa
pande mbili, Wayahudi na watu wa mataifa,

Kutambua mafungu ya maneno kama haya  vyema, kwa
ukubwa wa maneno  yenyewe Kuletwa ahadi za kuonekana kwa
Abrahamu, kumeongoza watu kwenye imani potovu la' Nafsi haifi’
ya kwamba Mwanadamu halisi anakuwepo  hai akifa. Wazo hili
halina msaada wa Biblia kabisa. Mungu  hapatikani na mauti, Mtu
mwenye utukufu, analifanya lengo lake, ili kwamba wanaume na
wanawake waweze kuitwa na kuishi katika ufalme wake  ujao
kwenye dunia hii, Kushiriki sifa, zilizoelezwa katika umbo la
mwili.

Waaminifu  wameahidi wa kwamba watarithi mwili wa
Mungu  (2 Pet. 1:4) Ikiwa Mungu si mtu mmoja, basi hii ina maana
tutaishi  milele kwa roho zisizo na mwili. Lakini hili si fundisho la
Biblia. Tutapewa mwili kama ule wa Yesu. (Flp. 3:21), Nasi
tunajua kwamba tutakuwa na  mwili halisi kwenye ufalme  mwili
utakaokuwa na mikono  macho na masikio  (Zek. 13:6, Isa. 11:3 ),
mafunzo ya Mungu  kuwa ni  Mmoja, kwa sababu  hii yanasimulia
Injili ya Ufalme.

Itakuwa  wazi kwamba  hakutaweza kuwa na wazo la kujua
Ibada,  dini au uhusiano  mmoja na Mungu  mpaka itambulike
kuwa Mungu  ni mtu mmoja, na kwamba kwa mwili sisi ni mfano
wake. Ingawa ni mfano usio kamili sana unahitajika kuukuza
kufuata  mfano wa akili yake, Hivyo basi, tutaweza kupata
utimilifu wa mfano wake unaoonekana katika ufalme wa Mungu.
Maana nyingi zaidi  na faraja tunaweza kupata kutoka  mafunzo ya
maneno ambayo yanamtaja Mungu kuwa ni Baba aliye na upendo,
akiturudi kama Baba afanyavyo kwa mwanae (mfano. Kum. 8:5).
Katika maneno yenyewe  ya mateso ya Kristo  tunasoma
20

kwamba,'Lakini BWANA aliriidhika kumchubua’  (Isa. 53:10
),Ingawa  “Alimlilia Mungu” aliisikia sauti yangu…….. Kilio
changu kikaingia masikioni mwake (Zab.18:6). Ahadi ya Mungu
kwa Daudi kuhusu mzao atakaye kuwa ni mwana wa Mungu
ilitakiwa azaliwe kwa Muujiza kwa Mwanadamu; Ikiwa Mungu
hakuwa ni mtu mmoja, asingekuwa na mwana huyo.

Kumfahamu Mungu kwa usahihi ni ufunguo unaofungua
maneno  mengi mengine ya muhimu katika mafundisho ya Biblia.
Lakini kama uongo mmoja  huongoza kwenye uongo mwingine,
Hivyo dhana potovu juu ya mungu inaficha utaratibu  wa kweli
ambao maandiko yanatoa. Kama umepata kuona  kuwa hii sehemu
inadhibitisha, au hata ikiwa ni ndogo, basi, swali linakuja. Je?
Unamjua Mungu kweli?. Sasa  tutachunguza maandiko ya Biblia
zaidi kuhusu  yeye.

1.3 Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake

Ikiwa Mungu yupo, inafaa kufikiri kuwa atakuwa  amevumbua
njia nyingine ya kutuambia habari zinazo mhusu yeye mwenyewe.
Tunaamini ya kwamba Biblia ni ufunuo wa Mungu kumjulisha
Mwanadamu,  na humo ndani ya kitabu tunaona kudhihirika tabia
ya sifa ya Mungu. Hii ndio sababu Neno la Mungu linasemwa
kuwa ni'Mbegu’ yake (1 Petro 1:23) Kwa kuwa kama likigeuza hali
ya mioyo yetu, kiumbe mpya anaumbwa ndani yetu ambaye ana
sifa za Mungu  (Yakobo. 1:18,  2Kor. 5:17). Kwa hiyo sisi
wenyewe tunapotumia  zaidi neno la Mungu na kuchukua masomo
sisi wenyewe, ndivyo zaidi tutafanana  mfano wa mwana wake (
Rum, 8:29) ambaye kwa tabia ya sifa alikuwa mfano kamili  wa
Mungu (Kol. 1:15).Kwa hii imelala thamani ya kusoma sehemu  za
historia ya Biblia, Zimejaa kadhia ya  masomo jinsi Mungu
   21

alivyojishughulisha na watu pamoja na matifa, Daima  akionyesha
msingi ule ule wa sifa.

Katika Kiebrania jina la mtu mara nyingi  lilileta tabia ya sifa
zao  au  taarifa zinazowahusu. Mifano mingine iliyowazi:

• ‘Yesu’'Mwokozi’  Kwa kuwa atawaokoa watu wake kutoka
dhambi zao’ (Math. 1:21)
• ‘Abrahamu’'Baba wa mkutano mkubwa’  Maana
nimekufanya kuwa baba wa mataifa mengi’(Mwa. 17:5)
• ‘Hawa (Eva)'Uhai’ Kwa kuwa alikuwa mama wa wenye
uhai wote (Mwa. 3:20)
• ‘Simeoni’'Kusikia’ Kwa kuwa bwana amesikia kwamba
nalichukiwa, kwa sababu amenipa mwana  huyu (Mwa. 29: 33).
Katika Yeremia 48:17, kuwajua watu wa Moabu ni sawa sawa
na kufahamu jina la moabu.Mara nyingi zaburi  zinamlinganisha
Mungu mwenyewe na jina lake, neno lake na matendo (Zab. 103:1,
105:1, 106:1,2,12,13.) Kwa sababu hii itegemewe kwamba majina
ya Mungu  na heshima vitatupatia  habari nyingi kuhusu yeye
mwenyewe, kwa kuwa  yapo maelekeo mengi  ya tabia ya sifa  na
kusudi  kwa kweli  ana jina zaidi ya moja.Somo lenye kueleza
jambo moja moja  la jina Mungu  linafaa baada ya Ubatizo;
kufahamu zaidi sifa na tabia ya Mungu  kumeelezwa katika jina
lake, ni jambo lingine ambalo  liendelee wakati wa maisha yetu
yote katika Bwana. Linalofuata sana kwa hilo, mengi ni Utangulizi.

Musa alipotaka aelimishwe kwa undani  kuhusu  Mungu ili
imani yake  iimalike wakati wa kipindi kisicho sahaulika sana  cha
maisha yake. Malaika,'Alitangaza
jina
la BWANA:
BWANA,BWANA Mungu, Mwingi wa huruma, Mwenye fadhili,
Si mwepesi wa hasira, Mwingi wa rehema na kweli, Mwenye
kuwaonea huruma watu elfu elfu, Mwenye kusamehe uovu na
22

makosa na dhambi; Wala si mwenye kumhesabia mtu  mwovu
kuwa hana hatia,’ (Kut. 34:5-7)

Huu ni ushahidi ulio  wazi wa kwamba  majina ya Mungu
yanaweka sifa zake.Tendo la kuwa nazo ni uhakika  kuwa ni mtu
mmoja, si busara  kufikiri ya kwamba  fungu la roho laweza kuwa
na dalili na sifa ya tabia  hizi  ambazo vile vile  zaweza
kuendelezwa  ndani yetu wanadamu.

Mungu amechagua hasa jina moja  ambalo amependa ajulikane
na kukumbukwa na watu wake, ni kwa  ufupi, maelezo mafupi, ya
kusudi lake kwa watu.

Israeli walikuwa watumwa Misri, Walihitajika kukumbushwa
lengo  la Mungu kwao. Musa aliambiwa awaambie  Jina la Mungu,
ili kwamba  hili liwasaidie  kuwaletea kusudi la kuondoka Misri na
kuanza safari kuelekea nchi ya Ahadi (1Kor. 10:1) Nasi pia
tunahitajika  kuelewa mambo ya msingi yahusuyo jina la Mungu
kabla ya kubatizwa na kuanza  safari yetu ya kuelekea Ufalme wa
Mungu. Mungu aliwaambia  Israeli  kuwa Jina lake alikuwa
YAHWEH-YAHU (Zab 89:8 uv); Maana yake“Mimi niko ambaye
NIKO” au limetafsiriwa kwa usahihi zaidi,'Nitakuwa ambaye
Nitakuwa’(Kut 3:13-15) Jina hili, kidogo likapanuka wakati ule:”
Tena  Mungu akamwambia  ( Ikiwa ni nyongeza) Musa, Hivi
ndivyo utawaambia wana wa Israel, BWANA (Yahweh) Mungu
wa Babu zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa
Yakobo, ….Hili ni Jina  langu Milele, la kumbukumbu yangu kwa
vizazi vyote. (Kut. 3:15). Kwa sababu hiyo jina kamili la Mungu ni
“BWANA Mungu”
Zaidi Agano la kale liliandikwa kwa Kiebrania  na tafsiri ya
Kiswahili ni lazima kutukia visivyo sawa sawa  wakati ujapo wa
kutafsiri maneno ya Kiebrania  hasa neno “Mungu”  mengi ya
   23

maelezo moja moja  yakosekana  - Tafsiri yetu ya Kiswahili
imetoka kwenye  Kiingereza. Moja ya maneno yanayotumiwa  na
Kiebrania  limetafsiriwa'Mungu’ ni Elohim (ELOI) maana
yake'Wenye Nguvu’ Kumbukumbu ya jina la Mungu, jina ambalo
anatutaka  tumkumbuke, kwa sababu hiyo.

YAHWEH  ELOHIM  -  YAHU  ELOI
 Maana yake
ATAKAYEDHIHIRIKA KATIKA KUNDI LA WENYE
NGUVU.

Kwa hiyo ni kusudi la Mungu kuidhihirisha tabia ya sifa yake,
Umuhimu wake katika kundi kubwa  la watu. Kwa kulitii neno lake
tunaweza  kukuza sifa zingine za Mungu  ndani yetu wenyewe
sasa, hivyo basi kadri ya busara  sana. Mungu alijifunua
mwenyewe  kwa waamini wa kweli katika maisha haya.lakini jina
lake Mungu ni la Unabii wa wakati ujao  hapo dunia itakapo jaa
watu  watakao kuwa sawa naye, pande mbili kwa tabia na mwili
(2Petr 1:4). Ikiwa tunataka kuungana na lengo la shabaha  ya
Mungu na kuwa kama Mungu bila hata kufa tena, kuishi milele
katika uadilifu  wote uliokamilika, basi yatupasa  sisi wenyewe
tujiunge na jina lake.

Namna ya kufanya hivi ni kubatizwa katika jina, yaani la
Yahweh Elohim (Math. 28:19). Hili linatufanya tuwe watoto
(‘Uzao’) wa Abrahamu (Gal,. 3:27-29) uliohaidiwa kurithi milele
nchi (Mwa. 17:8; Rum. 4:13) Kundi la wenye nguvu  (Elohim Eloi)

ambao unabii wa jina la Mungu  utatimilika. Limeelezwa
zaidi kwa habari katika  somo la  3.4. 
24

1.4  Malaika
Yote ambayo  tumeyapima sana katika somo hili yanaletwa
pamoja kwenye tafakari ya Malaika:

• Viumbe walio na mwili
• Huchukua jina la Mungu
• Wao ni njia ambayo roho wa Mungu  anatenda kazi ya
kutimiza mapenzi yake
• Wanapatana tabia na kusudi lake
• Na kwa hiyo wanamdhihirisha yeye.

