Thursday, May 24, 2018

IJUE HISTORIA YA BIBLIA YAKO!
 NA:MAJOR DERICDADY
email.dericglory@gmail.com
cont:0712412170,0679008354 

WAANDISHI
(Mwanzo, kutoka, walawi, hesabu, kumb/Torati) vimeandikwa na MUSA
Joshua ~Joshua
Waamuzi ~Samweli
Ruthu ~Samweli
1samweli~samweli, Gadi, Nathani
2Samweli~Gadi, Nathani
1Wafalme~Yeremia
2Wafalme~Yeremia
1Nyakati~Ezra
2Nyakati~Ezra
Ezra ~Ezra
Nehemia ~Nehemia
Esta ~Modekai
Ayubu ~#Musa
Zaburi ~Daudi, na wengine
Mithali ~Sulemani, Agur na Lemuel
Mhubiri ~Sulemani
Wimbo uliobora ~Sulemani
Isaya ~Isaya
Yeremia ~Yeremia
Maombolezo ~Yeremia
Ezekiel ~Ezekieli
Daniel ~Daniel
Hosea ~Hosea
Yoeli ~Yoeli
Amosi ~Amosi
Obadia ~Obadia
Yona ~Yona
Mika ~Mika
Nahumu ~Nahumu
Habakuki ~habakuki
Sefania ~Sefania
Hagai ~Hagai
Zekaria ~Zekaria
Malaki ~Malaki
Mathayo ~Mathayo
Marko ~Marko
Luka ~Luka
Yohana ~Yohana
Matendo ~Luka
Warumi ~Paulo
1wakorintho ~Paulo
2Wakorintho ~Paulo
Wagalatia ~Paulo
Waefeso ~Paulo
Wafilipi ~paulo
Wakolosai ~Paulo
1Wathesalonike ~paulo
2Wathesalonike ~Paulo
1Timotheo ~Paulo
2Timotheo ~Paulo
Tito ~Paulo
Filemoni ~Paulo
Waebrania ~Paulo
Yakobo ~Yakobo (ndugu yake Yesu)
1Petro ~Petro
2Petro ~Petro
1Yohana ~Yohana (mtume)
2Yohana ~Yohana (mtume)
3Yohana ~Yohana (mtume)
Yuda ~Yuda (ndugu yake Yesu)
Ufunuo ~Yohana Mtume
************************************************
BIBLIA KWA UJUMLA
Biblia INA Jumla ya vitabu 66
Ina Sura (chapters) 1,189
Ina Mistari (verses) 31,101
Ina jumla ya maneno (words) 783,137
Ina jumla ya herufi (letters) 3,116,480
Ina jumla ya ahadi tulizopewa sisi zilizoko kwenye Biblia ni 1,260
Jumla ya Unabii uliotimia ni 3,268 (verses)
Unabii ambao haujatimia ni 3,140(verses)
Maswali yalioko kwenye Biblia ni 3,294
Jina refu kuliko yote kwenye Biblia ni #MAHERSHALALHASHIBAZI (Isaya 8:1)
Fungu refu kuliko yote ni #Esta 8:9 (lina maneno 78)
Fungu fupi kuliko yote ni #Yohana 11:35 (lina maneno 2)
Kitabu cha katikati kati ya vitabu vyote ni #Mika +Nahumu (vyote vimechangia)
Sura ya katikati katika Biblia yote ni #Zaburi 117
Sura fupi kuliko zote kwa kuhesabu maneno ni #Zaburi 117
Sura ndefu kuliko zote katika Biblia yote ni #Zaburi 119
Kitabu kirefu kuliko vitabu vyote ktk Biblia ni #Zaburi ina sura 150
Kitabu kifupi kuliko vyote ni 3Yohana (kwa kuhesabu maneno)
************************************************
#MNYAMBULISHO
AGANO LA KALE
Agano la kale lina jumla ya vitabu ni 39
Agano la kale liko na sura 929
Agano la kale lina mafungu (verses) 23,114
Agano la kale lina jumla ya maneno 602,585
Lina jumla ya herufi (letters) 2,278,100
Kitabu cha katikati (kwa agano la kale) ni #Zaburi
Sura ya katikati ni #Ayubu sura ya 20
Fungu la katikati ni #2Nyakati 20:17-18
Kitabu kidogo ni #Obadia
Fungu fupi kuliko yote kwa agano la kale ni #1Nyakati 1:25
Fungu refu kuliko yote ni #Esta 8:9 (lina jumla ya maneno 78)
Sura ndefu ni #Zaburi 119
************************************************
AGANO JIPYA
Agano JIPYA lina jumla ya vitabu 27
Agano JIPYA lina jumala ya sura 260
Agano JIPYA lina mafungu(verses)7,957
Liko na jumla ya maneno 180,552
Liko na jumla ya herufi (letters) 838,380
Kitabu cha katikati (kwa agano JIPYA) ni #2Wathesanike
Sura ya katikati ni #Warumi 8:9
Fungu la katikati ni #Matendo 27:17
