Wednesday, May 23, 2018

         ZIJUE AINA ZA WATU NA TABIA ZAO
                         
      YALIYOMO
i.Shukrani……………………………………………………………………………………………………………… I
ii.Utangulizi…………………………………………………………………………………………………………… II.
             SURA YA KWANZA
1:0 aina za watu na tabia zao……………………………………………………………………..2
    1:1.melancolin na tabia zake…………………………………………………………………..2
    1:2. Mapungufu yao……………………………………………………………………………….2
           SURA YA PILI
2:0. Flagmentic tabia zake na mapungufu yake………………………………………5
      2:1. Mapungufu yao kitabia ………………………………………………………………11
            SURA YA TATU
3:0. Sanguine na tabia zake na mapungufu yake kitabia…………………………14
     3:1. Tabia za sanguine kwa ujumla……………………………………………………………..14
               SURA YA NNE
4:0. Tabia na mienendo ya colerick…………………………………………………………19
    4:1. Colerick  na tabia zake kwa ujumla……………………………………………………….19
    4:2. Mambo ya kuzingatia muhimu kujua……………………………………………………23
    4:3. Nitatambuaje mimi ni wakundi gani…………………………………………………….24






                              
                                                                  SURA YA KWANZA
                                                  1:0  AINA  ZA WATU NA TABIA ZAO
                               MAKUNDI MANNE YA WATU NA TABIA ZAO 
J  ZIFUATAZO NI CATEGORIA MBILI ZA MAKUNDI HAYA MANNE YA WATU
INTROVANT:watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri  na kiakili wanaotafakali mambo kwa kina.
Melancolin    
Fragmenti

EXTROVANTS:Watu wenye uwezo  wa kawaida wa kiakili na hawana tafakari zakina katika  mambo yao
SANGUINE
COLERICK

Na sasa  tuangalie  tabia  za kila  kundi  na mienendo yao  kimaisha wapoje,kiuchumi,kisiasa nk.

                                         
                      
1:1MELANCOLIN 
Watu wa kundi la  kwanza ni (male & female) wanasifa  zifuatazo
Wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence quotient).

Ni wagunduzi  wakubwa wa mambo ya kisayansi duniani.


Wana mudu vizuri masomo ya kisayansi na hesabu.

Ni watu wapole wasio na maneno mengi.


Wanahisia kali za upendo na inasadikika  kuwa ndio kundi linalo ongoza kwa upendo wa dhati.(melancolin akimpenda mtu huwa anamaanisha zaidi katika upendo na uwa hajui kudanganya katika upendo,iwe ni EROS upendo wa mahaba ,Au FILADEFIA upendo wa kirafiki).

Wanajali sana wenzao hasa wanapo kuwa katika shida na matatizo.hawajui kumpuuza mtu anapokuwa katika hali fulani ya maisha wanajua kujali hisia za ndani za mtu.

Wanamaombi wazuri sana kiimani.kwasababu wanajua kuheshimu hisia za wengine hii ndio sababu, ata wanaweza kuwa waombaji wazuri na wa mda mrefu zaidi na wakumaanisha kutokana na tabia zao za asili.


Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa.

Wanajitolea kwa haraka  na kwa dhati kwa mambo ya wengine.


Huondoa uchungu wao kwa machozi(wakiumizwa hulia haraka hasa kwa upande wa  wanawake /mabinti).

Wanapenda  kusoma,kusikiliza na kusimlia mambo yenye tafakari na uchambuzi wakina.kila wanachosoma lazima wamjue mwandishi, na elimu yake wadhifa wa mwandishi umri. wajue chanzo cha uandishi wake kimetokana na uchunguzi gani.(hawapendi umbea).

Wanapotoa mawaidha au mahubiri ama ushauri wengi wanaosikiliza  huwa wanaguswa nao na kubadirika haraka.kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo.

Hawapendi  kuvunja taratibu,sheria za eneo husika.wanaheshimu sana taratibu na sheria za mahali popote watakapofika.

Ni wavumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)

Hawapendi kufatilia mambo ya  wengine pasipo sababu za msingi

Wanaumia sana pindi wanapokosea   ama kushindwa jambo fulani

Wanabusara na hekima nyingi

Niwatu amabao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote

Niwepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine

Kundi linalopenda amani na utulivu

Mara nyingi wanapenda kuonesha sura ya tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa.

Hawapendi kumweleza kila mtu mambo yao binafsi.

Ni kundi lenye marafiki wachache,wao ni wagumu kuwa na marafiki wengi.

Ni waaminifu na wasema ukweli

Wanapenda kusaidia wengine  hata kupita uwezo wao,wanaweza jitolea ata viatu alivo vaa miguuni kumsaidia mtu,hata kama na yeye anacho icho icho kimoja.

Niwaaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani

Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu,(Hata wakimsaidia mtu hawaitaji wawepo vyombo vya habari au mamia ya watu ndo watoe msaada)


Wanahesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa(wanafurahia sana vitendo kuliko maneno,usimpe ahadi nitakununulia gauni ila we nunua gauni atakuhesabu unaupendo wa dhati kwa

    
    1:2.MAPUNGUFU YAO
Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa.mfano akitaka kuanzisha duka badala ya kutafakari itakuwaje nikipata faida ,wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto ,kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamzi wa kuahirisha uanzaji wa mradi huo.

Wanakata tamaa wanapo kosolewa.Akifanya jambo anaogopa sana watu wasimkosoe katika jambo hili maana ukimkosoa anaweza acha kabisa atakama alikuwa na mpango mzuri wa kumsaidia katika maisha yake.

Hawajiamini kwa  mambo wanayo yafanya(hata wakiwa darasani  si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu swali,hata wakijibu mtihani hasa wa maelezo uwa wanakata kata sana maelezo yao maana hawajiamini kama wako sahii na mara zote uwa wanachokiwaza nikitu sahii,ilakutokana na tabia hii upoteza ubora wao wa kiasili na ujuzi).

Wanapenda sana kutiwa moyo kirahisi.Ili wafanye jambo kubwa ni lazima umtie moyo sana kuwa anaweza fanya jambo fulani.


Nikundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya shinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana.

Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe.



Wanajeruhika mioyo yao kirahisi(wakiingiwa na pepo si rahisi kuwatoa kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyoni mwao).Napia ikumbukwe pia wao sio wepesi wa kusamehe.

Wana  aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao.

Nikundi la watu wanaoridhika haraka.Ndio maana maskini sana kwasababu ya kuridhika haraka.

Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka  kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa .

Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiza ndoto kutokana na uoga wa kuanzisha mambo mapya.
  
Wanaogopa sana matatizo,vikwazo na changamoto.

Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano
  mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuhadhibu watoto wao.Wanadekeza sana watoto wao .

Wakati mwingine hupenda kujikataa,huwa na tabia ya kijiona kuwa si kitu mbele za wengine na kujikataa hata katika nini wanafanya.



 Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana)kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari  kila wanachoshauriwa hivyo hijikuta kuwa wanayumba kimisimamo.hata hivyo wanatabia ya kuweka mambo moyoni sana wakiwa viongozi ni rahisi kuugua mara kwa mara matatizo ya moyo maana hawana vifua vya kusamehe mambo mapema).mfano :- kama mkurugezi /mwenyekiti wa eneo fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick.

Kingine kinacho wanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutoweza kuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa(Musa wa biblia alikuwa ni mmoja wa watu wa kundi hili alikuwa hajiamini,anakata tamaa mapema,mlalamishi,asiyeweza kujieleza,licha ya kupewa msaidizi na MUNGU bado tabia zake zilisababisha kukosa nchi ya ahadi.

Kwa upande wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi na kujifungua .hii ni kwasababu wanatunza kumbukumbu za makosa mengi moyoni hawasemi siku zote wanaishi na uchungu.

USHAURI KAMA WEWE NI WA KUNDI HILI
NI MHIMU SANA KUBORESHA YALE MAZURI YAKO MAANA MAFANIKIO YAKO KIUCHUMI NA KIJAMII YAPO KATIKA MAZURI YAKO.NA KUBWA EPUKA TABIA MOJA MOJA AMBAZO NI MAPUNGUFU KWAKO,HUWEZI HEPUKA ZOTE KWA MARA MOJA ILA UNAWEZA BORESHA HAYO MADHAIFU KUWA MAZURI KWAKO.(“TATIZO SI TATIZO ILA UTAKAVO LIANGALIA TATIZO NA KULICHUKULIA TATIZO LINAWEZA KUWA TATIZO” REV.ERIC SIXBERTH.


                


                      





                      SURA YA PILI
2:0.FLAGMENTIC TABIA ZAKE NA MAPUNGUFU YAKE

TABIA NJEMA ZA FLAGMENTIC
Watu wa kundi hili ni male and female
Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini

Mawakili,majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili.(Mawakili wengi mashuhuri duniani ni flagmentic,kutokana na uwezo wao wa kiasili)

Ni watu wanaopenda  kutafiti mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hutawaliwa na mifano na takwimu halisi.


Wanapenda kufatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote,ndio maana wanafaa sana kuwa wapelelezi na wachunguzi.(wanapenda ushushu)

Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili.wale ma FBI wa marekani nusu yao wanatoka katika kundi hili na wana tumia hizi tabia kuwachagua kutokana na tabia zao za asili.



Ni watu wasio umizwa kufanya makosa.flagmetic akikosea sirahisi kumkuta anajutia alichofanya ni ngumu kwake kujuta kwa jambo lolote.Maana hujihesabia haki mda wote hii inawasaidia kutopata magonjwa ya moyo ovyo maana hawajui kubeba mambo moyoni.
Hawapendi kuwaamini wenzao.wao si rahisi kumuamini mtu ovyo nimpaka wamchunguze sana pia wana ubaguzi wa kuamini vya wengine.

Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo  mbalimbali.wanapenda sana hata zawadi za wenzao lakini ni wagumu wao kutoa zawadi.


Wanatafakali mambo kwa kina na kuyatolea uamzi wa uhakika.wanapofanya tafakali juu ya jambo Fulani uwa wanafanya uchunguzi wa hali ya juu sana kabla ya kutolea uamzi wowote.

Mapenzi(love affairs) si kitu kinachowaumiza sana.(kundi linaloongoza kuwa single, na ambao ni rahisi kukubali taraka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao.
Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali jambo(they don’t care).Ukija kumfanyia fujo ni unajisumbua maana ukiondoka ameshakusamehe mapema na kusahau,ni wavumilivu kumvumilia mtu kwa mambo mbalimbali hasa ya kuwakwaza hawajali.

Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera vilevile si rahisi kuziacha imani ama sera walizozipokea.


Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao.Hata wakiongea watu 100 kwa jambo moja uwa hawashituki,hata magazeti yakiwaongea mabaya udharau na kusema wananipa umaarufu.

Ni wasuruhishi wazuri wa migogoro ya kijamii ama kimataifa na wenye   ushawishi wakina (i.e karama ya utele ya neno la upatanisho ipo kwao).


Ni kundi linalo fanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani .wanatabia ya kufanya mambo mengi mfano,akafungua biashara ya nafaka hapohapo akafungua na shule ya watoto chekechea vyote akaviongoza yeye,mafanikio huwa ni madogo kwao.

Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya usuruhishi inapogoma .wanapenda amani kuliko chochote duniani.


Wapo radhi wasalimishe chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace meker).
Wanapenda kutekeleza maagizo ya uso kwa uso wanayopewa kuliko maagizo ya pamoja.Hii inawasaidia kufanya kazi kwa usahii bila kukosea kosea katika majukumu yao.

                                 

                               2:1.MAPUNGUFU YAO KITABIA 
Ni wagumu wa kuomba msamaha i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi,ndio maana  hupoteza nguvu za MUNGU kirahisi(imani zao zikipona huwa si rahisi sana kuamka tena kiimani).

Nimabingwa wa kuharisha mambo(mfano kama akitaka kwenda kupalilia shamba,akafika na kukuta kuwa majani  ni machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msitu wa kupalilia).


Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuayaona kwa macho yao wenyewe.Wanaweza ambiwa kuna vita imetokea wakacheka tu nakupuuza ila akisikia kutoka kwa chanzo ndio huamini jambo hilo.
Hawapendi kusifia ama kukubali kazi za wenzao.(Hawa wanaongoza kuvunja wenzao moyo katika mambo mbalimbali. Hata ukianza biashara watakuvunja moyo mapema sana kuwa utafirisika.

Nikundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea.(kwenye mahusiano wana achika kwasababu ya ubishi wao,maana anachokiamini yeye ndio sahihi pekee).


Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi(anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kwa shingo upande.)

Sio watu wanao jali muda na ratiba.unaweza panga nae tuonane saa 6 akaja saa 8 na hajali ata kutoa sababu kwanini kachelewa kufika eneo husika.


Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yoyote pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.

Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani.Ukimkosea kukuumbua ata angalia mahari ni hapohapo anakueleza ukweli hajali iwe umedhalilika ama laha.Kama ni mwanaume humuabisha mkewe hadharani mbele za watu.


Ni kundi la watu wasio wakereketwa wa maswala ya usafi na unadhifu(i.e kimavazi na kiutaratibu)
Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala  wasiumizwe na kukwama huko.

Watu waliojaa dharau na majivuno mengi,wanajiona bora kuliko wengine katika mambo yote.


Hawapendi kuelezwa na viongozi wao na mara nyingi huwadharau viongozi wao.Mtu wa aina hii akiwa msaidizi wa boss, ni hatari sana maana anaweza yeye kuwa boss ama yeye akafukuzwa kazi maana siku zote atakuwa anapingana na boss wake.
Wakiwa viongozi wanajikuta wanachukiwa na watu hasa pale wanapokataa kujari matakwa ya wanao waongoza. 

     USHAURI KAMA WEWE NI WA KUNDI HILI
NI MHIMU SANA KUBORESHA YALE MAZURI YAKO MAANA MAFANIKIO YAKO KIUCHUMI NA KIJAMII YAPO KATIKA MAZURI YAKO.NA KUBWA EPUKA TABIA MOJA MOJA AMBAZO NI MAPUNGUFU KWAKO,HUWEZI HEPUKA ZOTE KWA MARA MOJA ILA UNAWEZA BORESHA HAYO MADHAIFU KUWA MAZURI KWAKO.(“TATIZO SI TATIZO ILA UTAKAVO LIANGALIA TATIZO NA KULICHUKULIA TATIZO LINAWEZA KUWA TATIZO” REV.ERIC SIXBERTH.



  SURA YA TATU
3:0.SANGUINE  NA TABIA ZAKE NA MAPUNGUFU YAKE KITABIA

Sanguine hawa ni extrovants,yaani wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakali ya kina katika mambo yao.

3:1.TABIA ZA SANGUINE KWA UJUMLA
Watu wa kundi hili ni male and female
Wana uwezo wa kawaida kiakili (muda mwingine mdogo).
Ni wacheshi sana.

Watu walio na maneno mengi wasio pumzika kuongea.sanguine anaweza ongea ata masaa 6 anahutubia tu achoki kuongea.

Wanajisikia raha sana pale wana pokuwaa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza.starehe kubwa kwa sanguine ni maongezi na kusikilizwa bila maswali mengi juu ya hoja zake .

Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya watu wengine.hawana siri hata juu ya mambo ya ndani.mfano anaweza kukuadisia jana aligombana na mke wake nayeye  alipigwa makofi mengi.

Waigizaji wa kuchekesha wengi wanatokea kundi hili.mfano kama kina mr.been,kingwendu,eric omondi wale ni sanguine pure.

Wanapenda sana kujisifu ata katika mambo yasiyo na mhimu .mfano unaweza mkuta anasema jana nililala na mke wa Fulani jambo ambalo ni aibu kwa jamii kusema na kutangaza.

Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya .mfano wakina diamond mwimbaji wa nyimbo,kila anachofanya anaweka mtandaoni ata wakienda chooni wanatangaza kwenye mitandao.

Wanavipaji vingi vizuri lakini wanaitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndio huvionyesha.pindi ukimsifia ni kama gari limewekewa mafuta linapata uhai mpya wa kutembea hata wao ukiwasifia sana juu ya jambo Fulani uwa wanafanya maajabu katika hilo jambo.

Wana hisia za zima moto(i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka .ikitokea ajali huwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kuanza kutoa msaada lakini akiondoka pale ana sahau kila kitu hata kama ametumwa kuleta gari ya wagonjwa.anaweza kuacha na kufanya shughuri zake nyingine.)

Muda wote wako nadhifu(ni wakeleketwa wa maswala ya usafi na unadhifu).uwezi wakuta wanatembea wachafu hata akiwa nyumbani uwa ni wanadhifu sana.

Wanakiherehere  sana.kwenye kila jambo huwa na kieleele sana.

Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau.ukimfundisha jambo ni lazima uongee kwa mifano mingi ili kuiteka akili yake kuelewa jambo husika.

Nivinyonga katika tabia zao(wanauwezo wa kuigiza  tabia zisizo zao kiuhalisiana watu wasio wajua wasi wagundue kiurahisi).

Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini pia wepesi kuyaacha .


Wasichana wa kundi hili si wepesi kuwarubuni kimapenzi ,kwa silaha ya maneno kwani wao wana maneno mengi sana.wasichana wakundi hili ni waongeaji sanaa.

Ni kundi linaroathiriwa sana na love affairs(i.e wao ni multiple lover s ni kawaida kumkuta  sanguine akiwa na mpenzi zaidi ya mmoja.inasemekana na mambo yao mengi na ufundi wao wakuigiza hisia na tabia wavulana na wanaume wa kundi hili huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa).

Wakiwa katika jamii upendwa na kukubalika sana kutokana na ukarimu wao na ucheshi wao.

Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwakujionesha.hata wakitoa msaada lazima waite wandishi wa habari ili jamii yote iwaone kuwa wametoa msaada kwa watoto yatima.

Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wa kukubarika kiurahisi.

Ni kundi la wainjilisti wanaongoza kwa kuwarudisha kondoo wengi kwa BWANA (wengi wana karama ya kuhubiri kwa mvuto na ushawishi wa pekee).

Hawaumii wanapokosolewa ama kukosea jambo.

Ni kundi la watu waoga sana(kimaneno wanajiamini sana kimatendo ni kunguru).wanaweza kumtisha mtu kwa maneno mpaka mtu akakimbia lakini kwenye vitendo wao ni wepesi kukimbia ama kukana maneno yao.

Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji).ukimuadisia jambo kesho unalikuta kachapisha kwenye gazeti la mtaani unapoishi.

Wanapenda kujaribu kila jambo linalo kuja mbele yao.kila jambo linalokuja kuja kwao uwa wanajalibu mfano:-wakimuona msanii mfulani wa nje ya nchi kanyoa hivi au kusuka hivi wao huwa wakwanza kuiga zile staili zao.

Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko watu wengine.

Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine .

Hawana aibu hata mbele ya watu wasio wafahamu wala kuwajua .

Wanaume wa kundi hili wanaamini walizaliwa kwaajili ya kuwasaidia wanawake.ndio maana wanaweza kuwa na wanawake wengi sana

Ni wavivu wa kufanya kazi ,wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zime watawala(wanapenda kuwaza jinsi ya  kupata bahati nasibu ,kuzawadiwa fedha na kuokota fedha  ama madini).

Ni watu wasiojua kupanga na kumudu bajeti kwa ustadi.ni watumiaji wa baya wa fedha zao.

Ni watu wa mipango isiyo ona mbali wakurupukaji.(minister’s of emmergency affairs).

Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kiurahisi na kwa dhati).


Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na baadaye huwa maarufu sana.



Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
Mfano:- Ni petro mtume wa biblia alipenda kujaribu kila kitu (alipomwona YESU anatembea juu ya maji alitaka nayeye kufanya hivo).
           :-Alipenda kufahamu kila kitu aliuliza juu ya habari za siku za mwisho.
           :-Alipenda kujionesha kuwa ni jasiri alihaidi kuteswa na YESU.
           :-Alikuwa ni muoga sana alimkana Yesu mara 3 kwa kuhofia kuteswa            na wayahudi.
           :- Alikuwa mwijiristi wa kutumainiwa (alihubiri siku ya pentekoste).
           :-Alikuwa mwepesi wa kukubali pindi alipokuwa anakosolewa  alikiri makosa baada ya kuonywa na paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasio tahiriwa.






     USHAURI KAMA WEWE NI WA KUNDI HILI
NI MHIMU SANA KUBORESHA YALE MAZURI YAKO MAANA MAFANIKIO YAKO KIUCHUMI NA KIJAMII YAPO KATIKA MAZURI YAKO.NA KUBWA EPUKA TABIA MOJA MOJA AMBAZO NI MAPUNGUFU KWAKO,HUWEZI HEPUKA ZOTE KWA MARA MOJA ILA UNAWEZA BORESHA HAYO MADHAIFU KUWA MAZURI KWAKO.(“TATIZO SI TATIZO ILA UTAKAVO LIANGALIA TATIZO NA KULICHUKULIA TATIZO LINAWEZA KUWA TATIZO” REV.ERIC SIXBERTH.







                                          



                                
                                       SURA YA NNE

                    4:0.TABIA NA MIENENDO YA COLERICK
4:1.COLERICK NA TABIA ZAKE KWA UJUMLA
Wana uwezo wa kawaida kiakili
Ni wakali na wakaidi,hawa ni tabia ya kuu kuwa wakali ata nyuso zao hazina tabasamu la kutoka moyoni,wanaweza tabasamu huku kwenye paji la uso amekunja ndita.

Hawana huruma wala unyenyekevu.kiwaida colerick sio wanyenyekevu katika mambo yote utumia force na nguvu kubwa.


Wanapenda kuwatawala  wenzao muda wote.mfano mkiwa darasani hata kama sio kiongozi atakuwa ndie “final say” wa darasa kutokana wanapenda sana utawala.
 
Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa.hawaitaji nguvu kubwa kujifunza uongozi maana wanazaliwa wakiwa na tabia asili za uongozi.


Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa.wakianzisha biashara yoyote,uwaza baada ya miezi mitatu nitakuwa na biashara 3 kupitia biashara hii,hata kama alipo hapana matumaini ya biashara hiyo.

Watu wasiokata tamaa  mapema.ni vigumu sana wao kukata tamaa katika jambo lolote wanalofanya hata kama kasha shindwa bado atajipa moyo ameshindwa.


Wanajiamini kupita kiasi.

Hawana uoga ni majasiri sana. huwezi mkuta anaogopa kitu ata kama kaona nyoka mkubwa sana atakuwa wa kwanza kumshambulia huyo nyoka.

Hisia zao za upendo azionekani kiurahisi.hawajui kutongoza wanawake kabisa.


Kundi la watu wenye nguvu nyingi.watu wenye nguvu nyingi duniani ni colerick,watu kama kina samson,mike tyson.

Ni madikteta.hii uonekana wazi kwao maana matendo yao mengi ni ya kidikteta sana.


Hawapendi kabisaa kupingwa wala kukosolewa.hata kama akiwa ni mtoto unaweza shangaa ukitaka kumhadhibu anapandisha hasira za ajabu mpaka anabadirika sura,maana hawapendi kupigwa ata kama amekosea kweli.

Watu wa kuripiza visasi.ukimkosea leo kesho analipiza kisasi kwa aina yoyote ile.


Watu wavitendo kuliko maneno.wanapenda vitendo kuliko maneno.hata wapenzi wao hunufaika sana kwa zawadi nyingi na za dhamani.

Wanapenda dhuruma na ubabe (waonevu).


Ni watu wa kurazimisha mambo ata kama hayawezekani.ndio maana hutumika sana kwenye kuanzisha mapinduzi mahari popote,maana hata kama wanachotaka kufanya hakiwezekani wao hulazimisha mpaka kinawezekana.

Huwa wanatumiwa sana kwaajili ya kuzima ghasia uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani  mahari Fulani.


Wanafaa sana kuwaongoza watu hasa kwa sera zao za ushawishi wenye mlengo wa kiukandamizaji.viongozi wengi bora duniani ni colerick,hata waasisi wa mataifa mengi duniani ni wa kundi hili.


Hawajui kubembeleza.kubembeleza kwao ni mwiko ata kama wanaumia moyoni hawajui bembeleza katika jambo lolote.


Hawaongei wala cheka ovyo.mkikaa nao katika kikao uwa wana ongea mwishoni mkimaliza kuongea wote, maana wana amini mawazo yao huwa ndio hitimisho la kikao.uwezi wakuta wanacheka ovyo ovyo.

Wanapotenda jambo uwa wanawaza namna ya kufanikiwa atakama alimsaidia mtu uwa anawaza namna ya kurudisha alichokitumia.
Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kudhubutu kutenda mambo na kuto ogopa hasara.wakina donald trump,geogre bush,billy gate,benjamini mkapa ni wa kundi hili.

Si watu wanaopenda suluhu za amani.hawajui suruhu za amani ukiwachokoza kama ni mtawala vita mtapigana ata kama haihusu taifa atalazimisha tu mpigane vita.


Unadhifu na usafi wao ni wa wastani.

Hawapendi starehe kwa wingi.hawapendi kupoteza pesa yao katika starehe kabisa.


Ni watu wanaoweza kufurahi mazingira yenye dhiki na shida.

Siki zote uwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistolia ili wakumbukwe  hata baada ya kufariki.


Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi,matukio na filamu zilizosheheni ukatili za kutisha.
Mfano wa watu katika kundi hili:- iddi amini,hitler,bush nk



SI  TABIA  ZOTE  ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA







      USHAURI KAMA WEWE NI WA KUNDI HILI
NI MHIMU SANA KUBORESHA YALE MAZURI YAKO MAANA MAFANIKIO YAKO KIUCHUMI NA KIJAMII YAPO KATIKA MAZURI YAKO.NA KUBWA EPUKA TABIA MOJA MOJA AMBAZO NI MAPUNGUFU KWAKO,HUWEZI HEPUKA ZOTE KWA MARA MOJA ILA UNAWEZA BORESHA HAYO MADHAIFU KUWA MAZURI KWAKO.(“TATIZO SI TATIZO ILA UTAKAVO LIANGALIA TATIZO NA KULICHUKULIA TATIZO LINAWEZA KUWA TATIZO” REV.ERIC SIXBERTH.



4:2 .MAMBO YA KUZINGATIA MUHIMU KUJUA.
KILA MTU AMEZALIWA NA TABIA FULANI ZINAZO MFANYA AWE KATIKA KUNDI FULANI
HUWEZI KUJIBADILISHA KUNDI
KUJIFAHAMU KUNDI LAKO KUNAWEZA KUKUSAIDIA KUREKEBISHA  MADHAIFU ULIYONAYO NA KUIMARISHA MAZURI ULIYONAYO PIA AINAKUSAIDIA KUWATAMBUA WATU WENGINE NAMNA GANI YA KUISHI NAO.
INAWEZEKANA KABISA KUJITAMBUA UPO KUNDI GANI KWA KUSOMA NA KUTIZAMA NI RAHISI KUTAMBUA MAKUNDI YA WENGINE.







4:3.NITATAMBUAJE MIMI NI WAKUNDI GANI.
Watu wengi wanatabia za makundi zaidi ya moja.
Kwa wale tabia zaidi ya asilimia themanini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure(ie pure sanguine ect).
Kama unatabia kutoka kundi zaidi  ya moja unaunganisha majina ya makundi mawili yenye tabia nyingi zaidi,unaanza jina la lile  lenye asilimia nyingi zaidi.
   Mfano flag-colerick,cole-flagmetic,sangu-melacoline,melaco-sanguine
























No comments:

Post a Comment