Tumetaja kwenye somo la 1.3  ya kwamba moja kati ya
maneno  yanayotumika zaidi katika  Kiebrania lililotafsiriwa
“Mungu” ni' Eloi’ ambalo hasa maana yake ' Wenye nguvu’
hawa,'Wenye nguvu’  ambao huchukua jina la Mungu
wanapotokea wana weza  kuitwa 'Mungu’  kwakushirikiana kwao
pamoja na naye karibu. Hawa viumbe wanaitwa Malaika.

Taarifa ya uumbaji wa ulimwengu katika mwanzo  1
inatuambia ya kwamba Mungu  alitamka amri halisi kuhusu
Uumbaji'Ikiwa hivyo’ walikuwa ni Malaika waliotimiza amri hizo:

“Enyi Malaika zake, mliohodari mtendao neno lake,
mkiisikiliza sauti ya neno lake (Zab. 103:20).

Kwa sababu hii  busara husadiki kuwa tunaposoma 'Mungu’
akiumba ulimwengu, kazi hii kweli ilifanywa na Malaika. (Ayubu
38:4-7) anadokeza vile vile namna hii. Sasa ni wakati mzuri
kuelezea kwa kifupi  matukio ya uumbaji kama yalivyoandikwa
Mwanzo 1:

   25

Siku ya Kwanza‘   Mungu  akasema, Na iwe nuru, Ikawa’
(Mstari  3)

Siku ya Pili
'Mungu  akasema, Na iwe anga katikati ya
maji, likayatenga  maji na maji.Mungu akalifanya anga ,akayatenga
yale maji   yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga: Ikawa
hivyo’  (Mstari 6,7)

Siku ya Tatu ‘Mungu  akasema, Maji yaliyo chini ya
mbingu na yakusanyike  mahali pamoja, (akifanya Bahari na
Bahari kuu)  ili pakavu paonekane; Ikawa hivyo’ (Mstari wa 9)

Siku ya Nne   ‘Mungu akasema, Na iwe  mianga katika
anga la mbingu… Ikawa hivyo’ (Mstari 14:15)

Siku ya Tano ‘Mungu akasema,  Maji na yajae kwawingi
na kitu kiendacho chenye uhai …. ndege waruke juu ya nchi …..
Mungu akaumba kila kiumbe  chenye uhai (Mstari wa 20:21),
Ikawa hivyo.

Siku ya Sita ‘Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe
haikwa jinsi  zake…. Mnyama wa kufugwa,nacho kitaambaacho
…. Ikawa hivyo (Mstari 24)

Siku hiyo hiyo ya sita mtu aliumbwa. Mungu akasema, na
tufanye  mtu  kwa mfano wetu, na kwa sura yetu  (Mwa 1:26).
Tuliwahi kutoa maelezo  juu ya mstari  huu katika somo la 1.2.
Kwa muda uliopo, tunataka kujua hapa ya kwamba.'Mungu’ sio tu
anatajwa Mungumwenyewe katika utu'Na tufanye mtu’ inaonyesha
kuwa Mungu anatajwa  mtu zaidi ya mmojaNeno  la Kiebrania
linalotafsiriwa hapa'Mungu’ ni Elohim (Eloi), Maana yake'Wenye
nguvu’ Ukiwa ni ushahidi unaotaja Malaika. Ukweli ni kwamba
26

Malaika  walituumba sisi kwa mfano wao  maana yake ni kuwa
wana sura ya mwili ule ule kama tulio nao. Kwa sababu hiyo ni wa
kweli, wa kugusika, viumbe wenye mwili, wakishiriki mwili ule
ule kama wa Mungu.

‘Mwili’ Kwa maana  hii unatajwa kwa msingi jinsi mtu
mwingine alivyo kwa sababu ya muundo wa mwili wao. Katika
Biblia ipo “Miili” ya  aina mbili  katika  maana halisi ya neno
haiwezekani kwa wakati huo huo kuwa miili hii ya aina mbili.


 Mwili wa Mungu (‘Mwili wa Uungu’)
 Hauwezi kutenda dhambi (Mkamilifu)  Rum 9:14,6:23;
Zab. 90:2, Math 5:48,Yak 1:13)Haupatikani na Mauti ( 1Timotheo
6:16)
 Una nguvu tele na uweza ( Isaya 40:28)

Huu  ndio mwili wa Mungu na Malaika na ambao alipewa
Yesu  baada ya kufufuliwa (Matendo 13:34; Ufunuo  1:18; Ebr.
1:3) Huu ndio mwili  ambao  tumeahaidiwa kupewa  (Luka
20:35,36; Isa. 40:28,31)

 Mwili wa mwanadamu
Hujaribiwa na kutenda dhambi ( Yak 1:13-15 )kwa nia mbaya
ya asili (Yer 17:9; Marko 7:21-23) Huangamia mautini, Yaani
unapatwa na kifo ( Rum. 5:12,17; 1Kor  15:22)  Una kikomo cha
nguvu, sehemu mbili,  kwa mwili (Isa. 40:30) na kwa akili ( Yer
10:23)

Huu ni mwili ambao watu wote, wema na wabaya, kwa sasa
wanao mwisho  wa mwili huo ni kifo (Rum 6:23). Ulikuwa ni
mwili ambao  Yesu alikuwa nao  wakati wa maisha yake  ya  mwili
   27

unaokufa  hapa duniani (Ebr. 2:14-18,Rum. 8:3 Yoh 2:25, Marko
10:18)

MATENDO YA KUONEKANA  NA  MALAIKA
Malaika wakiwa na mwili wa Uungu, inabidi wawe hawana
dhambi na kwa sababu hiyo hawawezi kufa  kwa kuona kwamba
dhambi  huleta mauti (Rum. 6:23). Inapasa wawe na umbo halisi na
mwili wa kuwepo mauti  “Na yaletwe basi maji kidogo  ukanawe
miguu, mkapumzike chini ya mti huu”(Mwanzo 18:4)

Wawili kati ya hao Malaika wakati ule  walikwenda kwa lutu
katika mji wa Sodoma. Tena, walitambuliwa kuwa ni watu  na lutu
pamoja na watu wa  Sodoma.'Basi,  wale malaika Wawili wakaja
Sodomaa jioni aliowakaribisha wakae kwake usiku. Lakini watu
wa Sodoma wakaja kwenye nyumba yake, wakiuliza kwa namna ya
kutisha,'Wawapi wale watu waliokuja  kwako usiku huu ?’ Lutu
akawasihi,' Watu hawa msiwatende neno’  Taarifa ya maandiko ya
Mungu  pia inawaita ni'Watu’, Wale watu ( Malaika )
wakanyoosha mikono yao, wakamwokoa Lutu,  Basi wale  watu
wakamwambia Lutu … BWANA ametutuma tuuharibu  Sodoma
(Mwanzo 19: 1,5,8,10,12,13).

Ufafanuzi wa  Agano jipya  juu ya matukio haya
yanadhibitisha kwamba Malaika wanafanana na umbile la watu.
“Msisahau kuwafadhili wageni; Maana kwa njia hii wengine (Kwa
mfano Lutu na Abrahamu ) waliwakaribisha Malaika pasipo kujua
(Ebr 13:2)

Yakobo alishindana usiku kucha na mtu mmoja ( Mwa 32:24)
ambaye baadae tumeambiwa kuwa  alikuwa Malaika (Hosea 12:4)

28

Watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe
walikuwepo kwenye  ufufuo (Luka 24:4) na wakati wa kupaa (Mat.
1:10) Yesu, kwa  uhakika hawa walikuwa ni Malaika. Ona
vidokezo vya'Kipimo cha Kibinadamu, maana yake cha Malaika’
(Uf 21:17).

MALAIKA   HAWATENDI    DHAMBI
Malaika wakiwa na mwili wa Uungu, hawawezi  kufa, kwa
sababu dhambi huleta mauti, Basi wao hawawezi  kutenda dhambi.
Maneno ya asili katika lugha ya Kiyunani na Kiebrania
yaliyotafsiriwa'Malaika’  maana yake ni mjumbe;  Malaika ni
wajumbe au watumishi wa Mungu, Watiifu kwake, Kwa hiyo
hawafikiriwi wao kuwa ni wenye dhambi. Kwa hivyo neno la
Kiyunani’Agelos’
lililotafsiriwa'Malaika’

vile vile
limetafsiriwa'Wajumbe’ Wanaposemwa wanadamu kwa mfano
Yohana mbatizaji, (Math 11:10) na  wajumbe wake (Luk. 7:25)
wajumbe wa Yesu (Luk. 9:52) na watu walioupeleleza mji wa
Yeriko (Yak. 2:25). Kwa kweli  inawezekana kwamba'Malaika’
katika maana ya wajumbe  wanadamu wanaweza kutenda dhambi.

Mafungu ya maneno yafuatayo ni wazi kwamba  Malaika wote
( Sio tu baadhi yao) kwa umbile ni watiifu kwa Mungu, na hivyo
hawawezi kutenda dhambi.

‘BWANA  ameweka kiti chake cha Enzi mbinguni Na Ufalme
wake unavitawala vitu  vyote (Yaani  haiwezekani kuwepo uasi juu
ya Mungu mbinguni)Mhimidini BWANA, Enyi  Malaika zake,
Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkisikiliza sauti ya  neno
lake Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake Yote;  Ninyi
watumishi wake  mfanyao mapenzi yake (Zab. 103:19-21)

   29

“Msifuni, enyi Malaika wake wote …. Majeshi yake yote (
Zab 148: 2 )  Je ! hao wote si roho (Malaika ) watumikao,
wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu ? ( Ebra. 1:
13,14 )

Kurudiwa kwa neno'Wote’ linaonyesha ya kwamba Malaika
hawajagawanyika katika makundi mawili, kundi moja zuri na
jingine lenye dhambi. umuhimu wa kufahamu vema  umbile la
malaika ni kwamba  thawabu ya waaminifu ni kushiriki mwili wao.
“Wale  wahesabiwao kuwa wamestahili…. Hawaoi  wala
hawaolewi … wala hawawezi kufa tena. kwa sababu huwa sawa
sawa na Malaika (Luk 20:35, 36).

Hili ni neno la muhimu  kulishika. Malaika hawawezi
kufa'Maana hatwai asili ya Malaika (Kwa kuwa tangu asili
hawajatenda dhambi). Ila atwaa asili ya mzao wa Abrahamu ,sababu

ya dhambi’ (Ebr 2:16) Ikiwa Malaika waweza kufanya
dhambi, Basi wale ambao  watakuwa wamestahili thawabu  ya
Kristo atakapo kuja bado  wataweza kutenda dhambi pia, Na kwa
kuwa dhambi huleta mauti  (Rum 6:23)  kwa sababu hiyo
hawataweza kuwa na uzima wa milele, kama tukiwa na uwezekano
wa kutenda dhambi  ni kufanya ahadi ya Mungu  ya uzima wa
milele  haina maana, kwa kufahamu kuwa thawabu yetu ni
kushiriki  mwili ule wa Malaika.  Ushuhuda wa'Malaika (Luk.
20:35,36) unaonyesha kwamba hakuna aina ya Malaika wema na
wenye dhambi; ipo aina moja ya Malaika tu.

Ikiwa  Malaika waweza kutenda dhambi, Basi Mungu
ameachwa  hana  nguvu  za kutenda  tendo la haki  katika maisha
yetu  na mambo ya ulimwengu, kwa kufahamu kuwa ameeleza
kwamba anafanya matendo yake kwa njia ya Malaika zake( Zab
103:19-21) Wamefanywa kwa'Roho wa Mungu  katika  maana  ya
30

kwamba anatimiza  yote kwa nguvu zake. Akitenda kazi katika
Malaika  (Zab 104:4). Kwamba wanamwasi Mungu  haiwezekani.
Mkristo amwombe  kila siku, Mungu ili ufalme  uje duniani, ili
mapenzi yake yafanyike  kama sasa yanavyofanyika mbinguni
(Math 6:10) Ikiwa Malaika wa Mungu iliwapasa washindane na
Malaika wenye dhambi  huko mbinguni, basi,  kwa utimilifu
mapenzi yake  hayakuweza kufanyika huko,  na kwa sababu hiyo
hali hiyo hiyo itapatikana kwenye ufalme wa Mungu  ujao.
Kutumia maisha ya milele kwenye ulimwengu  ambao utakuwa ni
uwanja wa vita  kati ya dhambi na utii, kwa shida hayo sio
matazamio  ya kutia moyo, lakini hilo, kwa kweli, sio ndiyo suala
lenyewe.

MALAIKA  NA  WATU  WANAOAMINI
Ipo sababu nzuri ya kuamini kuwa kila mwamini wa kweli ana
Malaika pengine mmoja maalumu-wa kuwasaidia katika maisha
yao:-

 ‘Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia na
kuwaokoa  wamchao’  (Zab 34:7)
Mmojawapo wa wadogo hawa  waniaminio  (Yaani wafuasi
dhaifu- Zek, 13:7  Mat 26:31)…Malaika wao mbinguni siku zote
huutazama uso wa  Baba yangu’ (Mat.
18:6,10)
 Wakristo wa kwanza ni wazi waliamini kwamba Petro
alikuwa na  Malaika mlinzi  (Matendo 12:14,15).
Watu  wa Israeli  walipita katika bahari ya Shamu,
waliongozwa na malaika  kwenye jangwa  kuelekea nchi ya Ahadi.
Kutembea kupitia katika bahari ya shamu maana yake ni Ubatizo
wetu katika maji  (1Kor 10:1), Hivyo nasi  vile vile  ina maana
tusadiki  kuwa baadae tunaongozwa  na kusaidiwa na Malaika
   31

tunaposafiri katika jangwa la maisha  kuel;ekea nchi ya ufalme wa
Mungu.
Ikiwa  Malaika wana weza kuwa waovu  katika maana ya
kuwa wenye dhambi, basi Ahadi hizi za Malaika kuongoza  na
kushawishi katika maisha  yetu zinakuwa laana badala ya Baraka.

• Basi tufahamu ya kuwa Malaika ni Viumbe………
• Wenye  mwili ulio sawa na Mungu na huonekana kwa mwili
• Ambao  hawawezi kutenda dhambi
• Daima hufuata amri za Mungu
• Wao ni njia ambayo Mungu katika Roho  nguvu hunena na
• kutenda kazi (Zab. 104:4)

 LAKINI..?
Makanisa mengi ya'Kikiristo’ yana wazo la kwamba  Malaika
wanaweza kutenda dhambi, na kwamba Malaika wenye dhambi
sasa hivi wapo na  wao  wanahusika na dhambi pamoja na matatizo
yaliyopo hapa Duniani. Tutajadili zaidi vya kutosha juu ya
kutofahamu vema jambo hili  kwenye somo la  6. Kwa sasa
tutatengeneza vipengele vifuatavyo:-

Inawezekana kwamba uumbaji ulikuwepo  uliotutangulia sisi
wa kweli,  yaani huo ulioandikwa katika  Mwanzo 1. Pia inaweza
kusadikika ya kwamba  Malaika waliopo walikuja kuwa na
fahamu  za'Wema na Ubaya’ (Mwa. 3:5) walipo kuwa katika hali
kama hii  tuliyonayo katika maisha haya.

Ya kwamba  viumbe wengine walioishi kwa kipindi kile
walitenda dhambi hatujakatazwa kufikiri;  lakini yote haya ni
mawazo  ambayo mioyo ya watu  hupenda kujishughulisha. Biblia
yatuambia kile ambacho tunakihitaji  kujua kuhusiana na hali
iliyopo,  ambayo ni kwamba hawapo Malaika  watenda dhambi,
Malaika wote ni watiifu kwa Mungu kabisa.
32

Hawawezi kuwepo viumbe wenye dhambi mbinguni, kwa
kufahamu kuwa Mungu'ana macho safi na hawezi  kuangalia
uovu’ (Ab. 1:3) katika maelezo haya,  Zaburi 5:4,5  yatuambia:-

‘Mtu mwovu  hatakaa kwako.  wajivunao hawatasimama
mbele za macho yako’ yaani makao ya mbinguni. Jambo la
kwamba ulikuwepo  Uasi juu ya Mungu mbinguni na Malaika
watenda dhambi  ni wazo linalopingana kabisa  na maneno
yaliyotolewa.
       
 Neno
la kiyunani
lililotafsiriwa'Malaika’ maana
yake'Mjumbe’
linataja
wanadamu,
kama
tulivyoonyeshwa'Wajumbe’  wanadamu hawa wanaweza  kwa
kweli kufanya dhambi.

Ya kwamba upo uovu, viumbe wenye dhambi ambao juu yao
mwelekeo wa maisha yote yasiyofaa  wanaweza kutupiwa lawama
kwa kawaida ni moja ya  Imani zaidi iliyoshikiliwa  katika
Upagani.Kwa njia hiyo hiyo mambo yanayohusu Krismas
yameingia kwenye  kile kinachodhaniwa ni'Ukristo’ Basi, vile vile
Ukristo una fikra hizo za Kipagani

Yapo mafungu ya maneno  ya Bibilia yaliyojaa tele ambayo
yanaweza kutoeleweka kusaidia wazo hili la Malaika wenye
dhambi kwa sasa wapo. Haya yamepimwa katika 'Kumsaka
Shetani’  yanapatikana kwa  wachapishaji - Mafungu haya ya
maneno  hayawezi kuruhusiwa kupingana na mafunzo tele ya
Biblia  kwa kutofautiana na haya yaliyokwisha tolewa.