Kitabu kidogo ni #3Yohana
Fungu fupi kuliko yote ni #Yohana 11:35
Fungu refu kuliko yote ni #Ufunuo 20:4 (ina jumla ya maneno 68)
Sura ndefu kuliko zote ni #Luka 1
************************************************
#BIBLIA
imeandikwa na waandishi 40 (approximately)
Biblia imetafsriwa zaidi ya lugha 1,200 duniani
Imeandikwa zaidi ya miaka 1,600
Imeandikwa zaidi ya vizazi (generation) 40
Imeandikwa kwa lugha 3 (kiebrania, kigreek, na Aramaic)
Imeandikwa katika mabara 3 (Ulaya, Asia na Africa)
Imeandikwa katika mazingira tofauti tofauti kama magerezani, jangwani, ikulu,nyumbani n.k
Waandishi wake walkua na hadhi tofauti tofauti kama Wafalme, madaktari (kama LUKA), wakulima, wavuvi, wakusanya kodi, mitume (kama paulo) n.k
Pia imeandikwa ktk vipindi na hali tofauti tofauti kama, Amani, Furaha, mateso, vifungoni, wakati wa vita, umasikini, uhuru , utumwani pia
***************************************
MENGINEYO
Naandika haya baada ya kuulizwa na rafiki yangu mmoja aliyetaka kujua tofauti ya Biblia ya vitabu 66 na ile Biblia ya vitabu 72. Rafiki yangu alisema hivi '' Kaka Biblia jumla inavitabu vingapi? Wengne wanasema 72 au 66,naomba msaada wako ndugu yangu''
Karibu tujifunze.
Biblia takatifu imeandikwa kwa miaka 1500 na imeandikwa na waandishi 40 ambao waliongozwa na ROHO MTAKATIFU kuandika, Ndio maana unaweza ukashangaa kwa mfano Musa alindika kuhusu uumbaji wa MUNGU, Musa hakuwepo wakati wa uumbaji lakini ROHO wa MUNGU alikuwepo na ndio maana aliwafunulia wanadamu na wakatambua . 2 Petro 1:21 '' .
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa MUNGU, wakiongozwa na ROHO MTAKATIFU. '' Kitabu cha Ayubu ni moja ya vitabu ambavyo viliandikwa zamani zaidi Mwandishi akiwa Musa lakini Musa hakuwepo wakati wa Ayubu, ROHO wa MUNGU alimwambia Mwandishi huyo wa kitabu hicho cha Ayubu.
Ndugu zangu ROHO MTAKATIFU ni wa milele na ndiye msimamizi wa waandishi wote wa Vitabu vya Biblia. 2 Timotjeo 3:16 '' Kila andiko, lenye pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki ''
Unaweza ukaona hapa jinsi MUNGU akimwambia mmoja wa waandishi wa Biblia aandike kile anachoelekezwa na yeye mwenyewe MUNGU Kutoka 17:14-15 '' BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake YEHOVA-nisi; ''
Biblia imedumu sasa kwa zaidi ya miaka 3500. Ni kitabu sahihi pekee maana vitabu vyote ambayo vilikuja baadae vya dini mbalimbali waandishi wake walikopi tu baadhi ya vitu ambayo viko kwenye Biblia na na kuviweka kwenye maandiko yao kwa kuchanganya na uongo ili tu kuhakikisha wanadamu hawaendi uzima wa milele. Jina ''Biblia'' linatokana na neno ''Bablos'' ambalo maana yake ni kitabu cha vitabu.
Biblia sahihi ni ile yenye vitabu 66 Nitatoa ufafanuzi hapo chini.
Agano la kale lina vitabu 39 ambavyo viko katika makundi 5.
1. Vitabu 5 vya Musa au vya sheria.
2.Vitabu 12 Vya Historia.
3. Vitabu 5 Vya Mashairi.
4. Vitabu 4 Vya Manabii wakubwa.
5.Vitabu 12 Vya Manabii wadogo.
Agano jipya lina vitabu 27 ambayo vimepangwa katika makundi 5.
1. Vitabu 4 vya injili.
2. Kitabu 1 Cha Historia.
3.Nyaraka 13 za Mtume Paulo.
4. Nyaraka 8 za Mitume wengine.
5. Kitabu 1 cha Ufunuo.

email.dericglory@gmail.com
cont:0712412170,0679008354

1 comment: