JIFUNZE JOGRAPHIA YA BIBLIA KAMA KIONGOZI
NA SENIOR PASTOR ERIC AND DERICDADY
Tujiandae vizuri kwa ajili ya kujifunza kozi hii, utakuwa na utajiri mkubwa wa ufahamu, juu ya kitabu cha ajabu kuliko vyote duniani Biblia.
SOMO LA KWANZA. Ulimwengu wa Agano la Kale.
I. Katika hali ya Kiroho Palestina au Kanaani ni Nchi ya Wakristo na Wayahudi vilevile.
A. Matukio ya KiBiblia kihistoria yalichukua nafasi huko katika ulimwengu wa
Agano la Kale.
1. Historia hiyo imeendelea kuwa changamoto kwa mwanadamu na ujumbe wa Mungu tuliopewa.
2. Mwanadamu ni kiumbe kinachohitaji Nafasi na Muda. Kwa hiyo
Jiographia na Historia lazima viongezwe.
PALESTINA MAHALI ILIPO, (ISRAELI)
II. Palestina (Kanaani) ipo pembezoni mwa Bahari ya Mediteranea pwani ya mashaariki
A. Kuna njia au barabara nyingi za kibiashara kuingia na kutoka Afrika na
Ulaya na Asia yote.
B. Wakati wote umuhimu wa Palestina umejitokea.
1. Katika Agano la Kale.
2. Katika Agano Jipya.
C. Imekuwa na majirani ambao ni waarabu na kumekuwa na ugomvi wa muda mrefu kati ya Taifa hili na Waarabu hivyo imekuwa n isababu ya hofu ya Kule mashariki ya kati nzima.
D. Mataifa ya sasa ya mashariki ya kati yanajitahidi kujenga Nchi hiyo tasa kuwa atakufikia Nchi ijaayo "Maziwa na asali".
III. Bahari Zinazopatikana Ulimwengu wa Agano la Kale.
A. Mediteranea: (Bahari kuu).
1. Kuna njia muhimu mno za baharini .
2. Ni mpaka wa Palestina kwa upande wa Magharibi, Yos.1:4.
3. Kuna bandari ya Joppa au Jaffa kwa sasa Tel Aviv. B. Ghuba la Uajemi.
1. Ipo mashariki mwa Peninsula ya Uarabuni.
2. Waandishi wengi wanasema Bahari hii ya Ghuba ya Persia imesababishwa na mito miwili Tigris na Frati.
3. Mji wa Uru. Ulikuwa maili 100 kutoka katika kichwa cha hii bahari hapo zamani.
C. Bahari ya Kaspiani.
1. Bahari kubwa kabisa ulimwenguni iliyozungukwa na Nchi kavu.
2. Maji yake ni ya chumvi.
IV. Bahari ya Shamu Au Bahari Nyekundu.
A. Maji mengi yaliyo katika ufa wa bonde Yordani. B. Ni mpaka kati ya Africa na Uarabuni.
C. Imezungukwa pande zote na Jangwa
V. Bahari Nyeusi.
A. Ni mpaka kati ya Ulaya na Asia.
B. Haionekani popote katika Agano la Kale.
VI. Bahari Ufi (Chumvi)
A. Bahari hii ni bahari ambayo maji yake yako chini sana. B. Pia imeitwa
1. Bahari ya Chumvi, Mwa. 14:3.
2. Bahari ya Araba, Kum. 3:17.
3. Bahari ya Mashariki, Yoeli 2:20.
Mito Muhimu ni Mitano.
I. Tigris
A. Jina lingine unaitwa Hidekeli, Mwa.2:14.
B. Unatokea kwenye miinuko ya Armenia katika Asia ndogo na kuishia katika
Bahari ya Ghuba la Persia.
C. Wakati wa zamani umuhimu wa miji ya Assyria ya Ashuru na Ninawi ilikuwa ukingoni mwa mto huu.
II. Frati
A. Chanzo chake ni mlima Taurus
III. Orente
A. Unaanzia Lebanon milimani unaishia Bahari ya Mediteranea.
IV. Mto Nili
A. Unaanzia Afrika mashariki katika ziwa Victoria au Nyanza mpaka Bahari ya
Mediteranea Misri.
B. Mto ulioleta ustaarabu wa Misri.
C. Wamisri waliufikiria mto huu kuwa Mungu.
V. Yordani
A. Ni mto mkubwa zaidi kule Palestina (Israeli)
B. Unaanzia katika mlima Hermon na kuishia Bahari mfu kwa kupitia Ziwa
Galilaya hapo ndipo inapopotelea kwa jumla.
C. Wakati mwingine ulijulikana kama mto wa Jangwani, Amo. 6:14; Yos. 12:2, Yoh. 3:23.
VI. Majina matano ya Nchi ya Israeli.
A. Palestina B. Kanaani C. Ahadi
D. Maziwa na Asali
E. Takatifu.
Milima Mikubwa.
I.. Ararati- 14,000 fts kileleni 17, 000 fts.
A. Mahali ambapo safina ya Nuhu ilipotua baada ya Gharika, Mwa. 8:4. B. Upo mashariki mwa Nchi ya Armenia kati ya Kaspiani na Bahari
Nyeusi.
C. Jina lingine kufuatana historia kuitwa Mlima wa Nuhu.
II. Zagros: 9000 FTS.
A. Ni safu za milima mashariki mwa mto Tigris unatokea kaskazini kuenda kusini
B. Zamani ulikuwa ni mpaka wa Ashuru na Umedi.
III. Taurus: 12,250 fts.
A. Jina lingine ni Fedha - madini inayopatikana. B. Kaskazini mwa mji wa Tarso.
IV. Lebanoni (Milima) - 10,200 ft. urefu.
A. Milima hii inafanywa na maendelezo ya Taurus.
V. Mlima Hermon - Kilele.
A. Maendelezo ya safu za milima ya Anti-Lebanoni uliyo upande wa pili wa miti
Lebanoni.
VI. Mlima Sinai.
A. Upo kusini katika Peninsula ya Sinai kati ya mfereji wa Suez na Ghuba la Agaba.
B. Hapa mdipo Musa alipopokea sheria kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kut.20 ff)
SOMO LA PILI
Utangulizi:
I. Tumekwisha elezea mambo huhimu katika ulimwengu wa Agano la Kale.
A. Miili mikubwa ya maji - Bahari. B. Mito.
C. Milima.
II. Sasa na tuendelee kuangalia Nchi Jinsi zilivyokuwa zinaonekana.
A. Hizi ni sehemu zinazoleta kumbukumbu tunapozisikia. B. Ni sehemu zilizoleta utaratibu kama tujuavyo.
1. Zilikuwa na watu maarufu.
2. Vilevile matukio makubwa yaliyotendeka huko.
3. Baadhi yake Mungu alizitumia kukamilisha kusudi lake la milele, Efe.
3:10 -11.
III. Tupo hapa sasa ni kwa sababu ya matukio yaliyochukua nafasi katika nchi hizo katika maelezo ya miaka mingi iliyopita.
IV. Utakapoendelea kukua na kuzifahamu nchi hizo basi utaongeza ufahamu mkubwa katika kujifunza Biblia
Mwilli:
I. Historia fupi juu ya Mataifa.
A. Historia inagawanyika asili yake kama ilivyo Sayansi.
1. Wengine walishikiria ustaraabu wa Mesopotamia sasa Irag.
2. Wengine walifiria ni Misri ya zamani.
3. Bado wengine kudai kuwa ustaarabu huu ni kutokea mashariki ya mbali kama ndiko asili ya mwanadamu.
II. Mpangilio wa Mataifa.
A. Yaliyotokana na wana watatu wa Nuhu, Mwa. 10.
1. Yapheti - Mataifa 7
2. Hamu - Mataifa 4, Mwa. 10:1.
3. Shemu - Mataifa 5
B. Yaphet: (mst. 2-5).
1. Gomeri - Indo-Ulaya.
2. Magogu - Scyilians (Kas./Mash. Bahari Kaspiani)
3. Madai - Umedi (Kusini ya Kaspian)
4. Yavani - Ugriki (Mwisho wa kusini Balkan Peninsula)
5. Tubali - Haifahamiki.
6. Mesheki - Haifahamiki.
7. Tirasi - Thracians (Kati ya Uyanani na Bahari Nyeusi pwani) C. Hamu: Ungua (mst. 6-14)
1. Kushi - Ethiopia.
2. Misri - (Mizraim) - Misri
3. Putu - Libya.
4. Kanaani - Palestina (Israeli - Uyahudi) D. Shemu: Jina (mst. 21-31)
1. Elamu - Waelamu (Kasi ya Uajemi na Mash. ya Bahari)
2. Ashuru - Assyria (Kusi Magh - Asia)
3. Arfaksadi - Ukalidayo (Tigrisi na Ufrati chini)
4. Ludi - Lyalia (Magh - Asia ndogo)
5. Aramu - Shemu (kati ya Ashuru na Kanani)
III. Nchi kubwa za Kibilia ni Tatu.
A. Armenia - Nchi ya zamani ambapo safina ilitua, 2 Fal. 19:37; Isa. 37:38.
B. Mede - Mungu aliwatumia watu hawa kutimiza maandiko juu ya maandishi ukutani 2 Fal. 17:6; 18 :11; Dan. 5:25-31; 6:28.
C. Ujemi - Ujemi na Umedi - ndizo zilizofuata kutawala dunia. Dan. 2:36-39; 7:5;
8:3; 11:2; Est. 1:3.
1. Nchi zilizowahi kutawala dunia yote kila moja kwa wakati mmoja. a. Misri.
b. Ashuru.
c. Alexander wa Makedonia, (Ulaya). d. Babeli.
e. Umedi na Uajemi. f. Rumi.
2. Dira ya mwelekeo wa dunia:
Kaskazini
Magharibi Mashariki
Kusini
D. Duniani kuna Mabara 7.
1. Afrika.
2. Marekani ya Kaskazini.
3. Marekani ya Kusini.
4. Asia.
5. Australia
6. Antartica
7. Ulaya.
E. Kuna bahari kubwa 4 Duniani.
1. Uhindi.
2. Arctic.
3. Pacific.
4. Atlantic.
F. Historia ya Agano la Kale inachukua mabara mawili tu kati ya Saba.
1. Afrika - Kaskazini Afrika (Kas. na Kas. Mash.)
2. Asia - Asia Ndogo.
G. Historia ya Agano Jipya iko katika mabara 3 kati ya saba.
1. Afrika - Afrika Kaskazini.
2. Asia - Asia Ndogo
3. Ulaya.
Nchi zilizokuwa wazi ni 5.
1. Sumer - Sehemu ya zamani ya Babeli, Mwa. 14:1; 11:31, Dan. 1:1
2. Ashuru - Kati ya Babeli, Armenia, na Umedi - Tigri Mto, Mwa. 2:14; 25:18
Yoh. 1:2.
3. Mesopotamia - sehemu ya wazi kati Tigris na Ufrati, Mwa. 24:7 -10
4. Elamu - Kaskazini ya Ghuba ya Uajemi, Mwa. 10:23.
5. Arabu - Peninsula kati ya Afrika na Asia, 1 Fal. 10 :15; 2 Nya.17:11, Ez. 27:21.
Nchi zilizo zunguka mashariki mwa Bahari ya Mediterania 6.
1. Asia ndogo - ilijumuisha falme:
a. Lidia.
b. Ashuru c. Hiti
2. Shemu mji mkuu ni Damaskus kwa Kiebrania - Aram.
Ilikuwa katika Ashuru na kanaani, 2 Sam. 8:6; 15:8; Ez. 17:16; Lk. 2:2; Mdo.
15:23, 41.
3. Kanaani - Mabaki ya chini ya meditranea pwani na Bonde la Yordani.
a. Mabaki ya wasio wayahudi wote, Mwa. 10:18 -20; Hes. 13:29; Josh.
11:3.
4. Phoeniki - Mstali mwemba Kaskazini mwa mlima Karmel walizungumza
Semitic lugha.
a. Miji yake mikubwa ni Tiro na Sidoni.
5. Philistina - Jina hili linatoka Palestina kuonyesha Nchi walipewa Waisrael
Yoe.3:4; Ebr. 11: 9; Zak. 2:12.
6. Misri - Nyumba ya utumwa kwa Israel.
a. Nchi yenye rutuba kando ya mto Nili, Mw.12:10; 39:1; 42:1; 47:28;
29; Mdo. 7:23, 24.
Nchi ya Palestina au Kanani.
I. Kanaani ni Jina lililotumika katika A.K. kwa nchi hiyo iliyokuwa katikati ya
Yordani na Mediterania kusini ilipakana na jagwa.
II. Kwa usahihi zaidi tunapozungumzia Palestina twaweza kuwa tunazungumzia mataifa mawili.
A. Nchi ya Wafilisti.
B. Nchi ziliyokaliwa na makabila 12 ya Israeli.
III. Migawanyo Yake ya Asili.
A. Uwanda wa Pwani. B. Ukanda wa katikati. C. Bonde la Yordani.
D. Ukanda wa mashariki.
E. Ukanda wa Jangwa (Mbele ya mashariki).
IV. Maji Yalivyo Katika Nchi ya Palestina.
A. Mto Yordani
B. Ziwa Hula.
C. Bahari ya Galilaya
D. Bahari Iliyokufa.
E. Mito mingine mingi midogo midogo.
V. Milima Ya Palestina.
A. Tabor - Debora na Baraka walitayarisha …. Wakanaani. B. Gilboa - Sauli na Jonathani walikufa vitani na Wafilsti.
C. Karmeli - Nabii Eliya aliwashinda manabii na makuhani wa Baali. D. Ebal na Gerzimu-
1. Baada ya wana Waisraeli kushinda Yoshua …. Amoc na
Musa
2. Baraka zilitangazwa - kutoka mlima Gelizimu.
3. Laana zilingazwa kutoka mlima Ebal, Kum. 11:29.
4. Mwanamke Msamaria, Yosh. 8:33-35, Yoh. 4:1
E. Mlima Sayuni - kwa kawaida Sayuni lilikuwa ni Jina la
Yerusalemu mji mtakatifu.
1. Mashariki mwa Yerusalemu Mlima Olivet au Olivus. (Mlima wa Mizeituni).
F. Mlima Hermon.
G. Mlima Gileadi - Gidioni alikusanya Jeshi (Waa. 7:3) H. Mlima Nebo
1. Mahali Musa alipotazama nchi Ahadi.
2. Uko katika nchi ya Wamoabu.
3. Mahali alipofia Musa.
VI. Njia kuu 3.
A. Njia ya Pwani. B. Njia za majini.
C. Njia kuu za wafalme.
MABABA WALIVYOSAFIRI. Utangulizi:
I. Maelezo ya mapema kabisa ya Biblia kuhusu Maisha ya Mwanadamu. II. Adamu maana yake "Mwanadamu"
III. Biblia inaeleza kuhusu mwanadamu juu mambo kadhaa.
A. Kuumbwa kwake. B. Kuanguka
C. Gharika ambapo vyote hivi vimeelezwa juu ya mwamadamu kama ni jumla.
D. Kuitwa kwa Abraham (Ibrahimu na Uzao wake) E. Rehema inaonyeshwa kwa watu kadhaa.
1. Rahabu, Yos. 2.
2. Ruth, Ruth. 1
3. Watu wa Ninawi, Yona.
IV. Lakini Mungu alitoa ufunuo kwa watu wake Israeli.
Mwili:
I. Kulikuwa na safari Tatu Kwa Mababa Watatu.
A. Ibrahimu
B. Isaka.
C. Yakobo.
II. Ibrahimu:
A. Historia ya Israeli inaanza na Ibrahimu.
B. Akaitwa " Baba wa Imani" Aliondoka Uru wa Ukaldayo kwenda asikokujua.
1. Uru wa Ukaldayo - (Mwa. 11:27-32)
2. Kutoka Uru mpaka Harani. (Mw. 11:27-12:4) Mesopotamia Kusini- ndipo palipokuwa nyumbani Ibrahimu.
3. Kanani - Mwa. 12:5-9 - Ibrahimu na mkewe Sara waliondolewa kutoka Harani. Kutoka harani waliambatana na Lutu Binamu yake- kwenda Kanani iliyokuwa chini ya Misri.
4. Misri, Mwa. 12:10-20.
a. Ibrahimu alienda kutafuta chakula.
b. Ibrahimu aliongopa - Sara ni dada yake.
c. Ibrahimu alifukuzwa na Farao baada ya kugundua. d. Ibrahimu alirudi Betheli.
5. Hebroni - Mwa. 13:5-18.
a. Ibrahimu na binamu yake Lutu walitengana.
b. Lutu alichagua - Sodoma bonde ambalo lilileta baadaye maangamizi ya Sodoma na Gomora.
1. Lilikuwa ni bonde zuri kwa mifugo.
c. Ibrahimu alichukua sehemu za miinuko kuzunguka Hebroni.
1. Hapo ndipo alipokufa mkewe Sara.
2. Alinunua mahali pa kumzika mkewe kwa Efroni Mhiti.
3. Daudi alianza kutawala akiwa Mfalme katika Hebron.
4. Uasi mbaya wa Absolomu ulianzaa hapa.
5. Kwa mara ya pili Ibrahimu aliambiwa hapa kuwa ni
"Rafiki" Mungu.
6. Vita vya wafalme, Mwa. 14.
7. Beersheba, Mwa. 20 - 25.
a. Baada ya maangamizi ya Sodoma na Gomora.
b. Hapa Ibrahimu aliungana na Abmeleki wa Gerali (Mwa. 26: 26
-33).
c. Katika siku za za Ahabu na Jezebeli, Eliya alipata kutoa sadaka hapa baada ya ushindi wake dhidi ya manabii wa Baali, (1 Fal.
19:3-4).
8. Moria - Mwa. 22.
a. Mahali alipotolewa Isaka kama sadaka.
b. Mahali palipokuwa pametulia mbali na mikiki ya shughuli za watu.
c. Mapokeo hudai Ibrahimu alikuwa katika "Nchi ya Moria".
III. Safari za Isaka.
A. Maisha ya Isaka katika Biblia yameelezwa kwa ufupi zaidi kuliko mababa wengine.
1. Beer-Lahai-Rol (Mwa. 16:7, 13; 14; 24:62)
a. Hapa ni mahali Malaika wa Bwana alipomtokea Hajiri kijakazi wa Sara (Mama yake Isaka,) wakati Hajiri anamkimbia mkuu wake.
b. Yawezekana Isaka aliishi hapo.
2. Gerari (Mwa. 26:1-16)
a. Ni mahali ambapo Isaka alipata makaribisho mazuri kutoka kwa
Mfalme wa Gerali Abimeleki.
b. Isaka aliongopa kuwa Rebeka ni Dada yake, mst. 7-11.
3. Rehobothi (Mwa. 26:23-33)
a. Isaka alifanya mapatano ya Amani na Wafilisti chini ya mfalme wao Abimeleki.
b. Mungu anarudia Ahadi yake juu ya Ibrahimu.
4. Hebroni (Mwa. 35:27).
a. Maisha yake ya mwisho aliyatumia akiwa HEBRONI.
b. Ni mahali alipofia na kuzikwa na wanawe Yakobo na Esau katika pango lilelile alilonunua Ibrahimu (makapela).