   33

Tumeacha  Kitambo sehemu ya 1:'Mungu ni roho’
(Yohana 4:24)

Katika somo la pili  tunafafanua  kwa  utaratibu zaidi  jinsi
Roho wa Mungu  alivyo. Tunaweza kutoa maelezo kwa ufupi
sababu zilizoonyeshwa  hapo kwa kusema kwamba  roho wa /ya
Mungu ni nguvu au pumzi yake ambayo kwa hiyo nafsi yake
mwenyewe,  Utu wake na tabia,  vimedhihirika kwa mwanadamu
kwa njia ya matendo yake ambavyo Roho huyo
anatimiza.Hivyo'Mungu ni Roho’ kama katika Yohana 4:24
atafsiriwe vema kwa kuwa Roho yake  ndiyo inafanya utu wake.

Mungu amesemwa kuwa yumo katika vitu vingi, kwa mfano:-

 ‘Mungu wetu ni moto ulao’   (Ebr. 12:29)
 ‘Mungu ni Nuru’

   (1 Yoh. 1:5)
 ‘Mungu ni Pendo

   (1 Yoh.4:8)
 ‘Neno (Kiyunani'Lagos’ - Mpango, Lengo,Kusudi, wazo)
  alikuwa Mungu’  (Yoh 1:1)

Hivyo,'Mungu’ ni sifa yake.  Ni kosa lililo wazi kuleta  sababu
za kupinga kwamba  sifa za upendo wa Mungu ni za kuwazika,
kwa kuwa tunasoma  kwamba 'Mungu ni pendo’  tunaweza
kumwita mtu mwingine  Mwema  wenyewe; lakini hii haina maana
kwamba  haupo bila mwili ni namna ya kuwepo yeye ndiko
kunatudhihirishia wema kwetu.

Roho ikiwa ni nguvu ya Mungu, mara nyingi tunasoma Mungu
akiituma au akiiongoza roho yake  kutimiliza mabo yake kwa
kupatana na mapenzi yake  na tabia ya sifa yake. Hata ameelezewa
kuwa anaumba roho  (Yaani Upepo UV). Kusema kwamba  Mungu
34

na roho yake katika maana safi iliyo halisi ni msemo ule ule kwa
namna nyingine - katika maana inakuwa  Uwepo wa Mungu.

Mifano ya  Mungu  akiiongoza Roho yake ni mingi,
inaonyesha mtengano wa Mungu na Roho yake:-

 ‘Yeye (Mungu)  aliyetia kati yao Roho yake mtakatifu’(Is. 63:11)
 ‘Nitatia Roho yangu  (Mungu)  juu yake  (Yesu )’ ( Math.12:18)
 ‘Baba huwapa  Roho mtakatifu’     (Luk. 11:13)
 ‘Roho akishuka kama  hua  toka Mbinguni’ (Yoh. 1:32)
 ‘Nitawamwagia watu wote Roho yangu’   (Matendo. 2:17).

Kwa kweli ushahidi  juu ya 'Roho wa Mungu’ ni uhakika wa
kutosha  kuwa Roho sio Mungu mwenyewe. Tofauti hizi kati ya
Mungu na Roho ni shida nyingine  ilio kwa wale wanao amini
kuwa Mungu ana  Nafsi'Tatu’ ambazo Mungu amelingana na Yesu
na Roho Mtakatifu. Jambo hili kama lingekuwa la  kweli, na kama
Mungu amedhaniwa kuwa sio mtu, basi halikadharika hata Yesu
naye sio mtu halisi.

Kwa umuhimu sana, Mungu asiye mtu hata sala  kuelekea
kwake inakuwa haina maana, kwenye alama  ambayo sala ni
mazungumuzo kati ya fahamu  zetu  na wazo la Mungu ambalo lipo
katika akili  zetu. Daima tunakumbushwa kwamba  tunamwomba
Mungu ambaye ana Umbo makao yake  yapo  Mbinguni (Mhu. 5:2;
Math. 6:9,5:16, 1Fal. 8:30) na kwamba Yesu sasa yuko  mkono wa
kuume huko ili kutoa maombi yetu mbele zake  (1Pet. 3:21, Ebr.
9:24).

Ikiwa Mungu si mtu binafsi, maneno haya yametolewa  bila
kuwa na maana. Bali, Mungu akieleweka kuwa ni wa kweli, Baba
mwenye upendo, Sala ya kumwomba inakuwa ya kweli, Jambo
   35

lililowazi na dhahiri - hasa  tukizungumza na mtu mwingine
ambaye tunamwamini ana mapenzi sana na anaweza kujibu.

Tumeacha  Kitambo sehemu ya 2:'Matumizi ya jina la
Mungu’

Tumefahamu kwamba Jina la Mungu na hilo la mwanae Yesu
yana maana  ya kina sana. Tunaposema 'Mungu’ tunagusa juu ya
kila mwelekeo  wa kusudi lake la Ajabu la upendo na kweli. Ya
kwamba Jina la Mungu  litumike bure kama upole  usio na maana
au kwa maelezo ya kukasirisha, ni moja ya mambo ambayo mtu
hufanya na kumnena  vibaya zaidi Muumba wake.  Kwa sababu hii
kila mtu anayetaka  kumpendeza Mungu na kumheshimu atafanya
kila jitihada  kutotumia vibaya Jina la Mungu  kirahisi- rahisi.
Katika jamii  ulimwenguni pote kufuru  hii  imekuwa sehemu ya
kawaida kwa Lugha za siku hizi;  Kukatisha ile iliyokuwa ni tabia
ya mazoea haita kuwa kazi rahisi. Sala ya kweli ya kuomba msaada
wa Mungu  hakika itasikika. Wale ambao  wapo ndani ya shughuli
yetu  ya kuwaongoza na kuwavuta,  Mf. Watoto,  pia
watakumbushwa
 hatari ya kukufuru:”Maana BWANA
hatamhesabia kuwa hana hatia alitajaye jina lake bure (Kum. 5:11)

Kwa upande mwingine  wapo wale wanaosisitiza kwamba
tusipotumia maneno ya Kiebrania Yahweh  au Yehova (Njia tofauti
ya kutamka  neno lile lile) Tunapozungumuza kuhusu Mungu,
wakati huo tunakuwa tumepotea sana. Miongoni mwao zaidi ya
hawa ni  Chama cha mlinzi, wanasisitiza kuwa  Mkristo asipojiita
mwenyewe ni'Shahidi wa  Yehova’  Basi hana uhusiano na Mungu.

Kwa kufanya hivi, watu hawa  wanatumia jina  takatifu  la
Mungu na  la ajabu kuchochea aina fulani ya mfumo wa Imani wa
36

kuelimisha kiroho, ambapo wanawadharau  watu wengine tu kwa
matamshi au matumizi ya neno moja. Hii sio kusema kuwa ni
vibaya  kutumia Jina la Mungu; Hasa kweli linafaa kutumika
kwenye Sala zetu wenyewe mara tukibatizwa kwa usahihi katika
Jina lake. Ingawa hivyo, Agano Jipya  halitupatii ishara yoyote
kuwa  hili ni lazima au  inatakiwa na Mungu. Aliongoza kuandika
Agano Jipya hivyo basi liliandikwa kwa Kiyunani (Kigriki)
likitumika neno moja la'Mungu’ -‘theos’  likiwa na maana  “Mtu
mkubwa”.

Hakuna tofauti  iliyofanywa  ndani yake  kati ya'Mungu’ na
'Yahweh’ wala haipo amri yoyote dhahiri  inayohusiana kwa
waamini wakiwa ni jumuiya wajiiteje.Petro anamsema mwamini
kuwa ni “ Mkristo” kuliko kumwita ni'Mtu wa Yehova’  au jambo
lingine kama hili (1 Petro 4:16)  kutilia mkazo zaidi  katika
matumizi ya Jina la 'Yehova’  kunapelekea kupunguza thamani ya
kazi  na  Nafsi ya BWANA'Yesu’  kwa njia hii ambayo  wakristo
wengi wa kiinjili wanatia msukumo zaidi kwenye jina  na kazi ya
Yesu huku wakiacha kuangalia  nafsi ya nguvu zaidi iliyo ya
Mungu.

Majina  mengine ambayo jumuia  ya waaminiao ya wakristo
wa kwanza  waliyojiita wenyewe,  hayatii ndani jina la Yehova:-
 
‘Jamii ya Israeli’ (Ef. 2:12)
‘Mkutano mkuu  na kanisa la wazaliwa wa kwanza’ (Ebr. 12:23)
‘Kanisa lake Mungu’ (Matendo 20:28)
‘Kanisa la Mungu aliye hai, Nguzo na Msingi  wa kweli’ (1
Timotheo 3:15)
‘Nyumba  ya Mungu’ ( 1 Timotheo 3:15)

   37

Tunapopita, ujue kuwa waamini
 hawakujiita
wenyewe'Wakristo’. Neno hili maana yake  lilikuwa la kuvunja
heshima, hawa watu wa Kristo walibezwa na maadui zao.

Tumeacha  Kitambo sehemu ya 3: 'Ufunuo wa Mungu’

Kinachufuata sio rahisi  kukishika chote wakati  tunaposoma
kwanza,lakini umuhimu wa jambo  tunalolizungumzia litakuwa
dhahiri kadri masomo yake yanavyosonga mbele. Tunajumuisha
kwenye maana hii ili  uliache somo hili lote  Msingi wa Biblia
ukisha pimwa wenye ufunuo kuhusu Mungu mwenyewe.

Jina la Mungu laweza kuchukuliwa na yeyote  ambaye
amemchagua kujifunua  au kujidhihirisha yeye mwenyewe. Hivyo
watu na Malaika  sawa sawa  na  Yesu huweza kuchukua jina la
Mungu. Hili ni jambo la muhimu ambalo  linatufunulia mengi ya
Biblia. Hata mwana anaweza kuchukua jina la Baba; ana mambo
mamoja na Baba yake,  anaweza kuwa na jina lile lile la kwanza-
lakini si mmoja na kuwa mtu yeye yule kama Baba.  Kwa njia hiyo
hiyo mwakilishi wa kundi  anaweza kusema kwa niaba ya kundi,
anaweza kumpigia mtu wa kwenye shughuli na kusema, Haloo !
hapa ni  wakulima, Si  Bw. Wakulima,  bali anachukua jina lao kwa
kuwa anafanya kazi kwa niaba yao. Basi hiyo hata kwa Yesu
ilikuwa hivyo.

MALAIKA HUCHUKUA JINA LA MUNGU
Tumeambiwa katika Kutoka 23:20,21 ya kwamba  Mungu
aliwaambia watu wa  Israeli kuwa Malaika atawatangulia mbele
yao;'Jina langu limo ndani yake’, waliambiwa. Jina lake Mungu
ni'Yahweh’. Basi,  Malaika huchukua jina la Yahweh,  na hivi
38

anaweza kuitwa Yahweh, au BWANA  kwa herufi kubwa neno
BWANA linatokana na Yahweh, katika Biblia UV ya Kiswahili ni
sehemu moja tu Zaburi  89:8 utakuta neno
YAHU = YAHWEH. Tumeambiwa  kuwa katika  kutoka
33:20 Mtu hataniona uso akaishi;  lakini katika Kutoka  33:11
tunasoma kwamba “BWANA”(Yahweh) alinena na Musa  uso kwa
uso, kama mtu anaposema na rafiki yake - Yaani  kirafiki. Hakuwa
ni BWANA, Yahweh  mwenyewe alikuwepo,  aliyenena na Musa
uso kwa uso,  Kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kumwona Mungu
yeye mwenyewe. Alikuwa ni Malaika  aliyechukua jina la Mungu
ndiye aliye fanya hivyo, na tunasoma  habari  za BWANA  akisema
uso kwa uso na Musa  wakati hasa ni Malaika aliyefanya hivyo
(Mdo. 7:30-33).