IV. Safari za Yakobo.
A. Jina lingene la Yakobo ni Isaraeli. B. Baba wa makabila 12 ya Israeli.
MAISHA YAKE YAKO KAMA IFUATAVYO KWA UFUPI.
I. BEER -SHEBA: (Mwa. 26:33 - 27-46).
A. Yeye na pacha mwenzie walizaliwa (Esau)
B. Alidanganya na kupata baraka za uzaliwa wa kwanza watu aliowadanganya watu wawili nao ni:
1. Isaka.
2. Esau.
C. Alikimbilia Harani - Baada ya kugundulika kwa mjomba wake Labani.
II. BETHELI: (Mwa. 28).
A. Alikimbia kulipizwa kisasi na Esau.
B. Alipewa na Mungu maono ya kurudia kwa amani katika nchi aliyozaliwa. C. Aliona ngazi kutoka Mbinguni.
D. Ndama kama mungu iliwekwa na Yeroboam I kuepusha watu kwenda
Yerusalem hekaluni, Ufalme wa Isaraeli ulipogawanyika (Yuda na Israeli).
III. HARANI: (Mwa. 29:30).
A. Alitumia muda mwingi hapo.
1. Alitumia miaka 7 kwa msichana mzuri Raheli badala yake alipewa
Lea ambaye hakuwa anavutiwa naye.
2. Alifanya miaka mingine 7 kwa ajili ya Raheli tena.
3. Alitumia maisha yake Harani kwa kuishi na mjomba wake Labani. IV. MAHANAIMU: (Mwa. 32:1).
A. Alitiwa moyo na malaika baada ya kuogopa kulipizwa kisasi na nduguye aliye mkosea miaka ishirini mapema.
B. Ni mahali ambapo baadaye mwana wa Sauli Ishi - Bosheth alitawala, wakati Daudi akitawala Yuda kutoka Hebroni.
C. Ni mahali ambapo kilitokea kifo cha mateso cha mtoto mzuri sana wa Daudi
Absalomu.
V. PENUELI (Mwa. 32:22 - 32).
A. Penueli maana yake ni "Sura ya Mungu."
B. Alipambana na Malaika, Yakobo alifanywa kilema na kupewa baraka.
VI. SUKOTHI (Mwa. 33:17).
A. Yakobo alipatana na nduguye Esau.
B. Alijenga madhabahu kwa ajili ya furaha ya kupatana na nduguye.
VII. SHEKEMU - (Mwa. 33:18-34:31).
A. Shekemu kwa sasa inajulikana kama - TELL-BALATA. B. Dina binti Yakobo alibakwa na Shekemu.
C. Simeon na Lawi waliwaua wanaume wote wa Shekemu.
VIII. BETHELI: (Mwa. 35:1-15)
A. Jina lingine - "Nyumba ya Mungu."
B. Yakobo alirudia agano lake na Mungu.
IX. EFRATH.
A. Jina lingeni ni Bethlemu (Mwa. 35:16-21). B. Maili 5 kusini ya Yerusalemu.
C. Ndipo alipokufa Raheli wakati anajifungua mtoto Benjamini mtoto wa mwisho wa Yakobo.
X. HEBRON - (Mwa.35:27).
A. Ni mahali ambapo Ibrahimu na Isaka waliwahi kukaa.
B. Mahali ambapo Yusufu mwana mpendwa wa Yakobo aliuzwa na ndugu zake
Utumwani kwa wa Ishimaili.
C. Kulikuwa na njia kutoka Damascus kwenda Misri.
XI. KULE MISRI (Mwa. 45-49)
A. Alikwenda kwa mwaliko wa Yusufu.
B. Yusufu alikuwa waziri mkuu wa Misri.
C. Aliishi katika Gosheni kule Misri - Sehemu ndogo lakini yenye rutuba sana.
D. Mwili wa Yakobo uliowekwa dawa ulihifadhiwa na kuchukuliwa kwenda kuzikwa Hebroni - Makapela.
KINAENDELEA UKIKITAKA CHOTE WEKA EMAIL
Shalom
ReplyDeleteNaomba Full detail yake.