Ipo mifano mingine mingi ya maneno' Mungu' na BWANA
ikitaja  Malaika  wakiwa Mungu mwenyewe. Mfano mmoja ulio
wazi ni Mwa. 1: 26 “Mungu (Malaika) akisema, na tufanye mtu
kwa mfano wetu”

WATU  NA  JINA  LA  MUNGU
Moja ya maneno  ambayo yanayosaidia  sana katika kuelezea
yote haya  ni katika Yohana 10:34-36. Hapa Wayahudi walifanya
kosa  ambalo wengi wanaoitwa'Wakristo’ wanafanya leo.
Walidhani kuwa Yesu alikuwa anasema kuwa yeye ni Mungu
mwenyewe. Yesu alisahihisha kwa kusema “Haija andikwa katika
sheria yenu,  nimesema Ninyi ni Mungu ? Ikiwa aliwaita Miungu
….. inakuwaje mimi ….” Mnaniambia ninakufuru, kwa sababu
nalisema,  Mimi ni mwana wa Mungu  ? Yesu kwa kweli alikuwa
anasema 'Katika Agano la Kale watu waliitwa Miungu;  mimi
nasema ni mwana wa Mungu, basi imekuwaje mnaudhika  sana?
   39

Yesu kwa kweli alikuwa ananukuu toka  Zab 82 mahali ambapo
waamuzi wa Israeli  waliitwa'Miungu’.

Kama ilivyoonekana, Jina kamili la Mungu katika Kiebrania ni
'Yahweh Elohim’  likiwa na maana, Nitadhihirika katika kundi la
wenye nguvu. Waamini wa kweli ni wale wengi  wenye nguvu
katika maana ndogo ya maisha  haya  nao watakuwa na nguvu tele
kwenye Ufalme. Kwa mlinganisho huu wote umeonyeshwa kwa
Isa. 64:4 na 1 Kor.2:9.

“Watu  hawakusikia,  wala kufahamu kwa masikio, wala jicho
halikumwona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake
amngojaye” Paulo ananukuu mstari huu katika  1 Kor.2:9-10:
Imeandikwa, Jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia wala
hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu
amewaandalia wampendao. Lakini  Mungu ametufunulia sisi kwa
Roho. Fungu la maneno katika Isa. 64:4  linasema hakuna hata
mmoja isipokuwa  Mungu anaweza kufahamu mambo
aliyowaandalia waamini; Lakini 1Kor. 2:10 mstari unasema
kwamba  mambo hayo yamefunuliwa kwetu, hivyo katika maana
sisi ni  “Mungu”: sio Mungu mwenyewe katika utu, bali ufunuo wa
Mungu kwa matokeo kuwa tumebatizwa katika jina lake na kujua
Ukweli.

YESU  NA  JINA  LA  MUNGU
Sio jambo la kushangaza kwamba Yesu,  Ikiwa ni mwana wa
Mungu na ufunuo wake mkuu kwa watu, Pia naye atachukua jina la
Mungu. Aliweza kusema “Nimekuja katika jina la Baba yangu”
(Yoh.5:43). Kwa utii  wake, Yesu alipaa kwenda mbinguni, naye
Mungu akampa jina lipitalo majina - Jina la Yahweh, la Mungu
mwenyewe
40

(Fil. 2:9).basi hii ndiyo sababu tunasoma  Yesu anasema katika
Uf 3:12  “Nami nitaandika juu yake  (Mwamini) Jina la Mungu
wangu……na jina langu mwenyewe, lile jpya”Kumbuka Yesu
alitoa kitabu cha Ufunuo miaka mingi baada ya kupaa  kwenda
mbinguni na akiisha kupewa jina la Mungu,  kama ilivyoelezwa
katika  Wafilipi 2:9.

Hivyo anaweza kuliita jina la Mungu “Jina langu Jipya”; Jina
ambalo hivi karibuni alipewa. Sasa tunaweza kuelewa vema  Isaya
9:6,  mahali ambapo kuhusu yeye tumeambiwa “Jina  lake (Ujue
kuwa) utaitwa, Mshauri wa Ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba
wa milele, ….” Huu ni Unabii wa kwamba Yesu  atachukua majina
yote ya Mungu ya kwamba atakuwa ni ufunuo  wote wa Mungu
kwetu.Na ndivyo kwa maana hii aliitwa  “Emmanueli” maana yake
'Mungu  ni pamoja nasi’ ingawa yeye hakuwa Mungu.

Somo  La Kwanza :  Maswali

1.Ni nini  kitakachotusaidia zaidi  kuamini Mungu ?
a)  Kwenda  Kanisani
b)  Maombi na Kusoma  Biblia
c)  Kuzungumuza na  Wakristo
d)  Kutazama maumbile.

2.  Yapi ya haya yafuatayo ni ufafanuzi  sahihi  zaidi wa
Mungu ?
a)  Ni wazo tu katika mioyo yetu
b)  Kipande cha Roho katika Hewa
c)  Mungu Hayupo
d)  Mtu halisi wa Umbo

   41

3.  Je ? Mungu ni
a)  Ummoja
b)  Utatu
c)  Miungu wengi katika mmoja
d)   Haiwezekani kufafanua kwa njia ya  yoyote

4.  Jina la Mungu' Yahweh  Elohim’  lina maana gani ?
a)  Yeye atakaye  kuwa
b)  Atakayedhihirika katika kundi la wenye nguvu
c)  Mkuu
d)  Nguvu

5.  neno'Malaika lina maana gani ?
a)  Kama mtu
b)  Aliyefunikwa na Mabawa
c)   Mjumbe
d)   Msaidizi

6.  Je ?  Malaika  anaweza  kutenda Dhambi ?

7. Ni kitu gani  kinacho kudhihirishia kuwa Mungu  yupo ?
42

No comments:

Post a Comment